Monday, 29 February 2016

BAADA YA KUCHEZEA KICHAPO WENGER AWATAKA ARSENAL KUJIPANGA ZAIDI


Kocha wa Washika bunduki wa London Arsene Wenger


Arsenal hawana budi kusahau kichapo cha Manchester United na kuganga ya Swansea.
Mkufunzi wa klabu hicho Arsene Wenger anasema kuwa kichapo hicho cha 3-2 uwanjani Old Trafford hakifai kuwadumaza washika bunduki hao kwani nia na azimio la ni kukata kiu cha kombe la ligi kuu ya Uingereza.

Arsenal wamesalia katika nafasi ya 3 lakini sasa wana alama 5 nyuma ya vinara wa msimu huu Leicester, Wakati Man Uwamejjikita katika nafasi ya 4 wakiwa na pointi 44 nyuma ya Man City kwa pointi3 wakiwa na kiporo cha Mchezo mmoja Mkonini.
Marcus Rashford mfungaji chipukizi wa Magoli2 katika Ushindi walioupata  Manchester United wa goli3-2 dhidi ya Arsenal,


FUATILIA MATOKEO HAPA: BBC swahili
Michezo mingine:

Tottenham waliichapa Swansea 2-1 na kusalia katika nafasi ya pili wakiwa na alama 54 tatu zaidi ya The Gunners.
''Kwa hakika hatuwezi kujihurumia eti kwa sababu tuliambulia kichapo Old Trafford ,lazima tujifurukute na kuthibitishia wapinzani wetu kuwa tupo kwenye kinyang'anyiro cha kombe la ligi msimu huu.'' alisema Wenger.

Arsenal wanaialika Swansea inayoorodheshwa katika nafasi ya 16 katika jedwali la ligi ya premia ya Uingereza uwanjani Emirati.

Huku zikiwa zimesalia mechi 9 pekee msimu huu ukamilike kila mechi na alama inaumuhimu mkubwa katika vilabu husika.
Wenger alisema " Kimsingi kichapo hicho kina maana zaidi ya moja kwetu,,,matokeo kamili yatabainika mwisho wa msimu.

Mara ya mwisho Arsenal walipotwaa kombe la ligi kuu ya Uingereza ilikuwa mwaka wa 2004 na hapo jana The Gunners walishindwa kumthibiti tineja Marcus Rashford alifuma kimiani mabao mawili kwa haraka.

Wenger hata hivyo alikataa katakata kukubali kuwa walishindwa na kikosi cha chipukizi cha United.

''tangu lini De Gea amekuwa mchezaji chipukizi, hawa wachezaji waliigharimu United mamilioni ya pauni, Watizame Memphis Depay, Morgan Schneiderlin na Juan Mata hicho ni kikosi dhabiti.''alinuna Wenger.

No comments:

Post a Comment