Thursday, 15 September 2016

Thursday, 1 September 2016

NAMNA YA KUTATUA MSONGO WA MAWAZO KWA MABINTI


Msongo wa mawazo mara nyingi huwapata mabinti wadogo kuanzia umri wa miaka 13-22, ambapo wakati huu kwa motto wa kike huwa ni kipindi cha Kuvunja Ungo (Balehe) na hivyo huanza kushuhudia mabadiliko kadha wa kadha katika miili yao.

KWA NINI HILI HUTUKIA
Mabadiliko ya kimwili. Kukua kwa haraka kunakotokea wakati wa kubalehe kunaweza kumfanya msichana awe na mkazo sana, hasa ikiwa amechelewa kukua au amewatangulia wasichana wenzake.
Marry * ambaye sasa ana umri wa miaka 20 anasema hivi: “Nilikuwa kati ya wasichana wa kwanza kuvaa sidiria, na niliona haya sana. Nilipojilinganisha na wasichana wengine, nilijiona kana kwamba nina kasoro fulani.”

Mabadiliko ya kihisia. Jackline, ambaye sasa ana umri wa miaka 17, anakumbuka hivi: “Nilichanganyikiwa, sikuelewa kwa nini nilikuwa na furaha mchana na usiku ulipofika nililia sana. Sikujua nilikuwa na tatizo gani. Nilishindwa kabisa kudhibiti hisia zangu.”

Kuanza kupata hedhi. Msichana anayeitwa Vivian anasema: “Nilipopata hedhi kwa mara ya kwanza nilishtuka sana ingawa mama yangu alikuwa ameniambia mengi kuhusu kipindi hicho. Nilioga mara nyingi kwa siku kwa sababu nilijihisi mchafu wakati wote. Na pia, kaka zangu watatu walinitania sana bila huruma. Walidhani kwamba kupata hedhi ni jambo la kuchekesha.”

Kushinikizwa na marafiki. Debora, ambaye sasa ana umri wa miaka 18, anakumbuka hivi: “Nilipokuwa na umri wa kati ya miaka 12 na 14, marafiki wangu walinishinikiza sana. Wanafunzi wenzangu walimchokoza yeyote aliyekuwa tofauti nao.”


MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA
Mtie moyo binti yako azungumzie mkazo anaokabili. Mwanzoni, anaweza kusita kuzungumzia jambo hilo. Lakini uwe mvumilivu na ujaribu kuzungumza naye kwa Upole zaidi naamini atakuelewa na kuweza kuikabili hali yake mujaraba.
.
Usipuuze mkazo anaopata binti yako. Kumbuka, hana uzoefu kama wewe kwa kuwa hajapitia mikazo maishani, hivyo hana ujuzi wa kumwezesha kushughulika nayo na pia isitoshe ni mabadiliko yanayotokea katika mwili wake ghafla tu.

 Usimpangie binti yako mambo mengi ya kufanya.  Vijana ambao wana mambo mengi sana ya kufanya “mara nyingi huonyesha dalili za mkazo, kama vile maumivu ya kichwa na tumbo. Na hii hutokea wakati Familia nyingi za kiAfrika na tamaduni zao humpangia zaidi mtoto wa kike majukumu mengi kuliko Mtoto wa Kiume.

Hakikisha binti yako anapumzika vya kutosha. Mara nyingi vijana hawalali vya kutosha. Binti yako asipolala vya kutosha, uwezo wake wa kufikiri utapungua na hivyo hataweza kukabiliana na mikazo wake unaomkabili.

Msaidie binti yako ajue jinsi ya kukabiliana na mkazo. Kwa wasichana wengi, mazoezi hupunguza mkazo.

Mfano: Wasichana wengi huona kwamba wanapoandika hisia zao kwenye kitabu, (Diary)  huweza kuwiasaidia kukabiliana na mkazo katika fikra zao. Hivyo nawe Mzazi pia unaweza kumjengea Binti yako utamaduni huu wa kujitunzia kumbukumbu zake mara kwa mara na hiyo inaweza kumfanya akaifahamu hali yake vyema na impasavyo.

