Miche ya Minyanya iliyopandwa kwa kufuata contua. Picha na iStock |
Ikiwa ungeulizwa kutaja tunda bora zaidi duniani , labda nyanya haitakuwa
akilini mwako, Lakini unalolihitaji kulifahamu ni kuwa nyanya ni tunda na huzalishwa
kwa wingi zaidi duniani kuliko tunda jingine lolote.
Baadhi ya watu hudai kuwa tunda la embe ndilo maarufu zaidi duniani kwa
misingi kuwa linaliwa kwenye nchi nyingi zaidi kuliko matunda mengine!.
Lakini ikiwa utapima umaarufu kwa uzalishaji kote duniani, na uhitajio mkubwa
zaidi kwa matumizi ya binadamu, utagundua kuwa nyanya zinaongoza (kama kiungo
muhimu cha mboga/chakula) na na matunda mengine kama Embe, ndizi na mengineyo yapo
nyuma ya tufaa kwa nyanya.
Tunda la nyanya huwa na muonekano wa rangi mbili (njano na Nyekundu) zikiwa zimeiva tayari kwa matumizi |
Nchi inayoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa tunda la ndizi duniani ni India,
ambapo Kuna zaidi ya tani 100 za ndizi ambazo huzalishwa kila mwaka.
Lakini kuhusu Nyanya, ambayo huweza kuliwa bila kupikwa (kama kwenye
kachumbari) au kwa kupikwa (kwenye mboga/chakula), Uzalishaji wake duniani kote
ikiwa ni tani 170 za nyanya, ambazo huzalishwa kila mwaka, na hivyo tunda hili
kupita hata uzalishaji wa ndizi.
Wengi huchukulia nyanya kama mboga, lakini ukweli ni kwamba nyaya ni tunda
kama nlivyokwambia kwa kuwa, kama ilivyo kwa matunda mengine Nyanya nayo ina mbegu
hali ambayo huiweka katika familia ya kundi (mimea jamii) la matunda.
Kwa utofauti wa nyanya Kuna zaidi ya aina 20,000 ya nyanya duniani kote,
kwa kujumuisha hata zile ziotazo maporini.
HISTORIA NA CHIMBUKO LA MCHE (Mmea) WA MNYANYA:
Muonekano wa Nyanya Nyekundu. |
CHIMBUKO / Chanzo Wikipedia,
Mnyanya ni mmea, ambao
daima huota na kukua kwa kutambaa, na hukuzwa kwa makusudi ya kutumiwa na watu,
Matunda yake yanaitwa nyanya.
Miongoni mwa
aina zaidi ya (makumi elfu) ya nyanya zinazozalishwa, kati ya hizo, nyingi sana
huwa na rangi nyekundu haswaa pindi inapoiva, huku nyingine zikiwa na rangi ya
manjano au machungwa.
Mnyanya huwa na
urefu wa mita 1-3 na huwa na shina laini ambalo mara nyingi hujibebelesha
kwenye mmea mwingine, au huitaji kushikishwa mimea mingine au miti kwa ajili
iweze kutambaa na kuzaa matunda mengi zaidi.
Mche wa mnyanya ukiwa umetokeleza maua, ambayo huonekana kwa rangi ya njano. Picha na iStock |
Majani yake huwa
na urefu wa sentimeta 1-25, na petali zake hufikia 5-9, huku Majani ya shina la
nyanya huwa na vinyweleo au (vimwiba vidogovidogo), Maua yake huwa na upana wa
sentimita (sm-1-2), na huonekana kwa rangi ya manjano, na majani yake
yakigawanyika sehemu tano (5leaf branches) na huvunwa kuanzia miezi3, 6 hadi mwaka
mmoja.
Historia
Nyanya zikiwa zimevunwa shambani na kuwekwa kwenye matenka tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda viwandani vya kusindika nyanya hizo. |
Asili ya mnyanya
ni Amerika ya Kusini. Na historia yake
huonesha kuwa mimea hii ilianzia nchini Peru, na Mimea hiyo ya mwanzo ya Peru
ndiyo imekuja kuwa na aina hizi nyingi za nyanya tulizonazo duniani hivi wa
leo.
Spishi moja
ilisafirishwa kutoka Peru mpaka Meksiko (Mexico) kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na Ushahidi
unaonyesha kuwa hapo awali mmea wake ulikuwa tunda dogo lenye rangi ya njano (kama zile ziotazo maporini).
Neno la
Kiingereza ‘tomato’, lenye maana ya nyanya, limetoka ana Nsha ya Manati
‘lomatl’.
Mtaalamu wa mmea
wa kifaransa, Joseph Pitton de Tournefort, alitoa jina la kisayansi
’Lycopersion esculum’ kwa nyanya, na wakati huo nyanya ilifikiriwa kuwa ina
sumu ndiyo maana ilipewa jina la mito lenye maana ya tunda la mbwa mwitu.
