Nguvu ya uwekezaji katika soka la kileo, huwa na matokeo
chanya haswaa Akihusishwa Mwanamke (kama tunavyokubaliana Palipo mafanikio ya
Mwanaume bhasi nyuma yake kuna mwanamke)
HAKUNA ubishi kuwa hapa nyumbani Tanzania, na duniani kote mchezo
maarufu zaidi ni soka, Ambapo soka ndiyo mchezo wenye mashabiki wengi zaidi
tena kwa kiwango kikubwa cha asilimia (88/100) nyingi.Hapa Tanzania, Wafanyabiashara watatu wakubwa ndiyo wameamua kuwekeza katika mchezo wa soka na mabadiliko yamekuwa yakionekana hata kama si sehemu zote.
Said Bakhresa, yeye ameamua kuanzisha timu yake ya Azam FC. Imekuwa na mafanikio makubwa kwa muda mfupi ingawa haijaweza kuwashawishi mashabiki sana kama ilivyo kwa wakongwe, Yanga na Simba.
Yusuf Manji, bilionea ambaye amekuwa hataki kuonekana au
kujitangaza sana kwa maana ya utajiri, yeye alikuwa tayari kuwekeza Yanga kwa
njia ya kukodisha lakini inaonekana kumekuwa na figisu, jambo linaloonekana
kuikwamisha Yanga na kuifanya iingie katika mwendo wa kusuasua.
Wakati Yanga bado hawajajua kipi ndiyo au hapana, Simba wapo
kwenye mchakato wa kukubali Sh bilioni 20, ofa kutoka kwa bilionea kijana zaidi
barani Afrika Mohammed Dewji ambaye utajiri wake unafikia dola bilioni 1.4
(zaidi ya Sh trilioni tatu).
Mo Dewji anataka kununua hisa za Simba kwa asilimia 51 ili
kuanza kuiendesha kwa nafasi na kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko.
Nadhani umeon nguvu ya uwekezaji?
Wakati mabilionea hao wa Tanzania wameingia katika soka,
upande wa Angola, mwanamama tajiri zaidi nchini humo na tajiri zaidi kuliko
wanawake wote barani Afrika, Isabela dos Santos, yeye amechaguliwa kuwa rais wa
klabu kongwe ya Petro Luanda, hali ambayo inaonyesha wazi sasa ameamua kuingia
kwenye mchezo huo wa soka.
Moja ya nyumba ya kifahari inayomilikiwa na Mwanamama Isabela. |
Utajiri wa Isabela ni dola bilioni 3.3 (zaidi ya Sh trilioni
7). Kumbuka mwanamama huyu mwenye watoto watatu ni mtoto wa Rais Jose Eduardo
dos Santos aliyewahi kuitawala nchi ya Angola.
Lakini ni mke wa Sindika Dokolo, bilionea kutoka DR Congo,
pia ni mtoto wa bilionea wa miaka nenda rudi wa nchini humo. Wawili hao
walikutana wakiwa shule barani Ulaya ambako walianzisha uhusiano wa kimapenzi.
Klabu ya Petro de Luanda ilianzishwa mwaka 1980 na kupata
mafanikio makubwa baadaye. Lakini miaka ya kuanzia 2000, ilianza kudorora na
sasa Isabela anakuwa kama mkombozi. Ushindi wake wa cheo cha rais, bila shaka
ni kama ukombozi kwa mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwa wanajua Isabela ni
mwanamama wa chuma ambaye hatakubali kuendesha kitu kinachodorora.
Isabela ni injinia kitaaluma. Lakini amekuwa mfanyabiashara
aliyejijenga katika mafuta, madini hasa almasi lakini barani Ulaya hasa Ureno
na Hispania amewekeza katika makampuni makubwa ya simu ambako anaingiza kiwango
kikubwa cha fedha.
Lakini hivi karibuni kajiingiza kwenye biashara ya saruji na
ameanza umiliki wa mabenki, hasa nchini Ureno.
Baadhi ya wananchi au wanasiasa wapinzani wamekuwa wakipinga
kwamba anapendelewa sana kwa kuwa ni binti wa kwanza wa rais dos Santos, akiwa
ni mtoto wa kwanza wa mkewe wa kwanza.
Mwanamama huyo ambaye pia ni Rais wa Shirika la Msalaba
Mwekundu nchini Angola, anasifika kwa kuwa na tabia ya kutaka ushindi au
mafanikio makubwa kwa kila anachokiongoza.
Kabla aliwahi kuwekeza nchini Marekani katika mpira wa magongo.
Lakini baada ya kushinda katika uchaguzi na kuwa Rais wa Petro de Luanda,
alisisitiza anataka kuona timu hiyo inakuwa kubwa zaidi barani Afrika.
