Thursday, 8 November 2018

UKWELI USIOUJUA KUHUSU RADI (THUNDER STORM) NA CHANZO CHAKE (LIGHTNING)



Na Stewart Meena

Radi hutokana na mvutano wa hali ya hewa kinzani katika tabaka la juu la mawingu ambapo ukinzani huo huchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa, mgando wa barafu “kuganda na kuyeyuka” matone ya mvua pamoja na mwendokasi wa mzunguko wadunia “kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake (rotation) na kuzunguka jua (revolution) pamoja na sayari nyingine.
Kimsingi katika dunia yetu ambayo ni sayari ya3, kumegawanyika karibu matabaka 4 ya mawingu, ambapo tabaka la juu kabisa hujulikana kama (stratosphere) na eneo la kwanza la tabaka hilo, hutafsiriwa kama mwisho wa upeo wa macho yetu kwa kuangalia angani, ambapo eneo hilo sio eneo la mawangu halisi.

Eneo unapoona rangi ya bluu na nyeupe hapa ndipo mwanzo wa mzalisho wa mawingu yenye barafu katika tabaka la pili la juu yake ambalo hilo ndilo husababisha mvua kunyesha pindi barafu inapoyeyuka kwa joto kupenya eneo hilo.
Eneo hili la kwanza sio mawingu halisi isipokuwa ni msafirisho wa mvuke na ukungu (fogs) unaozalishwa kwa baridi kuendelea kuzidi kwani kwa kadiri unavyopanda juu kutoka usawa wa bahari ndipo ongezeko la baridi linapotokea kwa wale waliobahatika kupanda mlima kama Kilimanjaro ukiwa karibia kileleni ukiangalia chini huwezi kuona villivyopo chini badala yake utaona ukungu huo mweupe unaotanda eneo hilo, na hii ndio sababu maeneo yote ya uwanda wa juu kaskazini na kusini kwa Tanzania yetu kunakuwa na baridi kali muda wote wa mwaka kutokana na mwinuko wao kutoka usawa wa bahari. Mfano:Iiringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Lushoto-Tanga nk.

Mvutano wa hewa nayozungumzia ni hewa inayopatikana eneo la chini ya tabaka la kwanza la mawingu (sehemu tuliyopo) inayoitwa ‘oxygen’ itolewayo na mimea na ile ya ‘carbon-dioxide’ tuitowayo wanadamu na wanyama wengine, na ile inayopatikana tabaka la juu la mawingu naitrojeni ‘nitrogen’ hizi huweza kuchagiza tabia tofauti ya hali ya hewa katika tabaka hilo la kati na la juu la mawingu na hata eneo tulilopo la ardhi na lile la chini kabisa ya ardhi.
Na hapo ndipo huwa chanzo cha kuzaliwa kwa nishati ya radi, uwepo wa tufani kadhaa duniani kama vile vimbunga na zile za baharini, uwepo wa tetemeko la ardhi ikisababishwa na kusafiri kwa volkaniki (volcano) chini ya ardhi n.k

TUNAPOSEMA RADI NDIO NINI, NA KWANINI HULETA MADHARA DUNIANI?

Radi (thunder) sio muungurumo, kama wengi mnavyodhani ila radi ni mwale wa kama shoti ya umeme unaotokea kabla ya muungurumo na baada ya muungurumo kupita; mwale huo ni nguvu kama nishati ya umeme ambao huu huwa na vipimo-nishati zaidi ya umeme (voltage & watts) ambayo hii huwa na kiasi cha Vol. zaidi ya elfu-10 ukilinganisha na ile ya umeme inayoanzia (vol.110/220-1000)
Kama tulivyoona mwanzo kwanini radi hutukia, lakini bado watu huwa na maswali mengi kwanini mara kadhaa imekuwa ikileta madhara kwa kupiga miti’ nyumba na watu wakati mwingine, hivyo kuhusisha radi hiyo na imani za kishirikina pamoja na kuvaa aina ya mavazi.

KUNA UHUSIANO GANI:
Kitaalamu hakuna uhusiano wa radi na imani za kishirikina isipokuwa kuna mazingira yanayoweza kuifanya radi kupenya kwenye mawingu na kushuka moja kwa moja aridhini na kuleta madhara mahala ilipofikia (gravitation area).
Radi huambatana na mvua na mvutano wa nishati kama ya msumaku, na endapo ikitokea ikawa inasafiri angani na kukawa kunauvutano wowote wa mfumo wa nishati kama ya umeme, umande umande wa barafu na mazingira ya mvua huweza kupiga na kushuka hadi eneo hilo.


Ndio maana nyumba zenye umeme huekewa chuma flani ya rangi ya shaba na kuchimbiwa ardhini ili kuzuia radi hiyo kuwa na uwezekeno mkubwa wa kuipiga nyumba hiyo, na hivyo ni hatari zaidi kutumia umeme wa moja kwa moja pasipo kuweka kizuizi hicho kwasababu nishati ya radi huwa ni mara maelfu zaidi ya umeme wa kawaida

Na inapotokea radi hiyo kupiga basi tambua kuna mvutano uliopo katika eneo hilo, mvutano ambao huivuta nishati ya radi na kuileta hadi aridhini na kisha kuleta madhara kwenye eneo husika palipo na kani mvutano huo (gravitation).


