Picha kwa hisani ya mtandao (Google search) |
Na Stewart Meena
Je unafahamu ya
kwamba rangi ya Mkojo wako (Ashakhum sio matusi nitatumia jina lake halisi
badala ya kupunguza ukali wa maneno kusema "haja ndogo" ili tuelewane) inakupa
matokeo sahihi kuhusu hali ya afya yako?
Lakini pia wajua maji
ndio afya yako! Kwa sababu asilimia kubwa ya ufanyizo wa mwili wako ni maji
(Yaani damu+maji) na asilimia 25% ni mjumuisho mwingine kwenye mwili wako, mfn.
Nyama za ndani na nje nk.
Kama jibu ni hapana basi
"MAKALA HII" inakusu wewe moja kwa moja; Kwani rangi ya mkojo kwa
mujibu wa watalamu wa afya kupitia mahojiano mbalimbali niliyoyafanya na madaktari
na wataalamu wa tiba za asili, pamoja na tafiti zangu zingine nlizozifanya kwa
kuandika, au kusoma vitabu na majarida mbalimbali yahusuyo Afya:
(Nikiwa
Fani yangu ni Mwandishi wa Habari)
Nimekuja na majibu
kuwa kupitia Rangi ya mkojo wako unauwezekano mkubwa na ndio kipimo sahihi
kinachoweza kukupa ukweli wewe juu ya afya yako, kuweza kujua dalili za awali
kabla hata ya kwenda kupima maabara au kufanyiwa uchunguzi wa vipimo na
daktari.
Ndio ili daktari ajue
wewe unaumwa nini, au niugonjwa gani unakusumbua kwa wakati huo "ukiacha scanning na kupigwa picha ya
X-rays" Daktari huitaji kupima damu yako kwa matatizo ya nje ya mfumo wa
tumbo lako au kupima haja ndogo (mkojo) na (haja kubwa) ili kujua matatizo ya
ndani ya mfumo ulioko tumboni mwako.
Asilimia takribani
75% kwa 25% ya mwili wako ni maji, damu na nyenzo mwili nyingine, na vyote hivi
hufanya kazi kwa pamoja katika kuendesha maisha ya muhusika na ikiwemo mwili
kujitengenezea kinga yake ya kutosha na muhusika kuishi kwa afya bora.
Naposema matatizo ya
ndani ya mfumo uliopo tumboni (namaanisha magonjwa ambayo tunayahisi kupitia
eneo la tumbo letu) Kama vile, maumivu ya tumbo na yanayoweza kuambatana na vichomi
vya mara kwa mara, ambayo haya huweza kusababishwa na maradhi-mwili kadhaa ya mfumo
huo kama vile typhoid, amoeba,
Vidonda vya tumbo, matatizo ya figo na ini, Safura, kansa ya utumbo, Chango na
ngiri nk.
HEBU NA TUJADILI SASA
UTAMBUZI WA AFYA YAKO KUPITIA RANGI YA MKOJO.
Maelezo Mengine Kwa
kina:
Picha kwa hisani ya mtandao (Google search) |
Kwa kawaida mkojo
tuutowao una rangi mbalimbali (pichani) zenye majina yake kufuatana na rangi au
muonekanao wake, Na hiyo huchagizwa na mazoea ya mtu kuijali afya yake au
kuipuuza afya yake kwa kujua au kutokujua.
(Ndio mbona uvutaji
wa tumbaku au sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako,
na imeandikwa hivyo lakini bado watu wanakunywa pombe kupitiliza na kuvuta
tumbaku!?).
Sawa, sasa na hebu
tuanze kuzichambua rangi hizo (Pichani) na
ZINAVYOASHIRIA KWENYE AFYA YA MWILI WAKO.
