HEBU
LEO TUANGAZIE KUHUSIANA NA MATANGO:
Watu wengi tunapenda kula baadhi ya matunda flani tu,
labda kutokana na ladha yake na kuyabagua mengine kutokana na kutokuwa na ladha
unayoihitaji, haswa wengi mkipenda ladha yenye utamu-utamu.
Lakini hasara zake kuna baadhi ya vitamin na faida
lukuki unazikosa kwa kutokula baadhi ya matunda mengine ambayo haya
hauyapendelei kuyala kutokana na uchachu wake, au kutoyazoea katika milo yako
ya kila siku.
Katika makala ya leo, Hebu tuangazie faida za kula
matango (Tango),
TANGO: Asili
ya kilimo cha matango inaaminika kuwa ilianzia kaskazini magharibi mwa India
ambako yamekuwa yakilimwa kwa zaidi ya miaka thelathini sasa, Hata hivyo kwa
sasa, matango, hustawishwa katika sehemu nyingi za kitropiki.
Matunda yake
hukatwa katwa na kuliwa kama achali, au kachumbari, au huwekwa kwenye siki na
pia hupikwa na kuliwa.
Katika nchi
yetu ya Tanzania matango hulimwa kwa wingi katika mikoa mbalimbali kama vile: Tanga, Morogoro, Mbeya, Lindi,
Mtwara na Pwani ambako kuna jua la kutosha, na Pia mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kilimo
cha matango hukubali vilevile.
Tango
(cucumber in English) ni zao muhimu katika mazao ya mboga na matunda nchini
Tanzania na hata nje ya Tanzania, kwani licha ya kuwa ni zao la biashara pia ni
zao la chakula.
Hili ni
tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini.
Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo, na kama ilivyo kwa
mboga kuwa muhimu kwa afya ya binadamu, Ndivyo Matango nayo yana faida nyingi
mbalimbali kw mlaji.
Kwa mkulima
hulifahamu vyema Tango. Ikiwa Tunda hili huwa na umbo refu hadi kufikia sm 15,
na Matunda yake hukatwakatwa na kuliwa kama achali au kachumbari, pia huweza
kuwekwa kwenye siki au kupikwa na kuliwa.
Ukuzaji wa
matango huwa njia ya kuongeza mapato kwa mkulima na kwa muda mfupi sana, pia
husadia kurutubisha ardhi kwa majani yake na mizizi yake kama ilivyo kwa
mkunde.
FAIDA YA
KULA MATANGO KWA BINADAMU:
1-KUONDOA
HARUFU MDOMONIMatango huondoa bakteria zinazofanya mdomo kunuka. Ili jambo hili litendeke unafaa kukata pande ya matango na kuweka mdomoni kwa dakika zisizopungua tano ukiwa umekaa kimya (Pasipo kuongea) ili iweze kutenda kazi au kuksaidia. Unafaa kuruda jambo hili mara tatu kila siku.
Mbali na kuswaki, Madaktari husema kuwa, Ulaji wa matango husaidia kuodoa joto jingi tumboni ambayo hua ndio sababu kuu ya mdomo kuwa na harufu hiyo mbaya.
2- KUPUNGUZA MAWAZO
Watu ambao hutumia mafikira sana katika kazi zao, hushauriwa kula matango kila siku kwani yana vitamini B, pamoja na B7, B5, B1 ambazo kwa pamoja hizo husaidia kupunguza mawazo mengi au (stress)
Na kwa Watumiaji wa pombe, au wanaofanya kazi nzito (za kutumia nguvu zaidi) huweza kuondoa hangover kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.
3- HUSAIDIA KATIKA UREMBO
Matango husaidia kulainisha ngozi ya mwili, kwa kina dada Unapokula matango nywele zako hupunguza kukatika, kuwa na afya bora na huweza kumea kwa haraka, Lakini pia matango hutumika kuondoa umbo la duara ambalo hupatikana machoni, kuondoa macho mekundu na kuwa meupe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.
(unafaa kufunga macho na kuekelea kipande cha tango
juu yake kisha kusubiri kwa masaa kadhaa kila siku au waweza kuyafunga machoni
usiku na kulala nayo hadi asubuhi kwa siku kadhaa – matokeo utayapata)
Unaweza
kuyaponda matango na kupaka usoni, kisha kuacha kwa dakika ishirini ili
kulainisha uso na baadaye kuosha uso, jaribu utajivunia sasa.
4- HUTUMIKA
KUONDOA SUMU MWILINI (Tango ni chanzo kizuri cha maji navitamin B
Tango huupa
mwili maji ya kutosha na vitamin B zote. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo
huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin
karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
Unaweza
kutengeneza kinywaji cha matango na matunda mengine kwa kuchanganya na mboga au
matunda mengine kama limau na machungwa ili kuondoa sumu ambayo hupatikana
mwilini, iliyojirundika baada ya muda mrefu.
5- HUSAIDIA KATIKA
UBONGO NA KUTIBU KANSA
Matango hua
na vitamini ambazo husaidia kukumbuka mambo kwa haraka, na kuchochea uwezo wa
kutunza kumbukumbu. Unashauriwa upendelee kuwapa watoto wako matango
kuchanganya na ndizi mbivu hiyo itawasaidia kuwa na akili na kufanya vizuri
darasani na katika shughuli mbalimbali za kibunifu.
Tango lina
virutubisho kama Lariciresinol,
Pinoresinol na Secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti
mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa
kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi
kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
FAIDA
NYINGINE ZA JUMLA: