Tuesday, 26 April 2016

BAYERN, ATLETICO HISTORIA KUJIRUDIA?



Nusu Fainali



Mechi za Kwanza



**Saa 3 Dakika 45 Usiku




Jumanne Aprili 26



Manchester City v Real Madrid



Jumatano Aprili 27



Atletico Madrid v Bayern Munich


 
Kumekucha UEFA

MANCHESTER CITY kushuka dimbani hii leo kuvaana na REAL MADRID katika mchezo wa Nusu Fainali kuwania kukata tikiti ya kucheza fainali kombe la UEFA
Huku mchezo mmoja ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wapenda soka ni hapo siku ya kesho jumatano kati ya Atletico na Bayern.

Atlético de Madrid na FC Bayern München zitakutana Estadio Vicente Calderon Jijini Madrid siku ya Jumatano Usiku kwa ajili ya Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Timu hizi zimekuwa zikifika mara kwa mara kwenye Nusu Fainali za Mashindano haya lakini mara ya mwisho kwao kukutana ni zaidi ya Miaka 40 iliyopita.
Atletico, chini ya Kocha Diego Simeone, wanatinga Nusu Fainali kwa mara ya pili ndani ya Miaka Mitatu wakati Bayern, ambao sasa wapo chini ya Kocha Pep Guardiola, hii itakuwa ni Nusu Fainali yao ya 5 mfululizo.

DONDOO:
-Atletico, chini ya Kocha Diego Simeone, wameshinda Mechi 12 kati ya 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI walizocheza kwao Estadio Vicente Calderon lakini wameshinda Mechi 1 tu kati ya 6 wakicheza Hatua ya Mtoano ya Mashindano haya walipotoka Sare 3 na Kufungwa 2.
-Bayern hawajashinda katika Mechi 7 zao za mwisho za Ugenini za UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kutoka Sare 4 na Kufungwa 3.

Historia.
Mara ya mwisho kwa Atletico Madrid na Bayern Munich kukutana katika Mashindano rasmi ya Ulaya ni Mwaka 1974 walipopambana kwenye Fainali ya Ulaya na Bayern kushinda 4-0 kwenye Mechi ya Marudiano kufuatia Sare ya 1-1 iliyokwenda hadi Dakika za Nyongeza bila Mshindi na kulazimisha Mechi hiyo ya Marudiano.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Atletico Madrid (Mfumo 4-4-2): Oblak; Juanfran, Godin, Gomez, Luis; Niguez, Gabi, Fernandez, Koke; Griezmann, Carrasco
Bayern Munich (Mfumo 4-1-4-1): Neuer; Lahm, Martinez, Kimmich, Alaba; Alonso; Costa, Vidal, Thiago, Ribery; Müller
REFA: Mark Clattenburg (England)

UEFA CHAMPIONZ LIGI

Nusu Fainali
Mechi za Pili
**Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumanne Mei 3
Bayern Munich v Atletico Madrid
Jumatano Mei 4
Real Madrid v Manchester City

Fainali
Jumamosi Mei 28
**Saa 3 Dakika 45 Usiku

No comments:

Post a Comment