No1. (Transparent)
Mweupe kabisa au
Mkojo usio na Rangi ya mkojo (Light yellow): Inaashiria Unakunywa maji mengi
sana, na sumu iliyoko katika mwili wako inasafishika vyema, Kwani figo yako kwa
msaada wa maji mengi mwilini huchuja sumu na taka mwili vyema kwa kutenga virutubisho
mwili na taka-mwili.
Kiafya, mkojo wa rangi hiyo (Nyeupe kama maji) sio
mzuri sana na huweza kuwa kwenye mwili wako kuna kasoro fulani au mmeng’enyo na
huenda uchakataji wa virutubisho na kuondoa sumu mwili haiko sawia kwako (balanced)
KIAFYA: Binadamu
anapaswa kunywa walau glasi 8 za maji kwa siku hadi lita mbili, na sio pungufu
kwa faida za kiafya, hivyo kunywa maji pia kupitiliza huleta matokeo mengine
tofauti kiafya.
Hivyo unashauriwa, utakapoona mkojo wako hauna rangi ya mkojo yani unatoka mweupe kama rangi ya maji hapo Kiafya kuna jambo haliko sawa (balanced) kwa hivyo unatakiwa aidha kupunguza kidogo unywaji mwingi wa maji au kuzingatia ulaji sahihi vya virutubisho mwili (balance-diet)
No2. (Lemonade) Hiyo
ni Excellent / great / better / Very good
Manjano isiyokoza
(Light yellow) inaashiria unakunywa maji
ya kutosha, afya yako iko vizuri na imara, hauna matatizo yoyote hivyo endelea
kufanya unacho kifanya kwa kula vyakula "balanced-diet", kula matunda
na kunywa maji mara kwa mara.
KIAFYA: Wewe unashauriwa
ushikilie hapo hapo katika utaratibu wako wa maisha ya kila siku "life
style" kwani mwili wako unajiendesha vyema.
Ili Kupata matokeo
haya: Unapaswa kula vyema vyakula vyenye virutubisho mwili vyote
(Wanga+Protini+Vitamini) ikiwemo na matunda kwa kuzingatia ulaji sahihi
(Balance diet) pamoja na unywaji wa maji mara kwa mara hata pasipo kuhisi kiu
(isipungue glasi 6-10 kwa siku)
No3. (Light like a
beer)
Majano isiyokoza
(yellow) yaani rangi halisi ya mkojo, inayokaribia kufanania na rangi ya asali
na isiyotoa harufu kali, inaashiria afya yako kwa wakati huo haina matatizo yoyote
na unazingatia ulaji mzuri wa vyakula na unaupenda mwili wako, #Isipokuwa
tatizo lako ni kuwa sio mnywaji mzuri wa maji ya kutosha vyema hivyo mwili wako
hauna maji ya kutosha.
KIAFYA:
Ukiona hivyo hupaswi
kuwa na wasiwasi, kwani kwa unywaji wako mdogo wa maji bado mwili wako
unajitengenezea maji ya kutosha pengine kutokana na aina ya vyakula uvilavyo
pia.
Isipokuwa unashauriwa tu kuongeza unywaji wa maji zaidi kwa siku kabla ya kula na baada ya kula unatakiwa usubiri angalau dakika20-30 hata kama hauna kiu ili kurahisishia figo yako ufanisi wake zaidi.
No4 (Amber) that is
Bad/Warning
Manjano
iliyochanganyika na uKijani kwambaali (Amber) Inaonyesha mwili wako upo upo
"kawaida" na una afya ingawa si mnywaji wa maji mengi na unasubiri hadi
uhisi kiu ndio unywe tena kidogo ndio maana unapokojoa mkojo hutoka na harufu
kali, hauzingatii ulaji wa virutubisho-mwili sahihi (yani wewe hauli
balance-diet kwa kuegemea aina ya vyakula fulani pekee na mara kwa mara, haswa
vile venye rangi ya uKijani kama mbogamboga na matunda" (mwili
unatengeneza vitamini na wanga pekee), ila kwa uchache unywao Mwili wako una
maji ya kutosha.
