Sunday, 3 December 2017

IMETHIBITIKA KITAMBI NA UNENE HUONGEZA HATARI YA KUKUMBWA NA SARATANI YA UTUMBO MPANA NA MATITI


IMAGE BY: by3.bp.blogspot.com
Kama tunavyofahamu, unene unaweza kuongeza hatari ya saratani, hasa mafuta ya tumboni ndiyo yanayoleta hatari hiyo kubwa zaidi, “mafuta haya ni yale yasiyohitajika mwilini ambayo hujijenga kutokana na kula vyakula vyenye mafuta mengi, na wanga, pasipo kuufanyisha mwili mazoezi”
Utafiti huu mpya umeonesha kuwa mafuta tumboni yanaweza kuzalisha protini inayohimiza seli za kawaida kuwa seli za saratani, ambapo Unene umethibitishwa kuhusika na saratani za aina mbalimbali, ikiwemo saratani ya matiti na saratani ya utumbo mpana.

Mafuta kujazana mwilini ndio hupelekea mtu kuwa mnene wa (Nyama Zembe), badala ya kuwa na unene waUzito uliojengeka kwa mifupa iliyochagizwa na kufanya mazoezi kwa wingi. (kuwa mzito kwa nyama na kuwa mzito kwa mifupa kunatofautiana)

Unene uliopitiliza hasa kwa wanawake, huchangia kupatwa  na matatizo katika moyo, na kujiweka katika hatari zaidi ya kukumbwa na presha, na tatizo linapozidi kuwa sugu huweza kukabiliwa na saratani ya matiti kwa seli za mwili za kupambana na maradhi mbalimbali kuzongwa na mafuta, na hivyo kuzalisha protini ambayo kubadilika mfumo wake na kuwa wa saratani.

Tambua tabia ya mafuta mwili, hukimbilia kujengeka katika sehemu za mwili ambazo hazipati rapsha-rapsha, au kwa maana nyingine hazitumiwi kama mikunjo pindi muhusika anapotenda mijongeo mbalimbali, kama pindi anapotembea, anapokaa, anapojigeuzageuza, anaposhika vitu n.k

Baadhi ya sehemu hizo ni kama vile kwenye nyonga, chini ya tumbo, kwenye utumbo, sehemu za ndani ya maini na nje ya moyo, mgongoni chini ya shingo na sehemu zinazoshabihiana na hizo.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Michigan cha Marekani wamesema, katika upande wa tathmini ya saratani, kutathmini kiwango cha mafuta tumboni ni sahihi zaidi ikilinganishwa na kutathmini hali ya unene ya mwili wa muhusika.

Timu hiyo ya utafiti imetoa ripoti ikisema, “wamewalisha panya chakula chenye mafuta mengi nandipo wakaufanya utafiti huu”. Wakagundua kuwa mafuta tumboni yamezalisha idadi kubwa ya protini maalumu ambayo inazifanya seli za kawaida kuwa dhaifu na kubadilika kuwa seli za saratani.
 
Yakilinganishwa na mafuta ya chini ya ngozi, na mafuta ndani ya maini yanayoweza kuzalisha protini nyingi zaidi ya aina kama hiyo yenye kuleta athari kubwa kwa binadamu pindi atakapopatwa na saratani hiyo. 
IMAGE: by mipashohottz
Sasa wapo baadhi ya watu wakiona wametoka kitambi hufurahi na kujiona kuwa “Sasa afya imekubali” kumbe tayari mafuta yamezidi mwilini, na hasa maeneo ya tumboni na kwenye maini na moyo ambapo kadiri siku zinavyokwenda mtu huyu huanza kupata matatizo ya mapigo ya moyo kwenda mbio, presha ya damu kushuka kwani damu ushindwa kusafiri kwenye mishipa yake vizuri kutokana na kuwa imeanza kuzingirwa na mafuta hayo, pamoja na kusumbuliwa na Vichomi mara kwa mara.

Kwanini usubirie haya yakupate!, wakati unaweza kuepuka matatizo mbalimbali ya mwili kama kushuka kwa kinga mwili pamoja na kukumbwa na saratani za aina tofauti, punde tu unapoamua kupangilia milo yako vizuri (Balance diet) pamoja na kufanya mazoezi “hata kutrot tu inatosha” 
Kufanya mazoezi, sio tu kunaujenga mwili wako bali pia kunasaidia kupandisha kinga ya mwili, na kuwa imara katika kupambana na magonjwa mbalimbali, na kumwezesha muhusika kutoumwa umwa ovyo, zinasema tafiti.
Katika tafiti hizo zilizofanywa na Michigan zikiwahusisha panya, zimesema pia watafiti hao waliyaweka mafuta yaliyokusanywa katika mwili wa binadamu kwenye mwili wa panya hao pia, na Matokeo yameonesha kuwa mafuta yanazalisha protini nyingi zaidi ya aina hiyo, seli nyingi zaidi zinakuwa seli za saratani.

Hivyo basi, sehemu ya Utafiti huo umependekeza kuwa, watu wanatakiwa kutilia maanani mafuta yaliyomo ndani ya tumbo, ili kudhibiti kitambi kupitia udhibiti wa vyakula tunavyokula pamoja na kujituma katika kufanya mazoezi mazoezi kwa wingi.

Ukifanya mazoezi katika umri wako wote: hupunguza kuzeeka haraka, kuongeza miaka ya kuishi na kuwa na afya bora na sio bora afya.
Taarifa za kiDaktari, tafiti za jarida la Watchtower,  na uchunguzi uliofanywa na chuo cha Michigani zimetumiwa hapa.

SAMBAZA TAARIFA HII KUWAPATIA

WENGINE ELIMU ZAIDI.

No comments:

Post a Comment