Thursday, 26 May 2016

HAKIKA HII NI ZAIDI YA MUUJIZA KATIKA SOKA, TIMU ECUADOR YALIMWA GOLI 44-1!


Timu ya Polileo ambayo ndio ilifanya mauwaji hayo. (goli 44-1)


Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.

Klabu hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200, ambapo Mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina pekee alifunga mabao 18.
 
Rais wa Indi Native Diego Culequi amesema matokeo hayo hayakutarajiwa na wachezaji hawakuwa wamezoea joto kali ambalo anasema lilichangia kushindwa kwao.

Mwandishi wa habari Mwingereza Tim Vickery, ambaye amekuwa Brazil kwa miaka 20, amesema Bon Accord kwa sasa wamejadiliwa sana katika vyombo vya habari Ecuador.

Anasema ligi ya daraja la tatu ya Ecuador huwa na ushindani mkubwa.
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Arbroath FC ya Scotland iliyofunga mabao 36-0 dhidi ya Bon Accord miaka 131 iliyopita.

Mwenyekiti wa Arbroath FC John Christison amesema ana wasiwasi kiasi kwamba rekodi yao waliyoiweka 1885 huenda ikavunjwa.
Amesema klabu hiyo itasubiri uamuzi wa Guinness World Records.

Tuesday, 24 May 2016

BAADA YA UBINGWA FA VAN GAAL SASA IMEKWISHA



 
Meneja wa Man U aliyemaliza muda wake, Lois Van Gaal akisalimiana na meneja mpya Jose Mourinho.
Meneja wa timu ya Manchester United ya Nchini Uingereza Louis van Gaal amenukuliwa akisema sasa imekwisha wakati akitarajiwa kumaliza kandarasi yake ya miaka miwili ya kuifundisha klabu hiyo.

Kuondoka kwa LVG kunafungua fursa ya kocha mpya wa timu hiyo Jose Mourinho ambaye sasa tayari ameshafunga mkataba wa kuinoa klabu hiyo ya Man united ambayo haijafanya vizuri tokea kustaafu kwa kocha wake wa muda mrefu (Ferguson) ambaye alikabidhi kandarasi kwa David Moyes kabla ya kutimulliwa na timu kukabidhiwa kwa Van gaal.

Mourinho amekubali kutia saini ya miaka mitatu ya kuinoa Man United na anatarajiwa kutangazwa mbele ya waandishi wa habari mapema wiki hii, ingawa kumekuwa na minongono kutoka kwa wachezaji wa zamani kuwa meneja huyo mpya hawezi kuipatia timu hiyo mafanikio yaliyokosekana kwa muda mrefu.

Van Gaal aliyechaguliwa kuinoa Man united tokea msimu wa 2014 ameiwezesha timu hiyo kutwaa taji moja pekee la FA CUP kwa kuichapa Crystal Palace mabao 2-1 fainali wikendi ya jana jumamosi, na amefanikiwa kumaliza nafasi ya tano msimu huu na hivyo timu hiyo ya Manchester itakosa kushiriki UEFA lakini  itashiriki michuano ya Uropa msimu huu unaofuata.

Mourinho, kocha mpya wa Manchester United alifukuzwa kutoka klabu ya Chelsea mwezi desemba mwaka jana baada ya mwenendo mbovu wa uchezaji wa timu hiyo.

KUELEKEA FIFA-2016 , TIMU YA TAIFA UJERUMANI YAAHIDIWA DONGE NONO


kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani maarufu kama (Die Mannschaft) watapokea bahashishi ya euro laki-3 kila mchezaji ikiwa watashinda Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016).
 
Shirikisho la kandanda la nchini Ujerumani (DFB) limesema licha ya kinyang'anyiro cha mwaka huu kuwa na timu nyingi, na kuongezwa kwa hatua za mechi za mchujo, viwango vya bahashishi vitakuwa sawa na vya michuano ya Euro-2012 ambapo Ujerumani iliondolewa katika hatua nne za mwisho.

Meneja wa timu hiyo Oliver Bierhoff amesema wamekubaliana na DFB pamoja na wachezaji kuwa “kabla ya kuanza kwa Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ukraine mwezi juni-12 Fedha hizo watakuwanazo mkononi, na endapo watinga hatua ya robo fainali watalipwa euro elfu-50 kila mchezaji, euro laki-1 kwa nusu fainali na Euro laki 1 na kwa kutinga hatua ya fainali.