4HISTORY UP-DATES GO HERE ALSO: www.facebook.com/stewart.meena

FUJO ZAIDI ZAZUKA MARA BAADA YA RAIS BONGO KUTANGAZWA MSHINDI WA UCHAGUZI NCHINI GABON

Fujo zimezuka katika mji mkuu wa Gabon, Libreville baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi.
Mgombea wa upinzani Jean Ping amesema watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuvamia makao makuu ya chama chake.
Serikali imesema inawaandama "wahalifu wenye silaha" ambao awali walikuwa wameteketeza majengo ya bunge

Wakati huohuo:

Wapinzani nchini Gabon wamechoma moto jengo la bunge la nchi hiyo baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi wa Rais Uliofanyika siku ya Jumamosi dhidi ya mpinzani wake mkuu Jean ping.

Kwa upande wake mgombea huyo aliyeshindwa amesema pia vikosi vya usalama vimeshambulia makao yake makuu kwenye mji mkuu Libreville.
Jean Ping aliliambia shirika la habari la ufaransa AFP kuwa vikosi vya ulinzi vimetumia helkopta kushambulia kwa mabomu jengo hilo kabla ya kulivamia.

Amearifu kuwa watu 19 wamejeruhiwa baadhi yao wakipata majeraha mabaya.
Awali, polisi katika mji mkuu wa Gabon, Libreville walitumia mabomu ya kutoa machozi kuweza kuwatawanya wafuasi wa Jean Ping, waliokuwa wamejawa na hasira na ambao wanaamini kuwa matokeo hayo ya uchaguzi yalikuwa ya udanganyifu.

Ni kura chache tu, zilizomuwezesha Bwana Bongo kumshinda mpinzani wake na hatimaye kutangazwa kuwa mshindi, huku eneo analotoka akionekana kupata kura nyingi zaidi.
Ujumbe uliokuwa ukiwakilisha upinzani katika Tume ya Uchaguzi ulitoka nje na kukataa kusaini karatasi, zinazompa ushindi Rais Bongo.

Mwangalizi wa Uchaguzi huo, kutoka Jumuia ya Ulaya, Sara Crozier ameelezea hali ilivyo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville, kuwa ni ya wasiwasi.
Familia ya Bongo imekuwa madarakani katika nchi hiyo ya Afrika ya kati kwa takriban miongo mitano.
SOURCE: BBC swahili

Thursday, 23 June 2016

FAHAMU KUHUSU HISTORIA MPIRA WA MIGUU (Soka)

LEO TUANGAZIE KUHUSU HISTORIA YA MPIRA WA MIGUU (Soka)

Makalla na Stewart Meena.
https://www.facebook.com/stewart.meena


  UTANGULIZI MAANA YA SOKA.
 

Mashirikisho tofauti Ya Kandanda Duniani (pichani)
Mpira wa miguu (pia soka au kandanda) ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji ishirini na wawili katika timu mbili husika, kila timu ikiwa na wachezaji kumi na mmoja.

Lengo hasa la mchezo huu ni wachezaji kuonyesha uwezo wao wa kuumiliki mpira kwa kutumia miguu na kuuingiza mpira katika wavu wa timu pinzani mara nyingi zaidi.
Matumizi ya mikono ni marufuku isipokuwa kwa mlinda mlango (golikipa) katika eneo maalumu na wakati wa kurudisha mpira baada ya ya kutoka nje ya uwanja.



HISTORIA YA MPIRA WA MIGUU


Mfano wa Mchoro unaoonyesha Mchezaji wa mpira wa miguu, Ugiriki Ya Kale.(karne ya 18-19)

Michezo mbalimbali ya kuchezea mpira inaweza kupatikana katika kila uwanja wa jiografia na historia, Wachina, Wajapani, Wakorea na Waitalia wote walikuwa wakicheza mpira zamani kabla ya enzi zetu.

Wagriki na Waromania walitumia michezo hiyo kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita. Hata hivyo, ni nchini Uingereza pekee ambapo umbo la soka la kisasa lilianza kuibuka.

Kuibuliwa kwake kulilianza wakati mashirikisho mawili (Shirikisho la Mpira wa miguu na Mpira wa Ragbi) yalitawanyika, ambapo Shirikisho la kwanza la soka lilibakia nchini  Uingereza.



Mnamo Oktoba-1963, Vilabu-11 vya London vilituma wawakilishi katika mkutano wa (Freemason) ili kujadili na kuweka kanuni zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa kati yao. Mkutano huo ulipelekea kuanzishwa kwa Shirikisho la Kandanda lililoitwa ‘Football Association’

Miongoni mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kukataa utumiaji wa mikono kushika mpira na kunyanganya kwa nguvu kama ilivyo kwa mchezo wa ragbi. Hapo ndio mwanzo wa Ragbi kugawanyika na mchezo wa soka.

