Kwa wale Wakristo, baada ya mfungo wa kwaresma na kuadhimisha Pasaka, niwatakie wote Hongera na Fanaka. ni kwa mara nyingine tena tunakutana kuendelea kuelimishana na kupashana habari mbalimbali.
Leo tuwaangazie Wadudu hawa wasumbufu kunguni, Je! Wajua kunguni anazuilikaje twende pamoja:
Mwndishi: Stewart Meena
KUNGUNI NI NANI?
Kunguni ni
wadudu ambao huishi kwa kufyonza damu ya binadamu, kwa kingereza wakijulikana
kama (Bed bugs) na makazi yao ni kwenye
mazingira machafu, wakisaidiwa na kujificha kwenye kingo za vitanda (chaga) na
kwenye pindo za mashuka/blanketi n.k.
Licha ya
kuhusishwa na uchafu, na mazingira duni, kunguni ameibuka kuwa mdudu mwenye
uwezo mkubwa wa kustahimili hatari dhidi ya maisha yake, kwa kujifanyizia kinga
maradufu kadiri anavyozidi kupuliziwa dawa nyingi za kuulia wadudu (sumu)
ambapo kwa kinga hiyo uwezekano wa yeye kufa hupungua au kutoweka kabisa.
Utafiti mpya
umebaini kuwa wadudu hawa wanaweza kustahimili sio tu tanuri ya moto, maji ya
moto na baridi kali bali pia madawa ya kisasa ya kuulia wadudu wanaotambaa, na
hivyo Kunguni hawa wanaweza kustahimili kupuliziwa dawa hizo nyingi ya sumu kwa
kuimarisha uwezo wake wa kujikinga dhidi ya sumu moja baada ya nyengine.
Na hiyo ni
dhahiri, kwani ukitaka kuthibitisha umwonapo mkamate naumweke sehemu
atakayoshindwa kutoka kisha mghasi kwa kumgusagusa, utaskia harufu flani kali
iendayo kwa kubadilika badilika itokayo miilini mwao, na hiyo ndio kinga yao
iwezayo kuwakinga kufa kwa wepesi.
Wadudu hawa
huishi kwa kufyonza damu ya wenyeji wake wakiwa usingizini na wakishaifyonza au
kuanza kufyonza damu hiyo hunda vina7 vyenye uwezo mkubwa wa kibayolojia wa
kujikinga dhidi ya sumu hizo kali za wadudu.
Hii ni kusema
kuwa kadri vizazi vya kunguni vinavyopuliziwa madawa yenye sumu ndivyo wadudu
hao wanavyoimarisha uwezo wake wakuzuia maafa miongoni mwa watoto wao.
(Sumu pekee iliyokuwa inauwezo wa
kuwaangamiza wadudu hawa ilikuwa ni DDT – iliyokuwa ikitumika kuuliwa wadudu wa
kwenye kahawa, ambayo kwasasa haitumiki tena au imepigwa marufuku kutengenezwa
kwa kuwa huwa na madhara pia kwa binadamu kwa kuvuta tu harufu yake)
Aidha, watafiti
wanasema kuwa vipimo 1000 vya sumu kali aina ya (neo-nicotinoid) vinahitajika
kuua kunguni katika maeneo mengine mbalimbali duniani, ambapo Watafiti hao wanasema
kuwa kuna hatari kubwa ya mdudu huyo kuenea kote duniani kutokana na utandawazi
na soko huria ambao umefanya ulimwengu kuwa kitongoji kikubwa tu.
Tafiti: Kwa Mujibu wa Jarida
la utabibu la The Journal of Medical of Entomology.
CHIMBUKO:
KUFIKIA katikati ya karne ya 20,
ilionekana kwamba wanadamu wamefaulu kuwadhibiti kunguni, lakini uhalisia
ilikuwa ni kuwapunguza tu na sio kwateketeza kabisa.
Watu fulani zamani waliwafahamu kunguni
kupitia tu wimbo wa zamani wa Kiingereza ulioimbwa na watoto wa shule za nasari
(au chekechea) uliosema: “Usiwaache kunguni wakuume.”