KIAFYA: Ukiona hivyo
ni ishara ya tahadhari au onyo mwili wako unakupatia ujumbe kuwa kuna kitu au
jambo haliko sawa mwilini mwako hivyo yakupasa ubadili mfumo wako wa maisha
mara moja; pia unatakiwa uzingatie unywaji wa maji hata pasipo kuhisi kiu,
pamoja na kula kwa kuchanganya vyakula vyenye kuupatia mwili wako madini ya
protini kwa wingi na Vitamini-C.
Protini inapatikanaje!?
Hii hupatikana kwa kula vyakula kama Nyama nyekundu (Ng'ombe, mbuzi nk) pamoja na vitu kama Maharagwe, samaki, maziwa nk.
No5 (Very bad /
Worse)
Manjano iliyochanganyika
na nyekundu au rangi ya udongo (Brown) isiyo na harufu kali ya mkojo na yenye
harufu kali au ya wastani, Inaashiria Upo kawaida tu ila mashakani, sababu wewe
kwanza si mywaji wa maji, pili hauzingatii ulaji sahihi wa chakula na pengine
hauli kwa muda sahihi pia na upo hatarini kupatwa na Vidonda vya tumbo (ulcers) Tatu,
kuna aina ya kemikali unazokula au kunywa na kusababisha mwili kukaushwa maji
yake kwa wingi zaidi.
KIAFYA:
Kunywa maji ya
kutosha kwa siku mbili au tatu, na kama hali ikiendelea hivyo yakupasa umwone daktari
upesi kwa vipimo vya mkojo wako kujua kama una UTI, baikteria mwilini waletwao
na unywaji wa maji machafu "typhoid" nk.
LABDA NIELEZEE HAPA
KIDOGO:
Kuna aina ya vinywaji
na vyakula tunavyokula ambavyo huweza kufyonza maji-mwili kwa wingi zaidi au
hata kazit unazozifanya kwa kupata mkate wetu wa kila siku.
Mfano kazi za kutumia
nguvu sana, kukaa karibu na moto kwa muda mrefu zaidi, kufanya kazi viwandani
haswa vile vyenye kutumia nishati ya umeme au moto na makaa ya mawe nk.
Kutembea kila siku
umbali mrefu tena juani kwenda na kurudi; kubeba mizigo mizito nk inafyonza
sana maji mengi mwilini.
Ukiwa mpasuaji mbao
kunywa maji yakutosha, ukiwa unafanya kazi ya upishi hakikisha unakunywa maji
ya kutosha tena mara kwa mara, ukiwa fundi ujenzi, makenika, injinia, dereva,
mbeba mizigo mizito, mfanyaji mazoezi mara kwa mara, mwana michezo, mchumia
juani nk. Hakikisha chupa ya maji haibanduki pembeni yako na unakunywa maji
mengi mara kwa mara.
Ndio maana wataalamu
wanasema na kushauri: Ikiwa unaishi kwenye ukanda na mikoa yenye joto kali (Dar
es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro,
Dodoma, Mara, Mwanza, Singida, Mtwara, Kilimanjaro "sehemu baadhi"
nk) yakupasa unywe maji mengi kwa siku kwa sababu maeneo hayo humfanya muhusika
kutokwa na jasho jingi kupita kiasi hata bila kufanya kazi nzito au kufanya
mazoezi.
Kutokunywa maji hayo
hupelekea mwili kudhoofu, kuharibu mfumo mzuri wa uchujaji wa sumu mwili,
chakula kutokusagika na kuchaguliwa vizuri nk. Na ikidumu hivyo kwa muda mrefu
ndipo mtu unaweza kupatwa na #magonjwa hatari zaidi kama vile figo kufeli,
kupata vidonda vya tumbo, ini kuungua, Kinga za mwili kushambuliwa na magonjwa
mengi zaidi na kwa mjumuisho wa hayo yote na pasipo kupata suluhisho la
kitabibu kama kumuona Daktari kinachofuatia ni kifo tu
hakuna cha ziada.
