NA:
Stewart Meena:
Je! Unasikiliza miondoko yote!, au ipo mirindimo ambayo huipendelea zaidi kuisikiliza..? kama vile Bongo-flavour, HipHop, Mduara, Charanga, Blues, Pop, Zouk, Soukus, Country, Ragga/ Reagae/ Danshal , Ngoma za Asili, Folks nk….
Katika mazingira ya kiAfrika, muziki (haswaa wa kitamaduni)
ulitumika kuwafundisha vijana mila na desturi zao, namna ya kuwa hodari katika
familia zao, pamoja na kuwa wazoefu wa jambo flani lililokusudiwa kufundishwa
kwa vijana hao.
Muziki huo ulipigwa kwa kutumia vyombo vya asili kama ngoma,
makopo yaliyowekwa mchanga, huku kukiwa na mshehereshaji au muimbaji
anayeongoza uimbaji kisha wengine huitikia kwa kumfuatisha muimbaji pamoja na
mirindimo ya ngoma husika.
Wengine wakipanga miduara huku wakicheza, na miilini mwao wakijitanda mavazi ya mapambo ya sili, yote hiyo ni kwanini kufikisha ujumbe Fulani kwa jamii, kuwafurahisha na kuwatuliza nafsi zao zinazotokana na mawazo mengi, uchovu wa siku pamoja na kukuza mshikamano.
Kuna baadhi ya tamaduni, ngoma hizi zikipigwa basi tambua lazima mtu ataozeshwa mke, au kupata mume, yote hayo ni matokeo yaletwayo na kamshange hizo..... Je! kwanini ngoma hizo zilikuwepo, ziliibuka wapi! au ni kwanini watu tokea Enzi waliona ndio njia sahihi ya kujiburudisha na kutuliza nafsi zao!?
Ila katika mila hizo hizo yapo baadhi ya makabila na tamaduni
zao, huwa na utaratibu wa kuimba nyimbo za kiasili ingawa hawakutumia vyombo
vya muziki vyovyote lakini walitoa ala flani za muziki uliochanganyika na
mirindimo ya mikolezeo kwa kutumia midomo yao.
Mfano mzuri ni kabila la Wamaasai ambao hawa huwa na taratibu za
uimbaji kwa wanaume 9Morani) kuruka juu huku wakiimba na Wanawake (Mama yeyoo)
wakiitikia kwa utaratibu uliopangilika kuendanda na taratibu zao, na hiyo
imekuwa ikifanyika kipindi cha Jando na Unyago.
Hivyo kwa tamaduni zetu, muziki sio jambo genii la ilitegemea na
ni wakati gani muziki huo au ngoma hizo zitachezwa. (Kiafrika tangu zamani ngoma
zilikuwa zikipigwa jioni baada ya kazi, na mara nyingi wakati wa wikendi, mfano
ngoma ya Baikoko tanga, chakacha-Kilimanjaro, nk)
Ingawa kwa Wazazi wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa watoto wao
kuwa, kupenda kwao kutizama na kusikiliza muziki mbalimbali zaidi kunapelekea
kushuka kwao kimasomo na kitaaluma pia.
Hiyo imekwenda mbali sana hadi wanafunzi hawaruhusiwi kwenda na
simu yoyote mashuleni na wakibainika hupokwa simu zao na kupewa notes ya
kuwaita wazazi wao, lakini kwa nchi za wenzetu wanafunzi huruhusiwa kwenda na
simu zao, computer zao mashuleni, (ivyo kikubwa hapa sio simu wala muziki bali ni matumizi yapi
sahihi ya simu hizo na Laptop zao)
KWELI MUZIKI UNAWEZA KUINUA UWEZO WA VIJANA KUBUNI MAMBO
MBALIMBALI
Mashuleni: Vijana wengi wa kileo (walioko mashuleni vyuoni nk)
muziki sio jambo geni kwani kwa sasa maendeleo ya sayansi na teknolojia umerahisisha
Vijana hao ku-download na kuhifadhi miziki mingi tofauti kwenye simu zao
(Smartphone) ambazo kwasasa zimeboreshwa na kuwekewa chip yenye uwezo mkubwa wa
kuhifadhi nyimbo hizo.
Ambapo ukikutana na wanafuzi hao utawaona wakiwa na Wingi wa
masomo, muda hafifu wa mapumziko nao pia unaelezwa kuleta matokeo tofauti ya
ubunifu kwa vijana wengi wa kiTanzania, ikiwemo kufanya vyema katika masomo yao
au shughuli zao za kila siku.