Hata hivyo, katika miaka ya 1970, nchi
nyingi ziliamua kupiga marufuku matumizi ya dawa ya DDT— ambayo iliyokuwa dawa
kuu ya kuulia kunguni kwa kuwa ilikuwa pekee yenye sumu kali na iliyoharibu
mazingira kwa ujumla wake ikiwemo kuweza kuleta madhara kwa wanadamu pia.
Lakini kiuhalisia kunguni, ametokea
katika chimbuko la wadudu watambaao wenye pingili na huelezwa chanzo chao kikuu
ni uchafu uliogandamana na kutengeneza baikteria ambao nao hubadili tabia siku
kadiri ya siku, kama ilivyo kwa kinyesi cha kuku ukikifunika na kikianza
kuvunda kwa joto utapata wadudu wa mfano huu wa kunguni wenye pingili (weupe)
ZAIDI HAPA: Bed Bugs
Hata hivyo, kemikali nyingine zilipotumiwa ilionekana kwamba kunguni walikuwa sugu na hazikuweza kuwaua, ila zilisaidia kuwapunguzia tu kasi ya kutoka kwa wingi kwenda kushambulia wenyeji wao usiku.
Pia watu walianza kusafiri mara nyingi zaidi
na bila kujua walihama pamoja nao. Matokeo yakawaje? Ripoti moja ya mwaka wa
2012 kuhusu kuwadhibiti wadudu hao inasema: “Katika miaka 12 ambayo imepita
kunguni wameanza kuonekana tena nchini Marekani, Kanada, Mashariki ya Kati,
nchi kadhaa za Ulaya, Australia, Afrika mashariki zaidi kuripotiwa ilikuwa
maeneo (kaunti) za Kisumu, Nakuru Kenya na maeneo kadhaa Tanzania na uganda.”
LINK: https://hivisasa.com/post/habari-njema-kwa-wanaosumbuliwa-na-kunguni
Awali jijini Moscow, Urusi, katika
mwaka mmoja hivi karibuni, ripoti za kutokea kwa kunguni ziliongezeka mara kumi
kuliko ilivyokuwa hapo awali, na Wakati huohuo, upande ule mwingine wa
ulimwengu, huko Australia, kumekuwa na ongezeko la asilimia 5,000 la
kunguni tangu mwaka wa 1999!
Watu fulani hubeba kunguni bila kujua
wanapoenda dukani, kwenye kumbi za sinema, au hotelini. “Upende usipende utabeba kunguni,” anasema meneja fulani wa
hoteli nchini Marekani, “Maadamu hoteli inapata wateja lazima kunguni
wataendelea kuwapo.”
SWALI
KUBWA KWA WATU KWA HIVI SASA NI KUWA NI:
Kwa nini ni vigumu kiasi
hicho kuwamaliza kunguni?
Unaweza kujilindaje dhidi
yao?
Na je Kunguni wanapoivamia
nyumba yako, unaweza kuchukua hatua gani zinazofaa ili kuwaondoa na kuwazuia
wasirudi tena?
Aidha
wanasayansi wa Jarida la ENTOMOLOGY wanashauri kutafutwa mbinu tofauti na iliyo mpya
ya kaajili ya kukabiliana na kunguni hao pasipo kutumia sumu zenye madhara kwa
mazingira, badala yake kuzalishwe wadudu wengine wanaoweza kuwala kunguni ili kuwazuia
wadudu hawa kuendea kuenea kwa kwasi ya hivi sasa maeneo mbalimbali duniani.
HII MUHIMU ZAIDI
KUFAHAMU,
JE WAJUA: Kunguni hawa huweza kustahimili kukaa
muda mrefu pasipo kufyonza damu ambayo ni chakula chao kikuu, Yaani wadudu hawa
wakivamia nyumba yako na ukasema unahama kwa muda ili ukirudi wawe wametokomea,
ukweli ni kuwa “Unajidanganya” hata ukae miezi sita ukirudi utawakuta tena sasa
wakiwa kijiji... hahahah!