Muhimu kutambua ni
kuwa: Mwili wa Binadamu hutegemea kupata maji yake kupitia pia aina ya vyakula
unavyokula kila siku, matunda, vinywaji, maji yenyewe na virutubisho-dawa,
ambapo kwa mjumuisho wavyo mtu huweza kuwa na maji ya kutosha mwilini, kuwa na
afya njema, kinga za mwili kufanya kazi sawia, na Kupambana na maradhi
nyemelezi, mwisho maradhi shambulizi yatakupitia pembeni (utayasikia kwa jirani
tu)
Mwili unafanyizwa na
seli mbili za damu (nyeupe na nyekundu) ambazo hizi ndio ngao zetu, kinga na
ndio huyafanya maisha yetu yasonge.
Ndio maana
ukipungukiwa na damu wewe ni wa ICU, ukipungukiwa na maji wewe ni wa ICU pia na
uzembeaji kidogo, malaika mtoa roho utamuona akipita pembeni yako mara kwa mara.
(NDUGU ZANGU AFYA NI
MALI NA NI UHAI WAKO USIUCHEZEE
Swali la kujiuliza
kabla ya kuhitimisha ni kuwa: Je! Unawezaje kuchezea uhai wako na afya yako!?
Binadamu huchezea
afya yake na kuhatarisha uhai wake kwa kufanya mambo mbalimbali (mengi
unayafahamu) na ndio maana unaweza kumsikia mtu akisema maisha yenyewe mafupi
haya!?
Sababu anafanya jambo
ingawa anatambua madhara yake, na hii ni kweli kabisa watu wengi walioelimika Wasomi
ndio haswa huongoza hapa: ni walevi wa pombe kali, watumiaji wa madawa ta
kulevya, hawazingatii ulaji sahihi na kwa wakati hupuuzia taarifa kama hizi
(uisomayo) na mwisho wa siku pyuuuuuuu!
They disappear forever!
Sio ajabu kizazi
chetu cha leo (karne ya 21) kumuona kijana umri mdogo kabisa lakini Kimuonekano
kashaZeeka kabisa, ndio si tunawaona mtaani huko!?
Wazee wetu (miaka ya
60, 50, 40, kurudi nyuma) ukiwaona leo hii bado ni imara licha ya changamoto ya
maisha na umaskini na huwezi kuwasikia wakiwa na matatizo kwa wingi kama
tuliyonayo vijana wa miaka hii (80, 90, 2000 kuja mbele) ambapo magonjwa kama
presha, kizukari, miguu kuvimba, utasa, kupoteza nguvu za kiume, yote haya anayo
mtu mmoja..
HIYO NDIO KUCHEZA NA
AFYA NA UHAI WAKO PIA.
Ndio! Ukipatwa na
hayo yote mwisho wa siku unafikiri nini kinafuatia!? Saa nyingine hebu tuache
kumbebesha MUNGU lawama na mizigo asiyostahili, amekupa maarifa ya kutambua
mema na mabaya yatumie!?
Acha kuwa kichwa_maji
(ashakhum sio matusi) Huwezi ukaambiwa unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari
kwa afya yako bado unakunywa! Tumbaku, bangi, cocaine ni hatari kwa afya yako
bado unavuta!?
Kunywa maji mengi
bado hunywi!, kula mlo kamili (balance diet) bado huli wakati afrika
tumejaaliwa vitu vyote hivyo, ungekuwa unaishi jangwani (deserts) ungesemaje!?
Wewe si mnywaji wa
maji, hivyo Endelea kunywa maji ya kutosha walau glasi 4-8 au zaidi kwa siku,
ukipata #Stakafeli kula, juisi ya Miwa, ndizi, nanasi, chungwa, limao,
tangawizi, karafuu, nazi, mihogo, #maharagwe, viazi "sio vya kukaanga na
mafuta" kula.
