Wengi tunafafamu kitunguu maji, (pichani) lakini bado wengi wetu hatufahamu faida zake nyingine, ambapo pia kitunguu maji hicho huweza kuwa tiba au dawa vilevile ambayo hukupatia afya bora, kukuondolea uchovu wa mwili, kupambana na kuondoa bakteria mwili pamoja na kupandisha kinga ya mwili.
Kama, tujuavyo: ulaji wa vitunguu maji haswa vikiwa vibichi kwa kachumbari, inashauriwa sana na wataalamu wa Afya walau kutumiwa kwenye kila mlo wako wa siku itakusaidia sana katika kuuzuia mwili wako kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama vile, homa, mafua "flu" kifua kubana, kuondoa harufu mbaya mdomoni, kupandisha kinga ya mwili kwa kuzipa nguvu seli nyeupe na nyekundu za mwili kupambana na maradhi hayo.
HEBU LEO TUANGAZIE FAIDA NYINGINE ZA KITUNGUU HICHO ENDAPO KIKIWEKWA KWENYE UNYAYO WA MIGUU NA KUBANWA NA SOKSI KISHA KULALA NACHO USIKU MZIMA MIGUUNI:
Msomaji, je! unafahamu chini ya miguu yako kuna neva (mawasiliano) "meridians" nyingi tofauti zinazopeleka mawasiliano kwenye sehemu mbalimbali kwenye kila kiungo cha mwili wako "ndani na nje ya mwili" (zaidi milango6 ya fahamu) viungo vya ndani ya mwili wako, kamavile: figo, maini, ubongo, kibofu cha mkojo, moyo nk!?
ANGALIA KUHUSU:
(FootReflexology )
Ndio fahamu hilo, kwasababu chini ya unyayo wako kumefanyizwa mishipa mbalimbali ambayo hupeleka mawasiliano ya moja kwamoja kwenye viungo vya ndani ya mwili wako na nje pia, na ndio maana chini ya unyayo, inaelezwa pia na wataalamu kuwa huwenda ndipo sehemu pekee yenye hisia mchanganyiko kubwa kwa mwanadamu..endapo ikipapaswa au kuminywaminywa na inapaswa kuwekewa uangalifu na umakini mkubwa zaidi.
Mfano mdogo, ikiwa ubongo wako umechoka, unamaumivu ya kichwa "kipandauso" au una unauchovu wa mwili Fanyiwa masaji "massages" maeneo hayo ya miguu kwa kukandwakandwa na barafu au maji ya ubaridi, halafu uone, majibu utayapata kwa mwili wako kusawijika au kuwa sawa na ubongo wako kuwa-active.
Hivyo: sambamba na hayo kitunguu maji pia huweza kutumiwa kuamsha_hisia za viungo tofauti vya mwili stimulation" na kuvifanya vifanye kazi zake kwa ubora na kiwango kilichokusudiwa kiafya..
JE! HII IPOJE!?
Mfano kwa kushusha Homa: OnaHapa Kwanza: FAIDA
Hivyo: MATUMIZI:
Chukua kitunguu maji, kikate vipande mviringo kisha viweke chini ya unyayo wako, lala nacho mpaka asubuhi Majimaji yake yatakusaidia kiafya kurekebisha mfumo wa mwili wako na kupandisha kinga mwili yako kupambana na maradhi mbalimbali, lakini pia kukuondolea harufu mbaya ya miguu.
"Kwa wale wenye miguu inayotoa harufu sababu yamiguu kutoa jasho"
Fanya hivyo mara1 au mbili tu kwa wiki:::: kwa msaada zaidi watafute wataalamu wa TibaLishe waulizie manufaa zaidi ya kitunguu maji katika mwili, na matumizi sahihi ni yapi.
TAHADHARI
Kila chenye faida kina hasara, uangalifu unapaswa kuchukuliwa; Isipokuwa matunda, viungo au dawa-lishe hizi, hazina madhara sana kwa mtumiaji ukilinganisha na mitishamba.
Hivyo katika matumizi yake, kitunguu hiki hakipaswi kutumiwa zaidi ya mara1, na pia kikishakatwa kilichosalia kisitumiwe sababu kinaweza kutengeneza bakteria sababu ya uchachu-asidi wake.. hivyo vitunguu vizuri ni vile vilivyo-"fresh" tu.
(Kwenye makala zijazo, nitachambua, Maajabu na ni kwavipi mguu unaweza kutumiwa kuamsha hisia za kufurahia tendo ktk mahusiano)
Kupata makala kama hizi, tafadhali LIKE PAGE yetu hii (History And Amazing Things) inayopatikana kwenye facebook:
Kisha Share ili na wenginge wapate elimu, na maarifa uliyoyapata wewe kupitia kusoma hapa kwenye blog hii.
No comments:
Post a Comment