Na stewart Meena
CHAZA NI KIUMBE
anayefanyiza gundi inayonata sana ambayo haiwezi kupenywa na maji, chaza huyu
huweza kufanya (recycle) ya uchafu, na hata kuwafundisha wanasayansi kuhusu
urekebishaji wa chembe za urithi, jina jengine la chaza huyu mdogo hujulikana
pia kama KOME.
Kome hupatikana
ulimwenguni pote na huishi Baharini Wengine huishi katika vijito na maziwa ya
maji yasiyo na chumvi, Ambapo zaidi hutumika sana na Wanadamu kama Sehemu ya
mapambo Majumbani mwao.
Ndani ya koa
zao mbili zilizounganishwa pamoja mna nyama nyororo. Nyama hiyo imefunikwa na
kiungo kilicho kama ngozi. Kiungo hicho huitwa Kiziba_ukono, Kama ilivyo katika
viumbe wote wa MOLUSKA, Kizibaukono huchanganya kemikali ya Kalisi na gesi ya
kaboni dayoksaidi ili kutengeneza Koa inayoweka ulinzi juu yao.
Muonekano wa ndani mdomoni mwa Konokono aitwaye Chaza. |
Kalisi na gesi
hiyo hupatikana katika chakula cha kome na katika maji. Ili kuiga ustadi wa
kome, itatubidi kumeza mawe, kisha tuyachanganye mwilini mwetu, na kuyatoa
yakiwa vifaa vya ujenzi vilivyo tayari kutumiwa kujenga kuta na madari! Lakini
kitu kinachowasisimua sana watafiti si koa lenyewe; bali ni mguu wa kome.
GUNDI YA KOME
INAYONATA SANA
Hebu jaribu
kumwondoa kome kutoka kwenye mwamba. Utagundua kwamba yeye hunata kabisa
mwambani. Ni lazima kome afanye hivyo ili akinze mawimbi yenye nguvu ya bahari
au mashambulizi ya ndege wa baharini mwenye njaa anayetumia mdomo wake
uliochongoka.
Yeye huwezaje
kujishikilia kwa nguvu hivyo?
Chaza waliopo chini ya maji ya Bahari wakiwa wamejifanyizia gundi yao ndani ya Miamba ya Matumbawe (coral reef) |
Chaza anapochagua maskani yake, yeye huchomoza mguu
wake wenye umbo la ulimi nje ya koa na kuufinya mahala pagumu, ambapo Tezi_Fulani_Maalumu
hufanyiza na kutoa umajimaji wenye protini kupitia kijia kilicho kwenye mguu
huo.
Umajimaji huo
hukauka upesi na kuwa uzi mwembamba unaonyumbulika wenye urefu wa sentimeta
mbili hivi, Kisha sehemu ndogo iliyo kwenye ncha ya uzi huo hutoa utomvu mdogo
wa gundi kwa nguvu.
Kome huinua
mguu wake, na hatua ya kwanza ya kujishikamanisha humalizika. Nyuzi hizo
zilizowekwa kwa ustadi huungana na kuwa kitita kinachoitwa BYSSUS. Kitita
hicho humfunga kome imara kwenye maskani yake mpya kama vile kamba za kukazia
hema zinavyolikaza hema liwe imara. Kazi hiyo huchukua dakika tatu au nne tu.
Chaza/kome hupatikana zaidi katika maji ya bahari yenye chumvichumvi, ambapo kuna jamii zaidi ya 100 ya konokono hawa ikitegemeana na Ukanda ama eneo walilopo. |
- Hebu_wazia kuna gundi inayonata sana, isiyokuwa na sumu na inayonyumbulika kwa urahisi hivi kwamba yaweza kupenya mianya na nyufa ndogondogo, na inaweza kunata mahala popote, hata ndani ya maji.Wajenzi wa meli wangefurahia kuwa na gundi kama hiyo wanaporekebisha meli kwani hawangepata hasara ya kuondoa meli majini.Mafundi wa magari wangependa rangi isiyopenywa na maji kabisa, inayozuia kutu.Madaktari-wapasuaji wangependa gundi inayonata kabisa kwa minajili ya kuunganisha mifupa iliyovunjika na kufunga majeraha.Madaktari wa meno wangeitumia kuziba mashimo kwenye meno na kurekebisha meno yaliyovunjika. Gundi hiyo ingetumiwa kufanya mambo mengi sana.Hata hivyo, wanasayansi hawafikirii kuwatumia kome ili kutengeneza gundi hiyo inayonata sana, Mfano Ili kutengeneza gramu moja tu ya gundi hiyo, kome 10,000 watahitajiwa, Kwahiyo iwapo njia hiyo ingetumiwa ili kutosheleza mahitaji ya ulimwengu ya gundi, kome wote wangemalizika, na tayari jamii nyingi zimo hatarini.Badala yake, watafiti wa Marekani wametenganisha na kutokeza chembe nyingine za urithi ili kupata protini tano za kome zinazofanyiza gundi. Hivi karibuni watazitokeza kwa wingi katika maabara ili ziweze kujaribiwa viwandani.Pia, wanasayansi wa Uingereza wanafanya utafiti kuhusu mojawapo ya protini hizo za gundi. Hata hivyo, bado kome amewashinda. Ni kome tu ajuaye mchanganyiko sahihi wa protini unaoweza kushikamanisha vitu mbalimbali. Frank Roberto, mwanabiolojia wa molekuli, aliuliza hivi kwa kustaajabishwa: “Je, mtaweza kweli kuiga jambo hilo?”