Miaka minane baada ya kuanzishwa, Shirikisho la Kandanda (FA) lilikuwa na wanachama 50. Shindano la kwanza la kandanda lilianza mwaka huo. Kombe la FA- ambalo lilifuatiwa na lile la Ligi ya Ubingwa miaka 17 baadaye.

Wachezaji wawili wa Kilabu ya Darwin, John Dove na Fergus Suter walikuwa wa kwanza kulipwa kwa mchezo wao. Kitendo hiki kilikuwa mwanzo wa soka ya kulipwa iliyohalalishwa mnamo mwaka wa 1885.

Mwamko huu ulipelekea kuanzishwa kwa Mashirikisho ya kitaifa nje ya Uingereza (Great Britain). Baada ya Shirikisho la Kandanda la Uingereza, Mashirikisho yaliyofuatia ni ya Uskoti (1873), Wales (1875) na Eire (1880).

Kutokana na ushawishi mkuu wa Uingereza katika mataifa ya Dunia, Soka ilizambaa kote duniani. Mataifa mengine yalianzisha Mashirikisho ya Kandanda kufikia 1904 wakati Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilipoanzishwa.

Tokea hapo mwanzo, kandanda ya kimataifa imekuwa ikikua licha ya vikwazo mbalimbali. Kufikia 1912, FIFA ilikuwa na uanachama wa mashirikisho 21, idadi iliyoongezeka na kufikia 36 kwa mwaka 1925.

Mnamo mwaka1930, kwa mara ya kwanza katika historia ya soka yalifanyika mashindano ya Kombe La Dunia (FIFA) ambapo ilikuwa na wanachama wapatao-41. Na mshindi wa jumla kwa mwaka huo wa kwanza alikuwa ni (URUGUAY) baada ya fainali kufanyikia nchini humo, na nchi ya Uruguay iliifunga timu ya Argentina mabao 4-2. (pichani chini)

URUGUAY VS ARGENTINA -1930

SHIRIKISHO LA KANDANDA DUNIANI (FIFA).

Shirikisho la kandanda Duniani (FIFA) ndilo shirikisho kuu linalosimamia Kandanda duniani (kwa nchi wanachama). Wanachama wake ni mashirikisho ya kandanda ya nchi mbalimbali, ambapo hadi kufikia mwaka wa 2000, FIFA ilikuwa na wanachama wapatao 204 kutoka pembe zote za dunia.

Shirikisho hili huandaa mashindano yote makuu duniani yahusuyo soka la kimataifa. (michuano mikuu hufanyika kila baada ya miaka-4)

Uwanja wa Cape-Town Stadium uliotumika kwa Fainali za FIFA Barani Afrika kwa mara ya kwanza (Nchini Afrika Kusini-2010)


HISTORIA ya kombe la dunia iliandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 1928 wakati Rais wa FIFA wakati huo, Jules Rimet alipoamua kuandaa michuano mikubwa zaidi duniani iliyohusisha mataifa mbalimbali, na Ufunguzi wa michuano hiyo ukafanyika miaka miwili baadaye mnamo mwaka-1930 nchini Uruguay na timu-13 zilialikwa kushiriki michuano hiyo.



Kuanzia hapo, FIFA ilifanikiwa kubadilisha miundo na mifumo mbalimbali ya michuano tofauti, ambayo imepelekea kuanzishwa kwa soka la kisasa zaidi.


Timu 32 zinapatikana baada ya mchakato wa mechi  zakufuzu ambazo zinashirikisha timu kutoka mataifa 200 duniani kote.

Kabla ya kombe la dunia Mechi ya kwanza ya kimataifa ya soka duniani ilichezwa mwaka 1872 kati ya England dhidi ya Scotland ingawa katika kipindi hicho ilikuwa ni mara chache kwa mchezo wa soka kuchezwa nje ya Uingereza.


Hata hivyo, kuanzia mwaka 1900 mchezo wa soka ulipata umaarufu duniani kote na vyama vingi vya soka vikaanzishwa. Mechi ya kwanza rasmi ya kimataifa kuchezwa nje ya Uingereza ilikuwa kati ya Ufaransa na Ubelgiji ambayo ilichezwa Paris,Mei 1904.

Mchezo huo ulisababisha kuanzishwa kwa Shirikisho la soka duniani (FIFA) Mei 22, 1904.

Itaendelea.........