Monday, 29 February 2016

JIONEE HAPA ZIWA LENYE RANGI YA WARIDI



KWELI DUNIANI KUNA MAAJABU YAKE

. JE, Ulishawahi Kujiuliza KWELI #Ziwa linaweza kuwa la rangi ya waridi?
Ziwa Retba linanaloiitwa Ziwa la Waridi Ambalo linapatikana Nchini Senegali. Jina hilo lometokana na maji yake yanavyonekana

Senegal 

Ziwa Retba linaitwa Ziwa la Waridi, na kwa kuwa liko kilometa 30 tu kutoka mji mkuu wa  Dakar, Senegal, ambayo ipo Afrika ya Magharibi,
Wageni hulitembelea Ziwa Hilo ili kujionea kama kweli lina rangi ya waridi. Lahaula ni kweli wafikapo hukuta kweli Ziwa Retba lina maji yanayong’aa na kwa kweli yana rangi ya waridi yenye kupendeza.
Mwangaza wa jua huathiri vijiumbe vilivyo majini na hivyo kutokeza rangi hiyo ya pekee. Hata hivyo, kuna mambo mengine yenye kupendeza mbali na rangi ya ziwa hilo.
Ziwa hilo lisilo na kina kirefu lina sakafu ya chumvi. Maji hayo yana chumvi nyingi sana hivi kwamba mtu anaweza kuelea kwa urahisi.
Wageni fulani wanachukua fursa hii kuelea kwenye ziwa hilo.
Mbali na Utalii Ni wazi kwamba watu wengi nchini Senegal hutegemea Ziwa la Waridi ili kupata riziki yao ya kila siku na kuyaendesha maisha yao.
Ziwa retba, muonekano wake kwa picha ya (Aerial photo) nyuzi 90.
 
UFAHARI WAKE MWINGINE:

(1). Kwenye kingo za ziwa hilo, wafanyakazi wanapakia chumvi kwenye malori. Tunatua kidogo ili kuwatazama wenyeji wakitoa chumvi kwenye ziwa. Tunawaona wanaume wakiwa wamesimama kwenye ziwa wakivunja chumvi kwa sururu huku maji yakiwa yamewafika kifuani.
Wanachota chumvi hiyo kwa kutumia sepetu na kuiweka kwenye vikapu kisha wanaipakia mashuani. Mmoja wa wafanyakazi hao anatuambia kwamba inachukua saa tatu kukusanya tani moja ya chumvi. Mashua hizo zimepakiwa chumvi nyingi sana hivi kwamba inakuwa vigumu kuelea
(2). Zinapofika ufuoni, wanawake wanapakua chumvi hiyo na kuibeba vichwani wakitumia ndoo,

(3). Wote wanafanya kazi hiyo kwa upatano.

HAKIKA DUNIA INA MENGI SANA TEMBEA UONE HAYO MENGI………

SOMA PIA ZAIDI KUHUSU ZIWA HILO PIA HAPA CHINI:

https://en.wikipedia.org/wiki/Lake_Retba

No comments:

Post a Comment