Embe, limao, nyama,
bamia, mboga za majani kulaaa-uwiiiiii!
Hahaha! Vingine unavijua! (Muhimu hakikisha mlo wako unajumuisha virutubisho na
madini ya - Vitamini, wanga na protini)
Makala zinazofuata,
ntajaribu kukuorodheshea baadhi ya vyakula na matunda ambavyo huweza kuupatia
mwili vitamini, wanga na protini.
KUMBUKA: Rangi ya mkojo inayotoka na “Uwekundu (mfano wa damu) na mkojo unaotoa harufu (Red urine colour) Ndugu yangu hapo kimbilia kituo cha Afya kilichopo karibu na wewe, na sio kuendelea kukaa nyumbani na kutumia muzugwa, dawa za miti shamba (hapo punde tunaweza kukuimbia ule wimbo wa parapanda)
RANGI HIYO KIAFYA: Mwili
Upo kawaida (sababu bado unaweza kujihisi una nguvu kiafya) ingawa sumu mwili
iliyopo katika damu haichujwi vyema na kusafishika na figo
zako, yaani Ini
limekataa kufanya kazi yake, hivyo madhara ya hivi muda mrefu huweza kuzalisha
matatizo katika figo zako kufa kabisa, kupata vichomi vya mara kwa mara, tumbo
kuuma, mwili kuishiwa nguvu nk.
HEBU SOMA HAPA KUHUSU
KUJUA KAMA FIGO ZAKO ZINA HITILAFU:
MKOJO wenye Rangi ya
Pinki, damu ya mzee na inayokaribia kuwa kama Nyekundu
(Blood colour). Kama
hujala matunda yoyote, chakula, au kinywaji chenye asili ya uwekundu kwa
wingi" (juisi ya rangi, ubuyu wa rangi nk)
Au Mwanamke haupo kwenye
siku zako za hedhi (ashakhum sio matusi)" basi huwenda una matatizo makubwa
kwenye mwili wako, ambapo damu hulazimika kuchanganyika na njia ya mkojo
"kwenye kibofu chako cha mkojo".
Ukiona dalili hiyo
tambua kuwa Inaweza ikawa sio ishara mbaya kwa mara moja ila ikijirudia kwa
muda wa siku zaidi ya 2 au 3 ni tatizo hilo, tena lenye kuhitaji vipimo na
matibabu ya kidaktari upesi zaidi.
Muone daktari haraka
sana Ufanyiwe Vipimo kujua kama, unakabiliwa na magonjwa yepi.
LABDA NIELEZEE KIDOGO
HAPA:
Mara nyingi (sio
zote) mkojo kutoka na rangi ya kama damu huwa inachagizwa na kuchanganyika na
damu, na hadi ikitokea hivyo zaidi ya mara2 au siku2, (Isipokuwa wanawake
wakati wa hedhi) basi kuna jambo ambalo halipo sawa mwilini. "Mwili una
dosari fulani)
Na huwenda muhusika anakabiliwa
na magonjwa kama vile ya zinaa (mf.Kaswende, pangusa nk); au kinaMama kuwa na
tatizo kwenye mlango wa kizazi "mwanamke", kuathirika kwa ini, tatizo
katika kibofu chako cha kuhifadhia mkojo, njia ya kupitishia mkojo, au pengine
inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, Ini au uvimbe kwenye njia hiyo ya mkojo
nk.
PATA USHAURI WA
KIDAKTARI NA PIMA AFYA YAKO MAABARA AU KITUO CHA AFYA AU KWA KUJICHUNGUZA
MABADILIKO YAKO MARA KWA MARA MWENYEWE HUKU UKIJIPENDA NA KUILINDA AFYA YA
MWILI WAKO PIA.
ENDELEA HAPA ZAIDI (Chanzo kingine):
Tafadhali waweza tufuatilia pia Facebook kwa page yetu ya: (FB-Page)
No comments:
Post a Comment