Sunday, 20 May 2018

ZIFAHAMU FAIDA NYINGI TOFAUTI ZA ULAJI WA MATANGO KATIKA MWILI WAKO



 

HEBU LEO TUANGAZIE KUHUSIANA NA MATANGO:
Watu wengi tunapenda kula baadhi ya matunda flani tu, labda kutokana na ladha yake na kuyabagua mengine kutokana na kutokuwa na ladha unayoihitaji, haswa wengi mkipenda ladha yenye utamu-utamu.
Lakini hasara zake kuna baadhi ya vitamin na faida lukuki unazikosa kwa kutokula baadhi ya matunda mengine ambayo haya hauyapendelei kuyala kutokana na uchachu wake, au kutoyazoea katika milo yako ya kila siku.

Katika makala ya leo, Hebu tuangazie faida za kula matango (Tango),

TANGO: Asili ya kilimo cha matango inaaminika kuwa ilianzia kaskazini magharibi mwa India ambako yamekuwa yakilimwa kwa zaidi ya miaka thelathini sasa, Hata hivyo kwa sasa, matango, hustawishwa katika sehemu nyingi za kitropiki.
Matunda yake hukatwa katwa na kuliwa kama achali, au kachumbari, au huwekwa kwenye siki na pia hupikwa na kuliwa.
Katika nchi yetu ya Tanzania matango hulimwa kwa wingi katika mikoa mbalimbali kama vile: Tanga, Morogoro, Mbeya, Lindi, Mtwara na Pwani ambako kuna jua la kutosha, na Pia mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kilimo cha matango hukubali vilevile.
Tango (cucumber in English) ni zao muhimu katika mazao ya mboga na matunda nchini Tanzania na hata nje ya Tanzania, kwani licha ya kuwa ni zao la biashara pia ni zao la chakula.
Hili ni tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo, na kama ilivyo kwa mboga kuwa muhimu kwa afya ya binadamu, Ndivyo Matango nayo yana faida nyingi mbalimbali kw mlaji.
Kwa mkulima hulifahamu vyema Tango. Ikiwa Tunda hili huwa na umbo refu hadi kufikia sm 15, na Matunda yake hukatwakatwa na kuliwa kama achali au kachumbari, pia huweza kuwekwa kwenye siki au kupikwa na kuliwa.
Ukuzaji wa matango huwa njia ya kuongeza mapato kwa mkulima na kwa muda mfupi sana, pia husadia kurutubisha ardhi kwa majani yake na mizizi yake kama ilivyo kwa mkunde.
FAIDA YA KULA MATANGO KWA BINADAMU:
1-KUONDOA HARUFU MDOMONI

Matango huondoa bakteria zinazofanya mdomo kunuka. Ili jambo hili litendeke unafaa kukata pande ya matango na kuweka mdomoni kwa dakika zisizopungua tano ukiwa umekaa kimya (Pasipo kuongea) ili iweze kutenda kazi au kuksaidia. Unafaa kuruda jambo hili mara tatu kila siku.

Mbali na kuswaki, Madaktari husema kuwa, Ulaji wa matango husaidia kuodoa joto jingi tumboni ambayo hua ndio sababu kuu ya mdomo kuwa na harufu hiyo mbaya.

2- KUPUNGUZA MAWAZO
Watu ambao hutumia mafikira sana katika kazi zao, hushauriwa kula matango kila siku kwani yana vitamini B, pamoja na B7, B5, B1 ambazo kwa pamoja hizo husaidia kupunguza mawazo mengi au (stress)

Na kwa Watumiaji wa pombe, au wanaofanya kazi nzito (za kutumia nguvu zaidi) huweza kuondoa hangover kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.

3- HUSAIDIA KATIKA UREMBO
Matango husaidia kulainisha ngozi ya mwili, kwa kina dada Unapokula matango nywele zako hupunguza kukatika, kuwa na afya bora na huweza kumea kwa haraka, Lakini pia matango hutumika kuondoa umbo la duara ambalo hupatikana machoni, kuondoa macho mekundu na kuwa meupe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.
 
(unafaa kufunga macho na kuekelea kipande cha tango juu yake kisha kusubiri kwa masaa kadhaa kila siku au waweza kuyafunga machoni usiku na kulala nayo hadi asubuhi kwa siku kadhaa – matokeo utayapata)
 
Unaweza kuyaponda matango na kupaka usoni, kisha kuacha kwa dakika ishirini ili kulainisha uso na baadaye kuosha uso, jaribu utajivunia sasa.
 
