Halloween,
hujulikana zaidi kama “Mkesha wa sikukuu ya Watakatifu Wote, na Husheherekewa
unakoishi”
Katika nchi kama Canada na Marekani
Halloween ni maharufu sana na husheherekewa kila ifikapo octoba 31 kila mwaka.
Hata hivyo sherehe hizo, zinazofanywa
wakati wa Halloween, kwasasa zimeenea katika sehemu tofautitoauti Ulimwenguni
pote.
Katika sehemu Fulani, kuna
sikukuu ambazo ingawa zimepewa majina tofauti, lakini zina kusudio kama la Halloween:
HALLOWEEN NI
NINI? “Halloween ni kuwasiliana na Viumbe Wa Roho (Mizuka) iwe ni kupitia roho
za Wafu, Wachawi, au hata Ibilisi na Malaika zake waovu.
Mara nyingi Alama
inayotumiwa na Wafuasi wa Imani hiyo ni (Pembe tatu-tatu 3/3 pamoja na alama ya
meno manne-juu & chini)
Huenda wewe binafsi Usiamini kwamba kuna Viumbe wa Roho wenye Nguvu zisizo za kawaida, na Pia huenda ukawa na Maoni tofauti ya kwamba Kushiriki katika Sherehe ya Halloween na Sherehe nyingine zinazofanana na hizo ni njia ya kujifurahisha tu na ya Kuwafundisha Watoto wako kuwa wabunifu.
Hata hivyo watu wengi wanaona Sikukuu hizo kuwa zenye Madhara kwa sababu zifuatazo:
Kitabu cha Encyclopedia of American Folklore (ensaiklopedia ya Desturi ya Wamarekani) kinasema: “Halloween inahusisha hasa kuwasiliana na Viumbe wa roho ambao wengi wao hutisha au kuogopesha.”
Huenda wewe binafsi Usiamini kwamba kuna Viumbe wa Roho wenye Nguvu zisizo za kawaida, na Pia huenda ukawa na Maoni tofauti ya kwamba Kushiriki katika Sherehe ya Halloween na Sherehe nyingine zinazofanana na hizo ni njia ya kujifurahisha tu na ya Kuwafundisha Watoto wako kuwa wabunifu.
Hata hivyo watu wengi wanaona Sikukuu hizo kuwa zenye Madhara kwa sababu zifuatazo:
Kitabu cha Encyclopedia of American Folklore (ensaiklopedia ya Desturi ya Wamarekani) kinasema: “Halloween inahusisha hasa kuwasiliana na Viumbe wa roho ambao wengi wao hutisha au kuogopesha.”
SIKUKUU
ZINAZOFANANA NA HALLOWEEN ULIMWENGUNI POTE.
Kwa Ujumla Halloween huonwa
kuwa sikukuu kwa wa Marekani, Lakini sasa sikukuu hiyo inapendwa sana katika
sehemu nyingine ulimwenguni, istoshe kuna sikukuu nyingine zinazofanana na hiyo
kwa maana kwamba Zinasheherekewa kuwapo kwa viumbe wa roho na utendaji wao
(Kufanya mila za matambiko).
Zifuatazo ni baadhi ya Sikukuu
Maarufu zinazofanana na Halloween ambazo zinapatikana Ulimwenguni pote.
Asia – sherehe ya ‘BON’
Afrika – dansi ya ‘EGUNGUN’
Amerika kusini –
‘KAWSASQANCHIS’
Amerika kaskazini na Ulaya
– ‘SIKU YA WAFU’ na ‘HALLOWEEN’
CHANZO CHAKE NI NINI?
Zipo baadhi ya imani
mbalimbali ambazo zinaelezea Chanzo kuhusu Roho Hawa wenye nguvu na
wasioonekana kwa macho ya kawaida, ambapo kila mmoja kwa Tamaduni yake ana Namna
anavyoweza kuelezea Viumbe hao wasionekana:
Baadhi Huamini kwamba; ni
Majini Yanayonyonya Damu za watu, mbweha n.k.
Wengine husema Roho hawa
huhusiana sna na Wachawi wanaowawangia watu usiku wakiwa wamelala, au kuhusisha
na imani za Iluminati (Feemason) ambavyo vyote hivyo hutendekea gizani au kwa uficho
na usiri mkubwa.
ISHARA ZINAZOTUMIWA:
WASELTI wa kale walijaribu Kuwatuliza
viumbe waovu kwa kuwapa Peremende, Baadaye Kanisa liliwatia watu moyo waende
nyumba kwa nyumba mkesha wa sikukuu ya Watakatifu wote ili kuwaombea wote
waliokufa katika Imani, na kupewa chakula kama malipo (matambiko)
Mwishowe hiyo ikaja kuwa
Desturi ya Halloween, na watu walienda nyumba kwa nyumba wakiomba Peremende na Kuwatisha
watu wasiowapa peremende.
