Friday, 27 October 2017

JE! WAJUA MUZIKI ULIOCHANGAMKA WABAINIKA KUINUA UWEZO WA KUBUNI?


Kujitambua ndio njia sahihi ya kuelimika na kufuta maadui watatu: Umaskini, Ujinga na Maradhi, ambapo ujinga huo ufutwa kwa kujiwekea taratibu za kusoma vitabu, kufuatilia wengine wanafanya nini na kuamua wewe ufanye nini.


NA:
      Stewart Meena:

Je! Unasikiliza miondoko yote!, au ipo mirindimo ambayo huipendelea zaidi kuisikiliza..? kama vile Bongo-flavour, HipHop, Mduara, Charanga, Blues, Pop, Zouk, Soukus, Country, Ragga/ Reagae/ Danshal , Ngoma za Asili, Folks nk….

Katika mazingira ya kiAfrika, muziki (haswaa wa kitamaduni) ulitumika kuwafundisha vijana mila na desturi zao, namna ya kuwa hodari katika familia zao, pamoja na kuwa wazoefu wa jambo flani lililokusudiwa kufundishwa kwa vijana hao.
 
 
Muziki huo ulipigwa kwa kutumia vyombo vya asili kama ngoma, makopo yaliyowekwa mchanga, huku kukiwa na mshehereshaji au muimbaji anayeongoza uimbaji kisha wengine huitikia kwa kumfuatisha muimbaji pamoja na mirindimo ya ngoma husika.
 
Wengine wakipanga miduara huku wakicheza, na miilini mwao wakijitanda mavazi ya mapambo ya sili, yote hiyo ni kwanini kufikisha ujumbe Fulani kwa jamii, kuwafurahisha na kuwatuliza nafsi zao zinazotokana na mawazo mengi, uchovu wa siku pamoja na kukuza mshikamano.
 
Kuna baadhi ya tamaduni, ngoma hizi zikipigwa basi tambua lazima mtu ataozeshwa mke, au kupata mume, yote hayo ni matokeo yaletwayo na kamshange hizo..... Je! kwanini ngoma hizo zilikuwepo, ziliibuka wapi! au ni kwanini watu tokea Enzi waliona ndio njia sahihi ya kujiburudisha na kutuliza nafsi zao!?
 
 
 
Ila katika mila hizo hizo yapo baadhi ya makabila na tamaduni zao, huwa na utaratibu wa kuimba nyimbo za kiasili ingawa hawakutumia vyombo vya muziki vyovyote lakini walitoa ala flani za muziki uliochanganyika na mirindimo ya mikolezeo kwa kutumia midomo yao.


Mfano mzuri ni kabila la Wamaasai ambao hawa huwa na taratibu za uimbaji kwa wanaume 9Morani) kuruka juu huku wakiimba na Wanawake (Mama yeyoo) wakiitikia kwa utaratibu uliopangilika kuendanda na taratibu zao, na hiyo imekuwa ikifanyika kipindi cha Jando na Unyago.

Hivyo kwa tamaduni zetu, muziki sio jambo genii la ilitegemea na ni wakati gani muziki huo au ngoma hizo zitachezwa. (Kiafrika tangu zamani ngoma zilikuwa zikipigwa jioni baada ya kazi, na mara nyingi wakati wa wikendi, mfano ngoma ya Baikoko tanga, chakacha-Kilimanjaro, nk)
 

 
Ingawa kwa Wazazi wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa watoto wao kuwa, kupenda kwao kutizama na kusikiliza muziki mbalimbali zaidi kunapelekea kushuka kwao kimasomo na kitaaluma pia.

Hiyo imekwenda mbali sana hadi wanafunzi hawaruhusiwi kwenda na simu yoyote mashuleni na wakibainika hupokwa simu zao na kupewa notes ya kuwaita wazazi wao, lakini kwa nchi za wenzetu wanafunzi huruhusiwa kwenda na simu zao, computer zao mashuleni, (ivyo kikubwa hapa sio simu wala muziki bali ni matumizi yapi sahihi ya simu hizo na Laptop zao)
 

 
KWELI MUZIKI UNAWEZA KUINUA UWEZO WA VIJANA KUBUNI MAMBO MBALIMBALI
 
Mashuleni: Vijana wengi wa kileo (walioko mashuleni vyuoni nk) muziki sio jambo geni kwani kwa sasa maendeleo ya sayansi na teknolojia umerahisisha Vijana hao ku-download na kuhifadhi miziki mingi tofauti kwenye simu zao (Smartphone) ambazo kwasasa zimeboreshwa na kuwekewa chip yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi nyimbo hizo.
 