4- HUTUMIKA KUONDOA SUMU MWILINI (Tango ni chanzo kizuri cha maji navitamin B
 
Tango huupa mwili maji ya kutosha na vitamin B zote. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
 
Unaweza kutengeneza kinywaji cha matango na matunda mengine kwa kuchanganya na mboga au matunda mengine kama limau na machungwa ili kuondoa sumu ambayo hupatikana mwilini, iliyojirundika baada ya muda mrefu.
 
5- HUSAIDIA KATIKA UBONGO NA KUTIBU KANSA
 
Matango hua na vitamini ambazo husaidia kukumbuka mambo kwa haraka, na kuchochea uwezo wa kutunza kumbukumbu. Unashauriwa upendelee kuwapa watoto wako matango kuchanganya na ndizi mbivu hiyo itawasaidia kuwa na akili na kufanya vizuri darasani na katika shughuli mbalimbali za kibunifu.
 
Tango lina virutubisho kama Lariciresinol, Pinoresinol na Secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
 
FAIDA NYINGINE ZA JUMLA:
 
Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

(Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo
Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure).
Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari.
Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho Sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu.
Tango lina kiwango kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure.
Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue).
Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).
Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango  kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji.
Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu.

KIUNDANI KUHUSU MMEA WA MTANGO HAPA: CUCUMBER
 
AINA ZA MATANGO: Zipo aina nyingi sana za matango ambayo hulimwa duniani lakini kuna aina kadhaa za begu za matango ambazo zimefanya vizuri hapa Tanzania nazo:
- Palmetto.
- Chicago
- Straight 8
- Colorado
HALI YA HEWA NA UDONGO: Matango hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto kidogo pia hustawi.
Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C – 25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi husababisha magonjwa kwenye majani na maua.
Kwa ustawi mzuri wa matango, udongo unatakiwa kuwa na rutuba ya kutosha, na chachu ya kuanzia 5.5 hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa ni kuanzia mita 1000-1200 kutoka usawa wa bahari. Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji.
Tofauti na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu maua na matunda, au mmea kwa ujumla.
UPANDAJI WA MATANGO Upandaji Zipo aina mbili za upandaji, 1.ya kwanza ni ile ya kupanda mbegu moja kwa moja na 2. ya pili ni ile ya kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10.
Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi. Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei itatumika Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda.
Matango huhitaji kupandwa wakati wa jua. Huu mmea unahitaji joto na maji mengi. Mbegu hupandwa kivyake kwanza karatasi lililo na mchanga na kutunzwa kabla ya kupandwa shambani. Mara nyingi matango hupandwa moja kwa moja shambani. Wakulima wengine hupanda kwenye vitalu au makopo na baadae kuhamishia miche inapofikia sentimita 8-12. Endapo mbegu zimepandwa shambani moja kwa moja, inatakiwa ipunguzwe na kubakia mche mmoja tu kwenye kila shimo.
Baada ya wiki moja mbegu zako zitaanza kuota, endelea kunyunyizia maji kila siku na baada ya wiki mbili hadi tatu mimea itakua na kuanza kutaka kutambaa. Mbegu hiyo humwagiliwa maji mara kwa mara kwa wiki tatu. Baada ya wiki tatu mmea huwa umetokea kwa mbegu hiyo hivi basi ni sawa kuupeleka shambani.
Kabla ya kupeleka mmea huo shambani, hakikisha kuwa umechagua pahali ambapo pana jua. Hakikisha mchanga huo una rutuba nyingi, ni vyema kumwita mtu aliye na ujuzi wa mchanga ili kukueleza kama mchanga huo unaweza kuzwa matango.
NAMNA YA UPANDAJI WA KISASA:
Changanya rutuba na mchanga hadi inchi nane chini. Weka mimea yako midogo ukihakikisha umezitofautisha kwa inchi kumi na mbili. Unapopanda mimea hakikisa umefunika mchanga na neti ii kuzuia wanyama au wadudu ambao hula mmea mdogo.
