IMAGE: By Internet |
Kampuni ya Toshiba ya Japan imesanifu betri
mpya ya magari yenye ukubwa wa mkono ambayo inahitaji kuchajiwa kwa dakika 6 tu
tofauti na zile nyingine za Oxide zinazohitaji masaa8-10.
Tofauti na betri nyingine za Li-ion ambazo
ncha hasi zilitengenezwa na grafati, betri mpya imetengenezwa na Niobium
Titanium Oxide, ambayo inaleta nishati nyingine na inaweza kuchajiwa kwa muda
mfupi sana.
Betri za kawaida za magari zikichajiwa kwa
nusu saa umeme utafikia asilimia 80, lakini betri mpya ikichaji kwa dakika 6,
umeme utafikia asilimia 90. Magari ya majaribio ya kampuni hiyo yalikwenda
kilomita 320 baada ya kuchajiwa kwa dakika 6 tu.
Aidha, betri mpya ikichajiwa na kutumiwa
kwa mara 5000, bado ina zaidi ya asilimia 90 ya ujazo wa betri mpya, na inaweza
kuchajiwa katika mazingira baridi yenye joto la nyuzi 10 chini ya sifuri
sentigredi.
Kampuni ya Toshiba itaendelea kuboresha
betri hiyo, na kujaribu kuuza bidhaa rasmi ifikapo mwaka 2019.
HABARI KAMILI ENDELEA HAPA CHINI KWENYE LINK:
HABARI KAMILI ENDELEA HAPA CHINI KWENYE LINK:
source:
https://www.greencarreports.com/news/1113332_toshiba-claims-6-minute-recharge-for-new-electric-car-battery-cell
No comments:
Post a Comment