Kuna uhusiano mkubwa sana uliopo kati ya nishati umeme wa radi na umeme wa majumbani, Uvutano wa sumaku, mvukizo wa joto la ardhi haswa maji yanaponyweshwa juu yake; na uwepo maji haswa yale ya mvua pamoja na yale ya bomba na aina ya nyenzo yanayopitia (mipira au chuma) wakati radi ikipiga.
Mabomba yaliyotengenezwa kwa chuma cha zinki, aluminium na shaba, hupitisha umeme na hivyo kwa kuwa maji hupita ndani yake, na ukayatumia wakati radi ikipiga kuna uhatarisho; lakini yale yaliyotengenezwa kwa mipira huwezi kuwepo kwenye uhatarishi ukilinganisha na hizo nlizozitaja.

MAVAZI:
Kuhusu mavazi hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kupigwa na radi na aina ya mavazi tunayoyavaa (Mfano watu husema ukivaa mavazi mekundu ni rahisi zaidi kupigwa na radi kweli?) Jibu ni kuwa sio kweli.!

Isipokuwa mavazi tunayoyavaa na tabia ya hali ya hewa kwa wakati huo, kwa kushirikiana huweza kuleta uwezekano huo kwa kufuata tabia ya miale ya radi inavyosafiri pekee na eneo ulilopo wakati huo kama ilivyo kwa tabia za vyanzo vya nishati nyingine kama jua na moto.
  • Mfano kivizikia (Physics): Jua hutufikia kwa njia a mnururisho;

  • Umeme au moto husafiri kwa njia ya mpitisho;
Hivyo katika mavazi nayo huwa na tabia yake katika kuakisi na kuvuta miale hiyo ya nguvu za sumaku, nishati ya jua, moto na nguvu nyingine za nishati ya umeme kama ilivyo kwa radi.

Mfano: mavazi meusi husharabu moto, joto au nishati ya jua;
Maazi meupe huakisi hali hiyo apo juu.

Mavazi mengine kama ‘Mekundu, Njano, Zambarau nk’ hayaakisi wala kusharabu nguvu hizo za nishati isipokuwa haya huwa na uwezo wa kutunza joto hilo kwa muda flani, na ndio maana katika uvutano wa sumaku mavazi haya na yale yenye asili ya unailoni au mipira huweza kuzalisha miale mfano wa cheche za moto ambazo hizi hutoa muangaza.
(Fanya zoezi moja: Chukua moja ya mavazi hayo, kasha yavae mwilini au yasugulie kwenye nywele zao kisha yafikiche yenyewe kwa yenyewe gizani usiku utaona yakitoa miale hiyo mfano wa cheche)

NINI KINATOKEA HAPO MTU KUPIGWA NA RADI NA UNAWEZA KUJIKINGAJE!:

Kwa utangulizi nilioueleza katika tafiti na makala yangu hapo juu: Imeelezwa kitaalamu kuwa radi huambatana na nishati nyingine duniani, na kuna uhusiano mkubwa sana kati yake na mvua/maji; uvutano wa sumaku na hali-joto ya mahali haswa ardhi wakati radi inapiga pamoja na mwingiliano wa hewa tofauti inayochagizwa na kujizungusha kwa dunia katika mhimili wake (Rotation) na kulizunguka jua (Revolution).
KUJIEPUSHA: usipende kukaa chini ya miti wakati mvua inanyesha na huku ukiwa umevaa mavazi yoyote yenye uwezo wa kutengeneza Usumaku yanapogusana (rejea kwenye mavazi juu); kuweka kizua radi majumbani unapofunga umeme lakini usipende kusikiliza redio au kutumia internet ukiwa kwenye eneo la mwinuko na penye umande umande au chini ya miti wakati mvua ninanyesha.

Unashauriwa kuepuka kutumia maji kwenye mabomba yasiyo ya mpira wakati radi inasafiri, kuoga wakati huo nk; lakini pia ni vyema ukapunguza matumizi makubwa ya vifaa vinavyotumia umeme wakati huo kama vile kuwasha Tvs, Radio, kutumia pasi na Heater kupikia au kuchemshia maji kuchaji simu kwa wakati mmoja.
MWISHO: radi ni mwale ule unaoonekana kabla ya muungurumo kusikika, na muungurumo huo huzalishwa kutokana na nguvu za radi hiyo (mwale) na mgandamizo wa barafu (Mawingu mazito yaliyoganda na matone ya mvua kugusa eneo hilo kutoka tabaka la juu zaidi la mawingu) msuguano wa hali za hewa kinzani.

Tahadhari: Radi ni kama ilivyo kwa nishati ya umeme, na huweza kuleta maafa kwa kuwakisha moto au kumuunguza muhusika, usikae karibu na nyaya za umeme (haswa unaosafirisha voltage kubwa) wakati mvua zinanyesha au radi kupiga.
JIFUNZE ZAIDI NAMNA GANI EATH-QUAKE NA THUNDER STORM’ HUTOKEA KWA KUBOFYA VISAIDIZI HAPA CHINI NA VILIVYO NA RANGI BLUU JUU:

Radi

Tetemeko la Ardhi

2 comments:

  1. Read More: https://www.nationalgeographic.com/science/article/science-of-superbolts-worlds-strongest-lightning-strikes?cmpid=org=ngp::mc=social::src=facebook::cmp=editorial::add=fb20231008science-superbolts&linkId=239832449&fbclid=IwAR1Ok_-xy5cOAndc-Gkp9PleA0xbjeL3Jc24PzfFRVBz2rDOwZwDRlBov40

    ReplyDelete