Kwanza kunguni Ni Wadudu
Wasiokufa kwa Urahisi
Hii ni kwa kuwa wadudu hao ni wadogo
kama mbegu ya tofaa na wana mwili bapa, kunguni wanaweza kujificha mahali
popote pale, ikiwemo katika godoro lako, fanicha zako, sehemu ya ukutani ya
kuunganishia vitu vya umeme, au hata kwenye simu yako.
Kwa kawaida kunguni hupenda kujificha
mita tatu hadi sita kutoka kwenye vitanda na maeneo ya kuketi.
Kwa nini? Ili wawe karibu na chakula chao,
yaani, wewe!
INGIA HAPA: *******
Mara nyingi, kunguni huwauma watu
wanapolala, Hata hivyo watu wengi hawahisi maumivu wakishadungwa (wanapoumwa)
kwa sababu mdudu huyo humdunga mtu kitu kinachogandisha kinachomwezesha
kuendelea kula kwa dakika kumi hivi bila kukatizwa.
Na ingawa wengi hudhani kunguni
wanaweza kula kila siku, lakini ni tofauti zaidi kwani tafiti mbalimbali
zanaonyesha kuwa, kunguni akishakunywa damu ya kutosha huweza kuitumia hiyohiyo
kwa takribani siku4-7, na hii inamaanisha kwamba wingi wa kunguni huchochea
kila siku kuhisi unang’atwa na wadudu hawa.
Na kipindi hicho cha wiki kinapopita
pasipo kupata damu, haiwadhuru sana kwani wanaweza kuendelea kuishi bila kula
kwa miezi mingi hata karibia na mwaka kwa kuendelea kula virutubisho vingine
vipatikanavyo kwa wadudu wengine au hata katika mavumbi na utando mwingine wa
uchafu vyumbani uwavutao wadudu wengine watambaao.
Hivyo njia kuu ya kupambana nao ni
kuweka mazingira safi ya nyumba na, kuhama kwa muda, na wasipopata damu basi
hufunga safari kuondoka eneo hilo.
PILI:
Tafiti kuhusu wadudu hawa zinaonyesha
kumbeba kunguni mmoja tu, na kumleta nyumbani mwako, huweza kuwazalisha wengine
zaidi ya mamia endapo watakutana na mazingira rafiki kwao ya uchafu, kwani
inasemekana jike mmoja wa kunguni huweza kutaga mayai zaidi ya 10 kwasiku sawa
na 80 kwa wiki na kuyaangua yote, hivyo na mtoto jike aliyeanguliwa humchukua
siku18-21 na yeye kutaga mayai mengine.
Hebu fikiria wameanguliwa 80 kwa wiki, na
baada ya wiki tatu kati ya hao 80, jike ni 40, nao 40 wakaangua 80 kila
mmoja..?! wanapatikana wangapi?
Tofauti na mbu na wadudu wengine,
inaonekana kwamba kunguni hawaenezi magonjwa ya kuambukiza, Hata hivyo,
wanapomuuma mtu wanatokeza mwasho na baadaye sehemu hiyo inavimba, na watu
wengi huweza kuathiriwa kihisia au kuweweseka mara kwa mara usiki, kukosa
kujiamini mbele ya wenzao nk.
VUTA
PICHA: “unaathirika
kisaikolojia kwanini..?” kwa kuwa kunguni wanatabia ya kunata kwenye pindo za
nguo, na pindi unapoivaa nao huwepo, hivyo pindi unapotembea nao na kwenda
mazingira tofauti, nao huambua na kuanza kuhama au kutoka sehemu waliyokuwepo
na kuzurura ili kutafuta sehemu nyingine iliyosalama zaidi kwao kujificha.
Watu walioumwa na kunguni wanaweza kupoteza usingizi,
kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni amewauma muda mrefu baada ya wadudu
hao kutoweka, Jarida moja nchini Sierra
Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi” na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”
Kunguni wanaweza kumsumbua mtu yeyote, Ni rahisi
kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba wapo, Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za
kwamba wapo nyumbani na unaposafiri, Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya
mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo
nyeusi au alama za damu.
