Monday, 25 December 2017

X-MASS ASILI YAKE NININI? NA JE! LENGO LA KUPEANA ZAWADI LIMEANZIA WAPI!


 
Na: Stewart Meena

Ni sauti ya ngombe  aliaye horini ikiwa ni utambulisho wa kuzaliwa Yesu kristo ambapo Kila mwaka ifikapo tarehe kama ya leo Desemba 25, Wakristo duniani kote huadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa Masiha wao (Yesu Kristo) aliyewaunganisha wanadamu na ufalme wa mbingu tena baada ya wanadamu kumwasi sana Mungu, Bwana Yesu Kristo.

Kiuhalisia, Wapo wanaojua maana halisi ya neno X-Mass kama siku ya kuzaliwa kwake Yesu, Lakini pia wapo baadi yao ambao hawaifahamu vyema siku hii.

JAPO KWA UCHACHE, HAYA HAPA MAELEZO MACHACHE AU TAFSIRI HALISI YA NENO HILI (X-MASS)

Kwa Kuanza Hebu Tujuzane Kwanza, Neno Christimass Limetokana Na Nini.!?

Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo Au kwa Kiswahili christimas ni Noel ambapo  Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "noël".

Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", likimaanisha "(siku ya) kuzaliwa..Christimass au Noel ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

 

Katika sikukuu hii watu hupenda kupamba nyumba zao kwa miti ya xmass na maua yenye rangi mbalimbali pamoja na taa za kuwakawaka vivyo hivyo utaratibu huu ulikuwepo toka zamani ambazo ni  kumbukumbu ya Alama za nyota zilizowapeleka mamajusi hadi Bethlehemu alikozaliwa Yesu kristo.

Halikadhalika kuna miti ya Krismasi  ambayo ni Ni ishara ya Krismasi ambapo zamani mti wa xmass  ulipambwa zaidi kwa matunda mbalimbali, siku hizi miti hiyo hupambwa kwa kuzungushiwa taa za vimulimuli, pamoja na maua yadukani (Spesho)

Pamoja hayo kumekuwa na desturi ya  watu kupeana zawadi ya maua na kadi zenye maneo mazuri ya kutakiana heri ya xmass  na jambohili la kadi na  kupeana zawadi mbalimbali  ambazo  hufunguliwa siku ya pili baada ya xmass  ambayo huitwa boxing day (26/12) yaani siku ya kufungua zawadi  ililikuwepo toka zamani.
KWA MFANO: (Ieleweke Hapa silengi Wafuasi flani, ila ni kuzidi kuelimishana)

Katika historia hapo mwanzo tunaelezwa  jambo  hili lilianzia kwa kiongozi mmoja wa dini  wa zamani aitwaye - Martin Luther yeye  enzi za uhai wake alikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu.



Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo na Hapo alikuwa  anarejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kwa mujibu wa maandiko.
Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha  hata kuwa ni  nafasi muhimu ya biashara.

VIPI SEHEMU NYINGINE DUNIANI:

Lakini Katika nchi nyingi Duniani ikiwemo na Tanzania mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine, Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na Kadi,miti ya xmass na  mapambo ya Krismasi vimekuwa vikiuzwa sana katika maduka mengi.
Lakini yote kwa yote, Wakati huu wa sikukuu ya Christmas ni wakati ambao familia huungana pamoja kwa shughuli mbali mbali ikiwemo kula,kunywa na kupeana zawadi hasa kwa watoto,kwa hivyo tusitumie nafasi hii kwa kufanya mambo yatakayo ziumiza familia zetu kwa namna moja au nyingine. Nakutakia Heri ya Christmas na Mwaka Mpya.

No comments:

Post a Comment