Hakikisha umeangalia mmea wako kila siku. Ili kupma kiwango cha maji ingiza kidole chako kisicho na maji mchangani kila siku, unapoona kuwa hakina maji katika mgawanyo wa kwanza wa kidole chako basi mimea yako inahitaji maji.
Wakati mzuri wa kunyunyuzia maji ni wakati wa asubuhi au masaa ya mwanzo wa mchana. Unaponyunyizia mmea huo hakikisha kuwa hununyizii matawi yae bali mchanga. Ni vyema kuchunguza kiwango cha maji kwani matango yasiyoshughulikiwa na maji huwa na ukali kiasi unapoliwa.
NAFASI: Nafasi kati ya mche na mche ni sentimita 60-70, na nafasi kati mstari na mstari ni sentimita 70-90. Mimea inatakiwa iwekewe miti ili iweze kuzaa matunda mengi na kuepuka kukaa chini ambapo matunda yanaweza kuoza au kuharibiwa na wadudu.
MBOLEA: Mbolea ni muhimu sana, kabla ya kupanda au kuhamisha miche. Mbolea inayoweza kutumika ni samadi au ya viwandani isiyokuwa na madhara kwa mazingira na afya ya binadamu. Baada ya kupanda, tumia mbolea ya maji maji kila baada ya siku 14-21, mpaka mmea uweke matunda.
Jambo la kuzingatia ni kuongeza rutuba katika mchanga. Baada ya kuongeza rutuba na kabla ya kuweka mmea katika mchanga, unafaa kungoja hadi wiki moja iishe kisha uongeze rutuba kila baada ya wiki tatu. Unaweza kuongeza rutuba ya mimea ambayo imeoza na kuchanganya na vyakula ambavyo umeviweka hivi basi vinaoza.
Rutuba nyingine ambayo unaweza kutumia ni kemikali unazonunua dukani, aina hii ya rutuba inafaa kuangaliwa kuwa kiwango chake cha nitrogen kiko chini nacho kiwango cha potassiumu kiko juu. Rutuba huwekwa kwa changa kando ya mmea, Unaweza kuweka ikiwa katika njia ya maji maji au mchanga mchanga.
Hakikisha kuwa hujaweka rutuba nyingi zaidi ya ile inayofaa  kwani jambo hili husababisha mmea kutoongezeka katika urefu. Pia waweza Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda na kisha tumia NPK yenye uwiano mmoja kama, 18:18:18, 17:17:17 ama 16:16:16 baada ya wiki tatu toka Usegekaji. Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza.
PALIZI: Palizi ni muhimu , ili kuepuka magonjwa na kunyang’anyana chakula kati ya zao na magugu. alilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Njia nyingine ni matumizi ya plastiki maalum kuzuia magugu yaani ‘plastic mulch’
Baada ya mmea kufikisha inchi nne, kata pande zake ambazo hazina maua. Unafaa kuweka majani kwa mchanga ili kuzuia mchanga usipoteze maji ambayo yanahitajika na mimea yao. Ni vyema kunyunyizia matango na maji ya sukari ili kuhakikisha nyuki zinafika kwa mimea hiyo na kuongeza maua.
Kuna uwezekano kuwa matango yako yasitoe matunda kwani maua yote ni ya aina ya kiume, ili matunda yatokee inafaa maua ya aina yote ya kiume na kike yawe yakimea pamoja. Unafaa uwe na uvumilivu kwani jambo hili laweza kuchukua muda kabla ya kutendeka. Kuchelewa kwa matunda kunaweza kusababishwa na kutowasili kwa nyuki katika mimea yako pengine kwa ajili ya hali ya hewa au baridi. Ndiposa unashauriwa kupanda matango wakati wa jua. Sababu nyingine ni kuwa umenyunyizia dawa ya kuwauwa wadudu.
MATANDAZO (MULCHING) Baada ya kupalilia na kuweka mbolea weka matandazo (mulch). Mkulima anaweza tumia nyasi au mabaki ya mimea mingine kufunika ardhi, baada ya miche kutambaa kwa kiasi unaweza weka matandazo kwaajili ya kuzuia upotevu wa unyevu, kupunguza uotaji wa magugu na pia matandazo yakioza huongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko.
Kita miti (staking) ya kupandia: Chomeka miti ya kupandia matango yanayotambaa. Hii husaidia matango yanayotambaa kupanda kufuata miti uliyoikita/chomeka. Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza.
UCHAVUSHAJI. Hii ni muhimu sana kuzingatiwa kwani tango huchavushwa kwa wadudu na si upepo, Bila wadudu kama nyuki uzalishaji huathrika sana, Ni muhimu kupanda mazao kama alizeti na maua mbali mbali yanayopendwa na wadudu wachavushaji ili kuhakikisha uwepo wa wadudu hao shambani.
Aidha inapolazimu ni vema kuweka mizinga kadhaa ya nyuki katika shamba la tango Matumizi ya viuatilifu Katika udhibiti wa wadudu na magonjwa matumizi ya viuatilifu yafanyike kwa maelekezo ya wataalam.
MAKALA KWA MSAADA WA:
Wikipedia
Anzisha project: (Here)
Tiba asilia (Natural Herbs


No comments:

Post a Comment