Wednesday, 6 December 2017

SAYARI MPYA ILIYOGUNDULIWA YAPATIKANA IKIWA NA UMBO-MCHONGOKO MFANO KAMA WA SIGARA


PICHA NA: NASA
Darubini ya taasisi ya unajimu ya Chuo Kikuu cha Hawaii cha Marekani imegundua sayari ndogo ya kipekee mwezi uliopita, Sayari hii imepewa jina la Oumuamua, ambalo linamaanisha "mjumbe kutoka mbali" katika lugha ya Kihawaii.

Hii ni mara ya kwanza kwa binadamu kugundua sayari inayotoka nje ya mfumo wa jua, ukiacha zile sayari 9 zilizogundulika na zinazofahamika hadi wa hivi sasa, na kufanya idadi ya sayari sasa kuzidi kuongezeka.

Lakini kuhusu picha za awali za sayari hiyo mpya “Oumuamua” iliyogunduliwa, haikuwezekana kukusanywa data za kutosha kwani ilikuwa tayari imeondoka katika eneo lake la awali na hivyo bado juhudi zinaendelea kufanyika ili kutambua kama sayari hiyo nayo inatumia mfumo (orbit) unaotumiwa na sayari nyingine kulizunguka jua.

Lakini ajabu kubwa hapa, Baada ya kugundua sayari hii watafiti wameichunguza kupitia darubini mbalimbali zilizoko duniani kote, na Uchunguzi huo unaonesha kuwa sayari hiyo inazunguka mara mmoja kila baada ya saa 7.3, na kiasi cha mwanga unaotolewa na sayari hiyo pia kinabadilika kwa mara 10, Hali hii haijawahi kutokea kwenye sayari ndogo au vimondo vya mfumo wa jua.
 

 
Mnajimu wa taasisi hiyo Karen J. Meech amesema mabadiliko makubwa ya mwanga yanamaanisha kuwa sayari hii ni nyembamba sana, ambayo ina kipenyo cha mita 400, na urefu wake huenda ni mara 10 ya kipenyo chake.

Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA inasema tarehe20 Novemba sayari hii ilikuwa umbali wa kilomita milioni200 kutoka dunia, na inatarajiwa kupita katika mzingo wa Jupiter mwezi Mei mwakani, na itaondoka kwenye mzingo huo mwezi Januari mwaka 2019 na kuelekea kundi la nyota la Pegasus.

Ili kufahamu kuhusu Oumuamua pamoja na (Link) ambazo zitakupa uelewa Zaidi kwa muhusika anayezungumziwa ingia kwa kubofya kwenye neno husika lililopigiwa mstari.

SOURCE: http://swahili.cri.cn/

No comments:

Post a Comment