Mfagiaji
Kome hula kwa kuchuja maji. Katika jamii nyingi za kome, kila kome huingiza lita kadhaa za maji mwilini kila siku na chakula, oksijeni na vilevile vichafuzi kama bakteria zinazodhuru na kemikali zenye sumu huchujwa. Kome husafisha maji vizuri sana kwa kutumia uwezo huo.Eneo la ndani mwa Kome milia (zebra) ambako ndomo huchomoza nyama yake ya ndani ambayo ni laini, Pia, wao hutumiwa kujua kimbele iwapo maji yamechafuliwa. Kwa mfano, mamia ya kome wameingizwa baharini karibu na eneo la Ekofisk lenye visima vya mafuta, karibu na pwani ya Norway. Kila baada ya miezi kadhaa, wanasayansi huwaondoa kwenye maskani yao na kupima kiasi cha uchafu ulio ndani ya magamba yao ili watambue iwapo kemikali zinazoingia baharini zinawadhuru viumbe wanaoishi humo.Tangu mwaka wa 1986, kome na chaza wametumiwa katika Mradi wa Mussel Watch kwenye sehemu za pwani na za bara katika Amerika Kaskazini. Watafiti hujua iwapo kuna mabadiliko yoyote katika ubora wa maji kwa kuchunguza chaza hao kila mwaka kuona kama wamemeza kemikali. Chaza hao wana faida kubwa kama nini!
Mara nyingi, jamii moja ya kome inayopatikana kwenye maji yasiyo na chumvi huonwa kuwa kiumbe mharibifu. Kome huyo mwenye milia huitwa kome aina ya zebra.(pichani juu)Kome huyo mdogo sana hupatikana hasa mashariki mwa Ulaya. Yamkini aliingizwa Amerika Kaskazini kiaksidenti katikati ya miaka ya 1980 wakati meli moja iliyokuwa ikivuka bahari ya Atlantiki ilipomwaga maji yanayofanya meli iwe thabiti. Tofauti na kome wengine, idadi ya kome aina ya zebra imeongezeka sana katika yale Maziwa Makubwa na milango-bahari iliyo kando yake na kusababisha hasara ya mamilioni ya dola kwa kuziba mabomba ya maji na kufanyiza magamba kwenye mashua, magati, na madaraja. Pia, kome huyo amepunguza idadi ya jamii nyingine kadhaa za kome zinazopatikana hasa katika eneo hilo.
Hata hivyo, kome hao wana faida fulani. Kwa kuwa kome aina ya zebra ndio walaji bora wa kuchuja maji, wao husafisha maji meusi ya ziwa haraka kwa kumeza mimea ya mwani inayoelea. Kisha, mimea ya kijani ambayo humea majini inaweza kunawiri tena na kuwaandalia makao viumbe wengine wanaoishi ziwani. Kwa sasa, wanasayansi wanachunguza iwapo wanaweza kutumia uwezo wa kome hao wa kuchuja maji ili kuondoa bakteria zinazodhuru kutoka kwenye mabwawa ya maji ya umma na hata kuondoa taka kutoka kwenye viwanda vya kusafishia maji machafu.Aina nyingine ya Chaza akiwa ndani ya kina kifupi cha Maji ya Bahari. STADI NYINGINE.
Je, ulijua kwamba kome fulani wanaopatikana kwenye maji yasiyo na chumvi hutengeneza lulu za asili, nyingine za thamani kubwa sana? Iwapo umewahi kuvaa vito vilivyofunikwa kwa lulumizi au umetumia vifungo vya lulu, huenda pia vilitengenezwa kutoka kwa kome. Lulumizi zinazong’aa zenye rangi ya upinde wa mvua, hufanyizwa kutokana na tabaka la ndani la koa za kome, na hutumiwa mara nyingi katika biashara ya kutengeneza lulu. Punje ndogo sana ya lulumizi, iliyokatwa kutoka kwenye koa la kome, huingizwa ndani ya chaza. Chaza anapowashwa na punje hiyo, yeye huanza kuifunika kwa lulumizi. Hatimaye, yeye hutokeza lulu.
Bila shaka, sisi hula kome fulani wa baharini pia! Kwa karne nyingi, watu wamefurahia kula nyama laini ya kome yenye lishe, inapopikwa kwa njia mbalimbali. Katika nyumba za Wafaransa, huenda ukala moules marinière, yaani kome aliyepikwa kwa kuchemshwa katika mchuzi wenye mvinyo na aina fulani ya vitunguu. Wahispania hupendelea kuwapika kwa kutumia viungo vingi. Chakula hicho huitwa paella. Nao Wabelgiji huwaandaa wakiwa moto katika sufuria kubwa na kuwala kwa chipsi.
Biashara ya kuvua kome hufanywa na mashirika makubwa-makubwa ulimwenguni pote, ingawa katika nchi fulani za Ulaya kungali kuna makampuni madogo-madogo yanayofanya biashara hiyo.
Nyama ya chaza/kome inayyotomika na Wanadamu kama chakula.
Tahadhari: Ikiwa unapanga kula chakula hiki kitamu, hakikisha kwamba chaza utakaotumia wametoka mahala panapoaminika, na usiwakusanye kutoka ufukoni isipokuwa uwe na hakika kabisa kwamba maji hayajachafuliwa.
-
what a beautful nature that, God offer to us..?
ReplyDelete