Tumia tochi unapowatafuta kunguni ili uweze kuwaona, kwani
huogopa kumulikwa na mwanga na huanza kuzurura ovyo, ndio maana hutoka usiku
pekee kutafuta damu na pindi ukiwa chumbani mwako umezima taa zote.
Usiruhusu kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha
vyumbani mwako, Ziba nyufa zote ukutani na kwenye viunzi vya milango, Ingawa
kunguni hawaletwi moja kwa moja na uchafu, lakini ndio kivutio chao kikubwa,
hivyo itakuwa rahisi zaidi kwako kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha
nyumba yako mara kwa mara sehemu zile zisizofikika kirahisi kama uvunguni mwa
kitanda, kwenye kona nza makabati, chaga nk. Pia, epuka kuacha fenicha zako
zikirundikana sehemu moja kwa muda mrfu, badilisha mkao wa fenicha zako mara
kwa mara na kupunguza vitu vilivyorundamana / kurundikana visivyotumika maeeo
hayo.
Usirundike nguo chafu hasa zenye uhusiano na chumvichumvi
kama jasho na mkojo kwa muda mrefu chumbani pasipo kuzifua bora uziloweke
kuliko kuziweka kwenya pipa la taka (Dustbeen)
Ukiwa hotelini, unaweza kupunguza uwezekano wa kubeba
kunguni kwa kuepuka kuweka masanduku yako ya nguo sakafuni na kitandani.
MWISHO: KUNGUNI WANAPOVAMIA NYUMBA YAKO
Ukipata kunguni nyumbani au hotelini,
huenda ukawa na wasiwasi au hata ukaaibika. Mfano nchini Uingereza , Japhet na
mke wake waliumwa na kunguni walipokuwa likizoni. Japhet anasema: “Tuliaibika
sana. Tulijiuliza tutawaambia nini watu wa familia na marafiki tutakapofika
nyumbani? Je, wakati wowote wanapojikuna au kupatwa na mwasho wa ngozi
wangejiambia ni kwa sababu walitutembelea?”
Hata ingawa ni kawaida kuwa na maoni
kama hayo, usiache aibu ikuzuie kutafuta msaada, Wizara ya Afya ya Mwili na
Akili ya New York City iliwahi kutoa uhakikisho huu: “Ni
vigumu, lakini inawezekana kuwaangamiza kunguni, endapo Ukitafuta mbinu za
kupambana nao.”
Kanza Chunguza uone kama kuna kunguni,
pili chukua hatua za kuwazuia wasijifiche nyumbani kwako na kuondoka.
Hata hivyo, usifikiri kwamba ni rahisi
kuwamaliza kunguni, Kunguni wakivamia nyumba yako, unaweza kupata msaada kutoka
kwa mtaalamu wa kuwadhibiti wadudu hao wasumbufu.
Ingawa kemikali na sumu zilizotajwa
awali hazitumiwi tena, lakini wataalamu hao hutumia mbinu kadhaa zinazofaa ili
kuwaangamiza kunguni, ikiwemo watu wengine hutumia majivu, au majani ya
maharagwe kuwanasa nk.
Dini M. Miller, mtaalamu wa wadudu
anasema hivi pia: “Kuwadhibiti kunguni kunahitaji ushirikiano mkubwa sana kati
ya wakaaji wa nyumba, wamiliki wa nyumba yenyewe, na kampuni ya kuwadhibiti
wadudu wasumbufu kama hao.” Kwa kufuata mwelekezo wa mtaalamu na kuchukua
tahadhari zinazohitajika, unaweza kutimiza sehemu yako na ‘kutowaacha kunguni
wakuume’!
Wataalamu wa
wadudu wanasema kwamba kunguni hula damu ya wanadamu na wanyama wengine kutia
ndani wanyama-vipenzi.
MAKALA HAYA KWA
MSAADA PIA WA: https://wol.jw.org/sw/wol/
BBC, WIKIPEDIA,
NA JARIDA LA ENTOMOLOGY
No comments:
Post a Comment