Je wajua?
RSM Titanic |
Hebu tafakari mwandishi wa
hadithi za kwenye vitabu anaandika kuhusu tukio la kufikirika, anatoa kitabu na
watunwanafurahianhadithi yake. Miaka michache baadaye, tukio kama hilo
aliloliandika kutoka kichwani mwake linatukia vilevile!
LINKI: http://www.cracked.com/article_18421_6-insane-coincidences-you-wont-believe-actually-happened.html
HAKIKA ITS AMAZING…..!
Kwa taarifa yako tukio kama
hilo limewahi kutokea likihusisha meli kubwa ya
Titanic. Je wajua ilikuwaje.!?
(Twende sawia)
Mnamo mwaka 1898, Mwandishi
wa mahiri wa vitabu kipindi hicho aitwaye Morgan Robertson alitoa kitabu cha
Hadithi alichokipa jina la Furtility (The wreck of The Titan).
Ndani ya kitabu hicho
Morgan alikuwa anaelezea Meli ya Kufikirika aliyoipa jina la Titan ambayo
ilikuwa na uwezo wa kubeba watu wengi na Mizigo mizito kuliko meli nyingine
zote kuwahi kutokea.
Katika Hadithi hiyo Morgan
alielezea jinsi Meli hiyo ya TITAN ilivyogonga Mwamba katika Bahari ya Atlantic na kusababisha izame.
Ndani yake kulikuwa na afisa Mstaafu wa Jeshi, John Rowland aliyekuwa ametopea
kwenye ulevi wa kupindukia na kusababisha maisha yake yapoteze mwelekeo.
Katika ajali hiyo Rowland
anageuka na kuwa shujaa baada ya kufanikiwa kumuokoa mtoto wa Mwanamke
aliyewahi kuwa naye kwenye mahusiano ya kimapenzi, akamkimbia kwasababu ya
ulevi.
Baada ya kunusurika kwenye
ajali hiyo Rowland anaanza ukurasa mpya wa maisha yake, anajirekebisha na
kuachana na tabia zote mbaya zilizosababisha maisha yake yakakosa mwelekeo.
Miaka 14 baadaye, katika Maisha halisi (achana na hadithi) kunatokea tukio Halisi ambalo linafanana kwa
kiasi kikubwa na kile kilichoandikwa na Morgan.
Meli kubwa ya RSM TITANIC
iliyokuwa na uwezo wa kubeba abiria wengi na Mizigo kuliko Meli nyingine yoyote
inazama kwenye bahari ya Atlantic baada ya kugonga mwamba.
Kuzama kwa Meli ya RSM Titanic katika bahari ya Atlantic, tarehe 14/04/1912, tukio lililo la kweli lililotabiriwa na Morgan, mwandishi wa riwaya. |
Katika Hadithi Morgan
alieleza kwamba meli ya Titan ilizama Aprili na ndani yake hakukuwa na maboya
ya kutosha kuokoa abiria waliokuwemo ndani yake.
Katika tukio halisi, Meli
ya Titanic Ilizama usiku wa Aprili-14, 1912 ikiwa na Maboya-16 tu kati ya
abiria zaidi ya elfu-3 iliyobeba.
Na katika Hadithi Morgan alieleza kuwa meli
hiyo ilikuwa na urefu wa mita-244, Meli halisi ya Titanic ilikuwa na urefu
unaokaribiana sana na huo.
Hata kwa upande wa majina
pia yanafanana, Meli ya kwenye kitabu ilikuwa ikiitwa Titan, na Meli halisi
ilikuwa ikiitwa Titanic.
Katika ajali ya kwenye
hadithi, zaidi ya watu-2500 waliokuwa kwenye meli waipoteza maisha. Katika
tukio halisi, zaidi ya watu-2200 walipoteza maisha.
Baadhi ya watu walianza
kumshutumu Morgan kwamba ndiye aliyetengeneza ajali hiyo.
Hata hivyo, Ilipotimu mwaka
1997 Star wa Muvi kutoka Hollywood, #Leornado akatumia wazo hilo kuigiza filamu
aliyoipa jina hilo la TITANIC…..
KUHUSU FILAMU ENDELEA HAPA:
https://simple.wikipedia.org/wiki/Titanic_%281997_movie%29
MAKALA KAMA HIZI PIA TEMBELEA HAPA: www.facebook,com/stewart.meena
No comments:
Post a Comment