Saturday, 29 January 2022

ZITAMBUE SIKU MAALUMU KUPATA UJAUZITO NA SALAMA ZISIZOTUNGA MIMBA

Menstruation_Circles: Mzunguko wa kila mwezi "Siku salama na siku za hatari kwa mwanamke kuweza kupata ujauzito" Katika mzunguko wa mwezi kwa kila mwanamke, umegawanyika katika pande tatu.
1, Mzunguko mrefu wenye siku35. 2,
Mzunguko wa kawaida siku 28. 3,
Mzunguko mfupi siku25.

Mfano: MZUNGUKO WA KAWAIDA SIKU 28: Kwenye pande hizo zote3, mzunguko umegawanyika katika "Siku salama (Pichani rangi ya Zambarau); Siku za hatari (Alama ya kijani) na siku za hedhi ambazo kimsingi ni siku2 hadi7 (alama nyekundu pichani) KiBiolojia, kwenye siku zenye alama ya kijani" Hizi ni siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga atapata ujauzito bila wasiwasi wowote labda kama ana matatizo ya uzazi ambayo huweza kupelekea, binti au mwanamke husika ashindwe kupata ujauzito licha ya kuwa katika siku hizo.

-Sababu nyingine, kama Mwanamke yu-salama basi tatizo pia huweza kuwa ni kwa mwanaume wake kuwa na tatizo la uzazi pia. Swali ni kuwa je! Utazijuaje siku hizo za hatari? Kwanza kabisa, ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako kama nlivyoainisha awali, ambapo kuna mzunguko mrefu, mfupi na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko ambao watu wengi wanao. Unajuaje mzunguko wako? Hesabu siku tangu siku ile ya kwanza uliyoona siku zako za hedhi mpaka siku moja kabla ya kuona siku zako za hedhi zinazofuata.

(Unashauriwa uchukue miezi mitatu mpaka sita ukihesabu ili uwe na uhakika kwamba mzunguko wa tarehe zako haubadilikibadiliki, na kama umeshahesabu tayari na unafahamu vyema kabla ya kusoma makala hii twende sambamba) Mfano umeanza kuona siku zako tarehe moja mwezi wa nne alafu siku zako zingine ukaziona tarehe 29 mwezi wa nne, chukua 29 toa 1 utapata 28.. maana yake wewe unamzunguko wa siku 28.

Je! siku za hatari ni zipi? Siku ya hatari ni siku ya 14 kabla ya kuona hedhi inayofuata na sio siku ya 14 baada ya kuona hedhi iliyopita na hapa ndio watu wengi wanachanganya na kupata ujauzito / mimba. Pichani:

Mfano kama mzunguko wako ni wa kawaida siku 28, chukua 28 toa 14 utapata 14, Hivyo siku yako ya hatari ni siku ya 14, lakini kwa kua mbegu ya kiume inaweza kuishi mpaka siku tano na yai la kike linaweza kuishi mpaka masaa24 ndani ya mfuko wa uzazi basi siku nne kabla na siku moja baada ya siku ya14 kwenye mzunguko wako ni hatari kushika mimba (ufafanuzi chini) Kama mzunguko wako ni mrefu labda siku 35 basi chukua 35 toa 14 utapata 21, Hivyo siku ya 21 ni hatari na zingine ni 17, 18,19,20, [21] na 22.

Kama mzunguko wako ni mfupi, mfano mzunguko wa siku 21, sasa ukichukua 21 ukatoa 14 unapata 7 yaani siku ya saba ni siku yai linashuka hivyo ni hatari kwa huyu mtu kupata ujauzito, na hivyo siku zingine za hatari kwa mtu huyu ni kuanzia siku ya 3, 4, 5, 6, [7] na8.

Kama mzunguko wako ni wa kawaida yaani siku 28 sasa chukua 28 toa 14 unapata14 yaani siku ya 14 ndio hatari zingine ni siku ya 10,11,12,13, [14], na15.

Dalili kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi? Kuongezeka kwa joto la mwili kidogo, kuwa na hamu ya tendo, na kupata ute-ute mweupe kutoka sehemu za siri.

MWISHO: Maelezo hayo hapo juu yanaweza kusaidia kupanga uzazi, kuchagua jinsia ya mtoto au kutafuta mtoto wa jinsia uitakayo.

Lakini pia tarehe zote nilizoweka mabano [..] ambazo ndio tarehe yai linashuka ndio za mtoto wa kiume zingine zote zilizobaki ni za watoto wa kike "xx", kwa sababu kibaolojia mbegu ya jinsi ya kiume yenye "y" hua ikichelewa kurutubishwa hufa, na sababu za kufa, huweza kufa kwa tindikali liyopo sehemu asilia ya uzazi wa mwanamke, au kukaa muda mrefu bila yai kushuka eneo la urutubishaji.

KWA MSAADA ZAIDI: Waone WATABIBU wa Afya, kwenye Vituo vya afya karibu na wewe kwa ushauri bora zaidi kwa ajili ya kupanga uzazi, kuwa na Afya bora, pamoja na maswala yote yahusuyo Afya ya Uzazi.

Subscribe hapa (MeenaTzNews ) kama bado na Share taarifa iliyokupendeza ili wengine nao wapate elimu na maarifa zaidi utakayoyapata wewe.
"AKHSANTE"

No comments:

Post a Comment