Ambapo ukikutana na wanafuzi hao utawaona wakiwa na Wingi wa masomo, muda hafifu wa mapumziko nao pia unaelezwa kuleta matokeo tofauti ya ubunifu kwa vijana wengi wa kiTanzania, ikiwemo kufanya vyema katika masomo yao au shughuli zao za kila siku.
 
Kwa mfano: Utafiti uliofanyika nchini Australia umeonesha kuwa, kusikiliza muziki uliochangamka sio tu kunaweza kuboresha hisia ya moyo wa muhusika, bali pia kunaweza kuinua uwezo wake wa kubuni mambo mbalimbali.
 
 
Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha (Sydney) wametoa ripoti hii ikisema, “katika utafiti wetu mpya tumechagua miziki minne, ambayo inaweza kuleta hisia ya utulivu, furaha, huzuni na wasiwasi”.

Ambapo katika majaribio ya kung’amua hilo, Watafiti hao waliwagawanya washiriki 155 kwenye vikundi vitano, na kuwataka kumalizia kazi zinazohitaji ubunifu, kama vile kufikiria matumizi tofauti ya ubunifu, ikiwemo ya kupanga vitofali vilivyovurugwa.

Vikundi vinne vilipewa kazi hiyo ya ubunifu kwa kusikilizishwa muziki wa aina nne tofauti (miondoko) ambao unaoleta hisia tofauti pia, huku kundi la tano waliifanya kazi hiyo pasipo kusikiliza muziki wa aina yoyote (yaani mazingira tulivu).

Baada ya zoezi hilo, Matokeo yameonesha kuwa, kusikiliza muziki uliochangamka kunaweza kuinua wazo la ubunifu kwani wote waliofanya ubuni huo waliibuka na aina tofauti pamoja na ufanisi tofauti wa kuifanya kazi hiyo.
 

Watafiti wamesema, kuinua uwezo wa uvumbuzi ni jambo muhimu la kuhimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia, na ni muhimu sana kuelewa athari zinazotokana na muziki kwenye maswala ya ubunifu, na hivyo jukumu lako kama mlezi, mzazi au mwangalizi wa muhusika unatakiwa utumie njia sahihi ya kuinua na kukuza ubunifu kwa walengwa.

Kwani Mazingira tofauti pia yanaweza kuathiri ubunifu huo wa wahusika, (mfano nyumbani wanakotokea, majukumu yanayowangojea, pamoja na wana himizwa vipi) kadhalika miondoko ya muziki pia ni moja ya njia zinazoweza kubadilisha mazingira hayo.

Kwamfano wapo baadhi ya watu wanapotizama filamu zenye mchanganyiko wa huzuni hujikuta nao machozi yakiwatoka pasipo kujizuia, au kulia, au matukio ya ajali huwafanya watazamaji kuhisi ni mojawapo ya eneo husika la ajali nk.

Swali kubwa ni kuwa je! Wewe huwa unapenda kusikiliza miondoko ya aina gani..? mzazi unamzuia vipi mwanao kuacha kusikiliza miziki isiyo na tija kwa taaluma yake? Muda gani unamuhimiza kujisomea vitabu mbalimbali ya kukuza ufahamu, kupumzika, na kufanya shughuli nyingine za nyumbani za kila siku.

 

NINI KIFANYIKE?

Kubwa zaidi wewe kama mzazi, unapaswa kuchagua aina za muziki ambazo utawapa watoto wako waisikilize wakati umewapa majaribio yanayohitaji ubunifu.

Kupanga ratiba za kujisomea vitabu na notes mbalimbali, na ukiwasimamia kuhakikisha hilo linatekelezeka, pamoja na kuzuia watoto wako kutumia muda wao mwingi kutizama filamu au televisheni.

(Katika nchi zilizoendelea huwezi kukuta watu wakitumia muda wao wa mapumziko zaidi ya masaa mawili kutizama filamu kwa siku)

Kija kujitambua nini unataka, ufanye nini kufikia malengo yako ya kitaaluma, kupumzika kwa wakati na kuwa na ratiba nzuri za kubadilishana mawazo na watu waliokuzidi taaluma nk.

Je! Aina gani za filamu zinazowafaa?, tafuta filamu nzuri zenye mafundisho kwa watoto wako ukilinganisha na jinsia, umri au rika lao (sio filamu za wavulana unawapa wasichana!)

Hata hivyo, kulingana na utafiti huo wa Chuo cha Sydney, bado Watafiti hao wanasema, wataendelea kutafiti athari za mitindo tofauti kwenye ubongo na kutoa matokeo zaidi kwa siku za usoni.

NINI MAONI YAKO, WAFIKISHIE WENGINE ELIMU HII KUIJENGA NCHI YAKO KWA VIJANA CHIPUKIZI (New generations)

Waweza show love HAPA PIA HISTORIA, Link: https://www.facebook.com/stewart.meena

No comments:

Post a Comment