MAVAZI YANAYOTUMIWA:
Waselti walivaa vinyago usoni
ili roho waovu wadhani kwamba wao ni miongoni mwao hivyo wasiwadhuru, Kanisa liliingiza
desturi za kipagani katika sherehe za sikukuu za wafu na siku ya Watakatifu
wote.
Baadaye waadhimishaji walienda
nyumba kwa nyumba wakiwa wamevalia kama watakatifu, malaika na Mashetani.
MABOGA:
Aina flani ya Boga linaloitwa Tanipu lilichongwa na kutiwa mshumaa hutumika katika sherehe hizo ikiaminika husaidia kuwatuliza au kuwafukuza roho waovu.
Watu flani huamini na husema
kwamba boga na mishumaa hiyo uliwakilisha nafsi zilizokuwa zimezuiliwa
toharani, ambapo baadaye watu walianza kutumia Maboga ya kawaida endapo yale ya
tanipu yasipopatikana.
KUMBUKA: Halloween na
sikukuu nyingine nyingi zina asili ya Kipagani
na huhusisha sana kuabudu watu waliokufa ambapo hata hivi wa leo, watu
wanaoisheherekea katika Nchi zao mbalimbali, idinazidi kuongezeka, na wengi wao
Hawatambui baadhi ya ishara na Mapambo ya majumbani wanayotumia Yanahusiana na
Wapagani waimani hizi.
Maelfu Ya Jamii Ya Kichawi
inayoitwa WICCAN,
Ambayo hufuata desturi za waselti wa kale bado huiita ‘Halloween’ kwa jina lake
la kale, yaani Samhain, nao husema kwamba huo ndio usiku mtakatifu zaidi katika
mwaka.
Gazeti
la USA TODAY likimnukuu mtu aliyejiita Mchawi linasema;
“Watu wa imani tofauti hawatambui kuwa Wanasheherekea sikukuu yetu pamoja nasi,
Tunafurahia jambo hilo”
HISTORIA YA HALLOWEEN
‘Hallow’ ni neno la kale linalomaanisha (mtakatifu) na ‘ween’ ikimaanisha (usiku) ambapo kwa ujumla muunganiko wa neno ‘Halloween’ linamaanisha (Usiku mtakatifu)
Karne ya-1 (w.k)
Watu wa Roma ya kale waliwashinda
waselti na
wakaanza kufuata desturi mpya za Samhain zinazohusiana
na roho za waovu.
Karne ya 5: (k.w.k)
Waselti wengi waliadhimisha
sherehe ya Samhain mwishoni mwa mwezi
Oktoba, mwezi ambao waliamini Mizuka na roho waovu walizurura duniani kuliko
wakati mwingine wowote.
Karne ya 7: (w.k)
Inasemekana kwamba Papa Boniface wa4
aliyeanzisha sherehe ya kila mwaka ya watakatifu wote (kwa wakatoliki) ili
kuwakumbuka Wafia_Imani wote.
Karne ya-11 (w.k)
Novemba2 inawekwa kuwa siku
ya Wafu, yaani siku ya kuwakumbuka wote waliokufa.
Karne-ya 18 (w.k): jina la
siku ya ‘Halloween’ linaanza kuonekana
katika machapisho.
Karne ya19 (w.k): Maelfu ya
watu wa IRELAND wanaohamia Marekani walikuja na desturi zao za Halloween na
baada ya muda, desturi hizo zinachanganywa na zile za wahamiaji wengine kutoka
Uingereza, Ujerumani, Afrika na sehemu nyingine ulimwenguni.
Karne ya 20 (w.k) Halloween inakuwa sikukuu maarufu zaidi nchini
Marekani.
Karne Ya 21: Halloween inakuwa
biashara kubwa inayowaingizia Wafanyabiashara mabilioni ya Pesa Ulimwenguni
pote kama ilivyo kwa sikukuu nyingine za iddi, au xmass.
NUKUU:
“Kwa sababu ya mambo yote
nliyoyazungumza katika makala haya, ni jambo jema na la hekima kulizingatia kwa
kujua chanzo cha HALLOWEEN na sikukuu nyingine zinazofanana na hiyo ili kujua
mambo kiundani na pia itakusaidia kuepuka kwa kujiunga na watu ambao husheherekea
sikukuu kama hizo”
SOURCES:
All saints day: © The Bridgeman Art
University of Michigan
Library And Google; customs,
Wikipedia,
Archieves; pope Boniface
IV.
No comments:
Post a Comment