Watu wa Acret na
wengine wanaanza kutumia nyanya kwenye mapishi yao, wakti huo ikilimwa huko
Peru, mnamo mwaka 500 K.K, Baadaye nyanya zilizobadilika na kuwa laini, kubwa
kutoka kwenye mboga laini, na kuanza kushamiri huko Amerika ya Mwanzo, na inaaminika
hii ndiyo asili ya nyanya tunazotumia sasa.
Baada ya utawala
wa wahispania huko Amerika, Wahispania walisambaza nyanya kwenye makoloni yake
yote mpaka Kusini mwa Asia na baadaye Asia yote, na baadaye walipieleka nyanya
hiyohiyo Ulaya pia kwa biashara.
Nyanya zilizozalishwa
wakati huo zilikuwa nzuri sana na bora, ndipo kilimo chake kilianza rasmi mnamo
1540 sehemu mbalimbali duniani ikiwemo eneo la miditeraniani.
Nyanya zilianza
kuliwa rasmi huko Hispania mnamo 1600, baada ya kufuta uvumi wa kwanza wa kuwa
nyanya ni sumu, ndipo Mwaka 1692, kilipatikana kitabu kinachoaminika kuwa
kilichapishwa huko Naples, kilichokuwa
kikielezea mapishi yaliyohusika zaidi na nyanya kama kiungo.
Uingereza
Kwa Kiswahili cha kienyeji, "Matomanti" ni miongoni mwa jamii maelfu za tunda la nyanya, zikipatikana sehemu zote, lakini kwa barani afrika Tanzania ikiwemo nyanya hizi hujiotea zenyewe maporini. |
Nyanya zilikuwa hazizalishwi huko
Uingereza mpaka 1590, kulingana na Smith, na Miongoni kati ya wakulima wa
mwanzo alikuwa ni John Geral, daktari-Kinyozi.
Kitabu cha “Kitotou
Geralds’s Iteneal’, kilichochapishwa mapema 1597, kilizua mjadala wa
kwanza kuhusu nyanya huko uingereza, ambapo Gerald
alijua kuwa nyanya zinaliwa huko Hispania na Italia.
Lakini aliamini majani yake yana
sumu na tunda lake (nyanya) ni salama, Na hadi kufikia miaka ya 1200, watu
wengi walikuwa tayari wanakula sana nyanya.
Afrika ya Kati
Nyanya ziliingia huko katika kilimo
cha Mashariki ya kati kupitia John Barker, mnamo 1799-1825, na Mnamo karne ya
19, matumizi yake makubwa yalikuwa bado ni kama kiungo, na ndio iliyokuwa pekee
ikitumika katika maeneo yale.
Nyanya ziliingia Mashariki ya kati
kutumia njia mbili, Njia ya kwanza ni kupitia uturuki na Armenia na njia ya pili
ni kupitia familia ya Mfalme wa Qatar,
iliyokuwa mara kadhaa ikisafiri kuelekea ufaransa.
Na hivyo kuzidi kusambaa, kusambaa
na kutapakaa sehemu zote barani Afrika ikiwemo Tanzania, wa hivi leo hakuna
sehemu yoyote afrika hawazalishi mmea au tunda hili la nyanya.
KUMBUKA: Kwa Amerika Nzima
Utambuzi wa kwanza wa nyanya huko
Amerika uliripotiwa na William Salmon, mnamo 1710, aliyesoma nyanya zilikuwa
huko ambako leo kunajulikana zaidi kama South Carolina, na Inawezekana nyanya
hizo zikawa zililetwa kutoka Karibeani, na mpaka sasa watu kadhaa huko wanaona
au hudhani kuwa nyanya bado huwa zina sumu, na ni hatari kwa kuliwa, na
hutumika sana kama mmea wa bustani na mapambo tu.
UMAARUFU USIOUDHANIA WA MATUMIZI YA
NYANYA HIVI SASA DUNIANI:
Licha ya kuwa tunda hili, (ambalo
hutumika kama kiungo maalumu cha chakula) kutumiwa sana na watu mbalimbali
duniani, pamoja na kujizolea umaarufu wake kwa sifa hizo za mapishi.
Lakini, kwa baadhi ya nchi kama
vile ilivyo Hispania nyanya hizi zimejipatia umaarufu wa tofauti sana kwa kuwa
zimewekwa katika sherehe na mila za utamaduni za waHispania, ambapo hutumiwa
kama kikolezeo cha sherehe husika.
Sherehe hizo za kijadi hujulikana
kama “La tomatina” ambapo watu huadhimisha kwa kurushiana (kulengana) nyanya
pamoja na kujitandaza miilini mwao.
“La Tomatina” ni
sherehe ambazo huandaliwa kila mwaka hasa zaidi kwenye mji mdogo wa Uhispania uitwao
(Bunol) ambapo katika sherehe hizo huweza kuwakusanya kwa pamoja wakaazi karibu
elfu arobaini (40.000) ambao hurushiana nyanya zilizokwiva vyema.
No comments:
Post a Comment