Ikiwa watashindwa katika hatua ya 16 bora za mwisho, au washindwe kufuzu katika Kundi lao wataambulia patupu, lakini Washindi hao wa Kombe la Dunia mwaka-2014 nchini Brazil, ni miongoni mwa timu 24 zinazopigiwa upatu wa kufanya vyema katika mashindano hayo.

Michuano hii inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 10 mwezi Juni mwaka huu, ambapo Ujerumani ipo katika Kundi C pamoja na timu za Ukraine, Poland na Ireland ya Kaskazini.

Wakati huo huo: Kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Guendogan mwenye umri wa miaka 25 atakosa dimba la Kombe la Mataifa ya Ulaya Euro 2016 baada ya kuumia goti wakati akifanya mazoezi na anatarajiwa  kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu.

Habari hii ni pigo kwa kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Loew na pia bahati mbaya mchezaji huyo aliyekosa tena Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kutokana na maumivu ya mgongo yaliyomweka nje kwa miezi 14 kuanzia Agosti 2013.

FIFA SASA KIMENUKA, WAANZA TIMUATIMUA


Jerome Valke, naibu katibu wa Shirikisho la Soka duniani FIFA

 Shirikisho la soka duniani Fifa limemtimua naibu katibu wake Markus Kattner kwa kujihusisha na ukiukwaji wa matumizi ya siri ya mamilioni ya dola.
Kattnet raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 45 alikua akiitumikia nafasi hiyo baada ya aliyekua katibu Jerome Valcke kutimuliwa kazi kutokana na kashfa za rushwa.
Kufutwa kazi kwa kiongozi huyu kulikuja mara moja baada ya bodi ya uchuguzi ya ndani ya Fifa kugundua kulikua na ukiukwaji na uvunjaji wa majukumu yake.
Kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha mapungufu katika majukumu yake kwa kutumia pesa za ziada ambazo waliamua kiasi gani rais, katibu mkuu na naibu katibu mkuu walipwe.

Monday, 23 May 2016

SOKA MATAIFA YA EURO-2016 NCHINI UFARANSA ZIMEBAKI WIKI MBILI TU.



Moja ya Kiwanja cha mpira wa Miguu nchini ufaransa (kati ya Viwanja 10) kitakachotumika kwa michuano ya mataifa ya ulaya (Euro-2016)

 Ikiwa zimebaki wiki mbili pekee kuanza kwa michuano ya UEFA-Euro 2016, hali ya usalama nchini Ufaransa Inakofanyika Michuano hiyo bado imeelezwa kuwa tete, ambapo Wanausalama nchini Ujerumani wameonya kuwa Mtanange huo huenda ukakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi.


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault anasema "Kila kitu kimefanywa kuimarisha usalama wa raia wa Ufaransa pamoja na wageni wote wataokuja kushiriki katika Euro 2016”


Mapema wiki hii Bunge la nchini Ufaransa limeidhinisha mswada wa kurefushwa kwa miezi miwili zaidi, kutangazwa kwa hali ya hatari ambayo iliyowekwa tangu mashambulizi ya kigaidi ya Novemba mwaka jana.


UEFA inapanga kuwaajiri maafisa usalama wa kibinafsi takribani elfu-10, wakati wa kinyang'anyiro hicho na kila uwanja kati ya viwanja-10 vitakavyotumika kutakuwa na maafisa 900 wa usalama watakaoweka ulinzi kwa kila mchuano.

Sunday, 22 May 2016

WATFORD SASA KUJIPANGA KIVINGINE, USAJILI.

Gerald Mazzari akitokea Inter Milan sasa atua rasmi Watford
 
Klabu ya Watford ya Nchini Uingereza imetangaza kumchukua mkufunzi wa zamani wa Inter Milan Walter Mazzarri, na sasa ndiye atakayekuwa meneja wao mpya kuanzia Julai mwaka huu.

Hii ni baada ya kuondoka kwa meneja Quique Sanchez Flores.
Mwitaliano huyo wa umri wa miaka 54, ambaye aliwahi kuwa mkufunzi Sampdoria na Napoli, ametia saini mkataba wa miaka mitatu Vicarage Road.

Mhispania Flores aliondoka baada ya kukaa chini ya mwaka mmoja Watford, ambapo aliwaongoza kumaliza nambari 13 na kufika nusufainali Kombe la FA ambapo aliondolewa na Crystal Palace.

