Tuesday, 15 May 2018

FAHAMU, ULAJI WA VYAKULA VYENYE MAFUTA MENGI HUWEZA KUATHIRI UMETABOLI


 
Ulaji wa vyakula vingi vyenye mafuta mengi kwa wakati mmoja, imeelezwakitaalamu kuwa ni moja ya sababu inayoweza kuathiri umetaboli katika mwili wa mwanadamu.
 
Utafiti huo umegunduliwa na Watafiti wa Ujerumani ambao walichunguza kwa kina watumiaji au walaji wa chakula chenye mafuta mengi kwa wakati mmoja ikiwemo hamburger, chips na pizza unaweza kuathiri umetaboli wa mwili, na kusababisha ugonjwa wa maini yenye mafuta na ugonjwa wa kisukari.
 
Kituo cha utafiti cha ugonjwa wa kisukari cha Ujerumani kimesema, wamewashirikisha wanaume wembamba wenye afya nzuri kwenye utafiti, na kuwapatia kikombe chenye mafuta ya zaituni au kikombe cha maji bila mpangilio. Mafuta ndani ya kinywaji kile ni sawa na hamburger mbili za nguruwe pamoja na chipsi au pizza mbili.
 
Watafiti hao walitumia njia ya MRI na kugundua kuwa, ulaji wa mafuta mengi kwa wakati mmoja unaweza kupunguza mchango wa insulin, na kusababisha ongezeko la kuzuia insulin na kiwango cha mafuta kwenye maini, huku ukileta athari kwrnyr umetaboli wa maini ambayo inafanana na athari zinazotokana na ugonjwa wa kisukari wa aina II au maradhi ya ini.
 
Watafiti wamesema, kinachoshangaza ni kwamba kula mafuta ya zaituni kunaweza kuathiri haraka na moja kwa moja maini ya watu wenye afya nzuri, ambayo mafuta hayo yamesababisha kuzuia insulin.
 
Lakini watafiti wamesema, watu wenye afya nzuri wanaweza kurekebisha athari zinazotokana na chakula chenye mafuta mengi, lakini ulaji wa chakula cha aina hiyo wa muda mrefu utaleta madhara kwa afya.
 
HIVYO CHUKUA TAHADHARI...      (Source-CRI radio)

No comments:

Post a Comment