Isabela anasema fedha ni suala linalotokana na ubunifu na
uwezo wa uamuzi hasa katika uchapaji kazi., lakini tatizo ni kuwa Wanawake
wenyewe hawakubaliani katika maswala ya kimaendeleo, lakini zaidi hawapendi
maendeleo ya wanawake wenyewe wao kwa wao, amkeni wanawake.
Amesisitiza Isabela, kama Waangola na hasa watu wa Klabu ya
Petro de Luanda wanaamua kwa kushirikiana naye bega kwa bega, basi hakuna
anayeweza kuizuia klabu hiyo kurudisha sifa yake na kuwa kubwa sana.
Baba wa Isabela na Rais mstaafu wa Angola, aliyelitawala taifa hilo kwa miaka takribani 38 kabla ya kustaafu. |
Kwa mashabiki wa Petro de Luanda ni faraja upya, lakini hofu
kubwa ni kwa mashabiki wa timu nyingine. Kwamba fedha za Isabela na kwa kuwa
ndiye binti kipenzi wa Rais wa Angola ambaye amekaa madarakani tokea mwishoni
mwa miaka ya 1980, mashabiki wengi huamini kuwa huenda upendeleo unaweza kuwa
wazi. Jambo ambalo ni mtizamo hasi.
Wengi wanaamini hata waamuzi, viongozi wa Shirikisho la Soka
la Angola, watakuwa waoga na kuipa nafasi Petro de Luanda kufanya vizuri hata
isipostahili.
Utaona, kuingia kwa bilionea huyo namba moja kwa upande wa
wanawake Angola na Afrika nzima, kumewagawanya wengi. Wapo walio na faraja kuu
na wengine hofu hasa ya haki Kutendeka, ndio imetawala.
Isabela kasisitiza kwamba mafanikio ndani ya Angola ni namba
moja lakini anachotaka yeye ni Petro de Luanda kuwa klabu kubwa zaidi Afrika na
angependa kuona inazipa shida kubwa timu kubwa kutoka Afrika Kaskazini,
Magharibi na ikiwezekana zile za Afrika Kusini huku akiitaja Mamelodi Sundowns
ambayo pia iliwahi kuwa na rais mwanamama.
Wanawake mnaweza, narudia tena Mnaweza, hii ni changamoto
kwenu kuchangamkia fursa hata katika michezo, nitafurahi zaidi mkuu wa TFF, awe
mwanamke, Kwenye klabu zote za soka Tz bara kuwe na uwekezaji wa mwanamke, ndio
nini kinashindikana! Mnaweza! Kama ilivyo kwa isabela.
Isabela anaishi kwenye nyumba ya kifahari ambayo inaaminika
ni ghali zaidi kuliko Ikulu ya Angola ambayo inaongozwa na baba yake mzazi.
Lakini si rahisi kuipiga picha kutokana na ulinzi mkali.
Anamiliki boti ya kisasa, ndege mbili kwa ajili yake na
magari zaidi ya 12 ya kifahari likiwemo aina ya Maybach Exelero lenye thamani
ya dola 250,000 (zaidi ya Sh milioni 544) ambalo wengi waliamini ni la kisela
na si kwa mtu kama yeye.
Kwa kuwa ana umri wa miaka 43, Isabela amekuwa haoni shida
‘kujiachia’ na msisitizo wake ni kwamba yeye ni mama kijana anayehitaji kuishi
anavyoamini kwake ni sahihi.
Lakini amekuwa akisisitiza pia kuwa, sasa furaha yake ni
soka na anaamini uwekezaji wake katika mchezo huo utakuwa sawa na ilivyo
kuwekeza katika madini au zaidi.
Hakuna aliyepinga kuingia kwake katika uwekezaji. Wengi
wanajua si mpenzi sana wa soka au haujui vizuri. Lakini wanaamini kwa kuwa ni
mfanyabiashara, atasaidia kupatikana kwa mabadiliko kwa kuwa anajua ili kufanya
biashara vizuri katika soka, basi lazima timu inayotaka kufanya vizuri ishinde
na kupata makombe.
Isabela anataka makombe yamsaidie kupata biashara. Hivyo
lazima atahakikisha Petro de Luanda inaamka na kuwa bora zaidi ya sasa na
kumsaidia kupata na kufanya biashara ya uhakika.
VIPI KWA SIMBA NA YANGA? ENDELEENI KUGAWA HIZO HISA ZENU BHANA
ILI KUKUZA SOKA LETU TANZANIA:
MAELEZO ZAIDI KUHUSU ISABELA NA MZOZO ULIOPO KATI YA BABA YAKE
(Dos santos - Rais aliyetawala Angola kwa miaka38) na Rais wa sasa wa Angola (João Lourenço) Bofya Hapa:Makala NA: Stewart Meena+Mtandao
No comments:
Post a Comment