Kwa mfano: Utafiti uliofanyika nchini Australia umeonesha kuwa,
kusikiliza muziki uliochangamka sio tu kunaweza kuboresha hisia ya moyo wa
muhusika, bali pia kunaweza kuinua uwezo wake wa kubuni mambo mbalimbali.
Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha (Sydney)
wametoa ripoti hii ikisema, “katika utafiti wetu mpya tumechagua miziki minne,
ambayo inaweza kuleta hisia ya utulivu, furaha, huzuni na wasiwasi”.
Ambapo katika majaribio ya kung’amua hilo, Watafiti hao waliwagawanya
washiriki 155 kwenye vikundi vitano, na kuwataka kumalizia kazi zinazohitaji
ubunifu, kama vile kufikiria matumizi tofauti ya ubunifu, ikiwemo ya kupanga
vitofali vilivyovurugwa.
Vikundi vinne vilipewa kazi hiyo ya ubunifu kwa kusikilizishwa
muziki wa aina nne tofauti (miondoko) ambao unaoleta hisia tofauti pia, huku kundi
la tano waliifanya kazi hiyo pasipo kusikiliza muziki wa aina yoyote (yaani
mazingira tulivu).
Baada ya zoezi hilo, Matokeo yameonesha kuwa, kusikiliza muziki
uliochangamka kunaweza kuinua wazo la ubunifu kwani wote waliofanya ubuni huo
waliibuka na aina tofauti pamoja na ufanisi tofauti wa kuifanya kazi hiyo.
Watafiti wamesema, kuinua uwezo wa uvumbuzi ni jambo muhimu la
kuhimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia, na ni muhimu sana kuelewa athari
zinazotokana na muziki kwenye maswala ya ubunifu, na hivyo jukumu lako kama
mlezi, mzazi au mwangalizi wa muhusika unatakiwa utumie njia sahihi ya kuinua
na kukuza ubunifu kwa walengwa.
Kwani Mazingira tofauti pia yanaweza kuathiri ubunifu huo wa
wahusika, (mfano nyumbani wanakotokea, majukumu yanayowangojea, pamoja na wana himizwa vipi) kadhalika miondoko ya muziki pia ni moja ya njia zinazoweza
kubadilisha mazingira hayo.
Kwamfano wapo baadhi ya watu wanapotizama filamu zenye mchanganyiko wa huzuni hujikuta nao machozi yakiwatoka pasipo kujizuia, au kulia, au matukio ya ajali huwafanya watazamaji kuhisi ni mojawapo ya eneo husika la ajali nk.
Swali kubwa ni kuwa je! Wewe huwa unapenda kusikiliza miondoko
ya aina gani..? mzazi unamzuia vipi mwanao kuacha kusikiliza miziki isiyo na
tija kwa taaluma yake? Muda gani unamuhimiza kujisomea vitabu mbalimbali ya
kukuza ufahamu, kupumzika, na kufanya shughuli nyingine za nyumbani za kila
siku.
NINI KIFANYIKE?
Kubwa zaidi wewe kama mzazi, unapaswa kuchagua aina za muziki
ambazo utawapa watoto wako waisikilize wakati umewapa majaribio yanayohitaji
ubunifu.
Kupanga ratiba za kujisomea vitabu na notes mbalimbali, na
ukiwasimamia kuhakikisha hilo linatekelezeka, pamoja na kuzuia watoto wako
kutumia muda wao mwingi kutizama filamu au televisheni.
(Katika nchi zilizoendelea huwezi kukuta watu wakitumia muda wao
wa mapumziko zaidi ya masaa mawili kutizama filamu kwa siku)
Kija kujitambua nini unataka, ufanye nini kufikia malengo yako
ya kitaaluma, kupumzika kwa wakati na kuwa na ratiba nzuri za kubadilishana
mawazo na watu waliokuzidi taaluma nk.
Je! Aina gani za filamu zinazowafaa?, tafuta filamu nzuri zenye
mafundisho kwa watoto wako ukilinganisha na jinsia, umri au rika lao (sio
filamu za wavulana unawapa wasichana!)
Hata hivyo, kulingana na utafiti huo wa Chuo cha Sydney, bado Watafiti
hao wanasema, wataendelea kutafiti athari za mitindo tofauti kwenye ubongo na
kutoa matokeo zaidi kwa siku za usoni.
NINI MAONI YAKO, WAFIKISHIE WENGINE ELIMU HII KUIJENGA NCHI YAKO
KWA VIJANA CHIPUKIZI (New generations)
Waweza show love HAPA PIA HISTORIA, Link: https://www.facebook.com/stewart.meena
No comments:
Post a Comment