Sumbawanga ni moja ya Wilaya zinazounda mkoa wa Rukwa, ikiingia moja kwa moja kwenye ziwa Rukwa mashariki na Ziwa Tanganyika upande wa magharibi. |
Sumbawanga ni neno lenye asili ya Kifipa likitamkwa ‘Sumbu wanga’ kwa lugha ya Kiswahili likiwa na maana ya (Tupa uchawi wako – throw away your witchcraft in english) na lilianzishwa na Mwana wa mtawala mmoja wa zamani wa eneo hilo aliyeitwa (Mwene Ngalu).
Sumbawanga ni Wilaya mojawapo inayounda mkoa wa Rukwa, ikiwa na wakazi takribani laki2 na 50 (250.000) na ipo ukanda wa eneo la magharibi mwa nchi ya Tanzania, na ikipakana na mikoa ya Mbeya na Shinyanga, na inaingia hadi ziwa Tanganyika.
Wilaya hii ina makabila mengi, lakini kabila la asili kabisa hapa (wenye wilaya yao) ni Wafipa, ambapo Sumbawanga ni mji ulioanzishwa rasmi mwaka 1803 chini ya chifu wa kwanza wa ufipa aliyeitwa (Chifu KAPUFI) ambaye alitawala miaka ya 1885 wakati wa ujio wa Wajerumani Tanganyika.
Chini
ya milki ya wajerumani alianza makazi yake eneo hili la Ufipa na makao yake
makuu yalikuwa kijiji cha KISUMBA nje kidogo ya mji wa sumbawanga (Lakini huyu
sio mwanzilishi halisi, alikuwa mtawala tu kwa jina lingine). Wakazi wa huko
bila shaka mtakifahamu kijiji hiki.
Mke
wa mwazilishi wa eneo hili aliitwa (Mwene Wakulosi) ambaye walijaaliwa kupata
watoto wa3, wakwanza wa kiume (Mwene Kiatu) na wawili waliofuatia walikuwa
mabinti (Mwene Ngalu Chisichaafipa na Mwene Mwati). CHISICHAAFIPA ni jina la
asili lenye maana ya ‘Utawala’.
Hakujaaliwa kupata watoto, na alipofariki utawala wake ulirithiwa na dada yake aliyemfuatia (Mwene Ngalu) ambaye ndiye mwanzilishi halisi wa mji wa Sumbawanga.
Cifu Mwene Ngalu alikuwa mtu mwenye upendo, na hakupenda mauza-uza ya aina yoyote ikiwemo uchawi, hivyo kabla ya kuingia kijiji cha sumbawanga alichokianzisha (kabla ya kuwa wilaya) aliwataka watu wote wanaomfuata na kumkubali yeye kama kiongozi wao WATUPE UCHAWI WAO WOTE WALIOKUWA NAO KWENYE MTO LWICHE kisha waingie katika kijiji cha Sumbawanga wakiwa watu safi kabisa.