Mazzarri ndiye meneja wa nane kupewa kazi Watford katika kipindi cha miaka minne.
Mazzarri alishinda Coppa Italia akiwa na Napoli in 2012 ana akawasaidia kumaliza nambari mbili Serie A msimu uliofuata.

Alijiunga na Inter kwa mkataba wa miaka miwili Mei 2013 na akawaongoza kumaliza nambari tano ligini msimu wake wa kwanza.
Lakini amekuwa bila kazi tangu kutimuliwa
San Siro Novemba 2014, klabu hiyo ilipokuwa nambari tisa kwenye jedwali, alama 12 nyuma ya viongozi wa ligi Juve.

Saturday, 21 May 2016

NJIA NYEUPE KWA VAN GAAL, FA UBINGWA?

Rashfod shujaa, Man U ubibwa FA

Manchester United wameshinda Kombe la FA baada ya kuwalaza Crystal Palace 2-1 katika fainali iliyochezewa uwanja wa Wembley.
Ni mara yao ya kwanza kushinda kikombe hicho tangu 2004.
Mabao ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata na Jesse Lingard.
Bao la kufutia machozi la Crystal Palace limefungwa na Jason Puncheon.
Ushindi huo ni nafuu sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutokana na kutofana kwa klabu hiyo.
Kwa ushindi huo, Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Van Gaal alisema amefurahia sana kushinda kikombe hicho.
"Ni muhimu sana kushindia klabu kikombe hiki, kwaa mashabiki, na mimi pia kwa sababu sasa nimeshinda katika mataifa manne, na si mameneja wengi wamefanikiwa kufanya hivyo," amesema.
"Tukiwa na wachezaji 10, na tulikuwa tumecheza Jumanne jioni pia, lakini tulistahiki. Lilikuwa bao zuri sana, sio?"

JE! WAIJUA THAMANI YA VIWANJA 10 BEI MBAYA AFRIKA.. ONA HAPA

MIONGONI MWA VIWANJA VYA SOKA VYENYE THAMANI KUBWA ZAIDI BARANI AFRIKA.....


10- Chini Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam huu ulijengwa kwa dola milioni 53 na nusu ya hela za ujenzi huo zilitolewa msaada na serikali ya China. ulifunguliwa mwaka 2007 na unauwezo wa kuchukua mashabiki 60000.
9- Chini: Stade Olympique de Radès huu ni uwanja uliopo Tunisia mji wa Rades, uwezo wake wa kuchukua mashabiki ni sawa na uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, ila gharama yake inatajwa kufikia dola milioni 110, ulijengwa mwaka 2001.
8-Mbombela Stadium ni moja kati ya viwanja vilivyotumika katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika ya Kusini, kina thamani ya dola milioni 140, kina uwezo wa kuchukua mashabiki 40,929.  

7- Estádio 11 de Novembro upo Angola lakini ulitumika kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2010, umejengwa kwa dola milioni 227 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000.
5-Nelson Mandela Bay Stadium huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 270 upo katika mji wa Port Elizabeth na unauwezo wa kubeba mashabiki 48,459. Jina lake limetoka na Rais wa kwanza wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela.
3-FNB Stadium ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 440, ulichezewa fainali za Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini. FNB Stadium jina lake lilizoeleka na wengi ni Soccer City. Huu ndio uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi zaidi barani Afrika, unauwezo wa kubeba watu 94,736.
2- Moses Mabhida Stadium ulijengwa kwa dola milioni 450 , uwanja huu upo Durban Afrika Kusini na ulitumika kwa baadhi ya mechi za fainali ya Kombe la Dunia 2010, ulikuwa na uwezo wa kuingia mashabiki 62,760 lakini wakati wa fainali za Kombe la Dunia ulipunguzwa na kuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 54000.
1-Cape Town Stadium huu ndio uwanja wenye thamani kuliko vyote barani Afrika, kwani zimetumika dola milioni 600, unauwezo wa kuingia mashabiki 64,100.

4-Abuja Stadium hiki ni moja kati ya viwanja vilivyojengwa kwa gharama zaidi barani Afrika, dola milioni 360 ndio zilitumika kujenga uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,491 upo  mji mkuu wa Nigeria Abuja. 
6- Peter Mokaba Stadium huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, ulijengwa kwa dola milioni 150 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 41,733, kwa sasa unatumiwa na klabu ya Black Leopards FC kama uwanja wa nyumbani.