AP Image caption
|
hombo hicho kitakuwa na nyaya ndefu za urefu wa mita 700
(nusu maili) ambazo zitatumiwa kuokota taka hizo. Nyaya hizo zitaundwa kwa
madini ya aluminiamu na chuma cha pua.
Mtambo huo umeundwa kwa usaidizi kutoka kwa kampuni ya
uvuvi na serikali ya Japani kwa kuwahusisha watafiti na wanasayansi wake.Inakadiriwa kwamba kuna zaidi ya vipande milioni 100 vya taka kwenye mzingo wa dunia, ambapo vipande hivyo huchagizwa na mabaki ya satelite kumeguka zikiwa angani, au pengine vyombo vinavyopelekwa kufanya utafiti sayari nyingine kugongana na vimondo na kumeguka nk.
Vipande vingi kati ya hivi vinasonga kwa kasi sana kuizunguka dunia kwenye mzingo wake, baadhi vikifikia kasi ya kilomita 28,000 kwa saa (maili 17,500 kwa saa) na kuna wasiwasi kwamba vinaweza kusababisha ajali mbaya au kuharibu mitambo inayosaidia mawasiliano duniani.
Taka hizo zimerundikana katika kipindi cha miaka 50 tangu binadamu aweze kuruka kwenya anga za juu, setilaiti ya Sputnik iliporushwa anga za juu na Muungano wa Usovieti mwaka 1957.
Mgongano kati ya setilaiti na kufanyiwa majaribio kwa mitambo ya kujikinga dhidi ya mshambulio ya setilaiti vimezidisha tatizo la taka anga za juu
Caption:
|
Watafiti wanasema nyaya hizo zinazotumia nguvu za maalum za sumaku ambazo kwa Kiingereza huitwa electro-dynamic, kitazalisha nguzu za kutosha kubadili mwelekeo wa vipande hivyo na kuvielekeza kwenye anga ya dunia ambapo vitateketea.
Kampuni ya wataalamu wa kuunda nyavu za kutumiwa na wavuvi Nitto Seimo Co, ambayo imekuwepo kwa miaka 106, imeshirikiana na shirika la anga za juu la Japan kuunda mtambo huo.
Majaribio ya kutumia mtambo huo ni moja ya juhudi za kuhakikisha anga za juu ni salama kwa wana anga kwa kupunguza taka zilizokuwepo kwa muda mrefu na kufanya maeneo hayo kutokuwa salama zaidi kwa wasafiri wa anga za juu kwendea sayari nyingine.
Inatarajiwa kwamba itasaidia kulinda vituo vilivyo anga za juu pamoja na setilaiti za kutabiri hali ya hewa na zile zinazotumiwa kwa mawasiliano, vyote vya thamani ya mabilioni ya dola.
Wataalamu wanasema kuna
manufaa mengi yatakayotokana na kuondolewa kwa taka kwa kutumia mradi huo wa
Japan, lakini wanasema huenda ukafanikiwa kwa vipande vikubwa pekee vya taka.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment