Friday, 27 October 2017

ITAMBUE BETRI MPYA YA MAGARI INAYOHITAJI KUCHAJIWA KWA DAKIKA 6 TU.


IMAGE: By Internet


Kampuni ya Toshiba ya Japan imesanifu betri mpya ya magari yenye ukubwa wa mkono ambayo inahitaji kuchajiwa kwa dakika 6 tu tofauti na zile nyingine za Oxide zinazohitaji masaa8-10.

Tofauti na betri nyingine za Li-ion ambazo ncha hasi zilitengenezwa na grafati, betri mpya imetengenezwa na Niobium Titanium Oxide, ambayo inaleta nishati nyingine na inaweza kuchajiwa kwa muda mfupi sana.

Betri za kawaida za magari zikichajiwa kwa nusu saa umeme utafikia asilimia 80, lakini betri mpya ikichaji kwa dakika 6, umeme utafikia asilimia 90. Magari ya majaribio ya kampuni hiyo yalikwenda kilomita 320 baada ya kuchajiwa kwa dakika 6 tu.

Aidha, betri mpya ikichajiwa na kutumiwa kwa mara 5000, bado ina zaidi ya asilimia 90 ya ujazo wa betri mpya, na inaweza kuchajiwa katika mazingira baridi yenye joto la nyuzi 10 chini ya sifuri sentigredi.

Kampuni ya Toshiba itaendelea kuboresha betri hiyo, na kujaribu kuuza bidhaa rasmi ifikapo mwaka 2019.

HABARI KAMILI ENDELEA HAPA CHINI KWENYE LINK:

source:
https://www.greencarreports.com/news/1113332_toshiba-claims-6-minute-recharge-for-new-electric-car-battery-cell

MAREKANI: SELI ZA KINGA MWILI, SASA HUENDA ZIKABADILISHIKA KWA MAFANIKIO.!


 
Serikali ya Marekani imepitisha tiba ya kubadilisha seli za kinga ya maradhi ya mwili wa wagonjwa ili kutibu ugonjwa wa damu ambayo hii ni tiba ya jeni ya kwanza inayoidhinishwa na Marekani.

Wataalamu wanaona kuwa tiba hiyo imefungua ukurasa mpya wa tiba ya saratani.

Idara ya usimamizi wa chakula na dawa ya Marekani imetoa taarifa ikisema, tiba mpya ya kampuni ya Novartis ya Uswisi imeidhinishwa, ambayo itatumiwa kutibu wagonjwa wa damu chini ya miaka 25.

"Imeongeza kuwa hii ni hatua ya kihistoria itakayofungua ukurasa wa kutibu saratani na maradhi mengine makali ya kuharibu maisha"

Tiba hiyo mpya ni tiba ya CAR-T inayoendelezwa katika miaka ya hivi karibuni. Tiba hiyo inakusanya seli za T zinazotoa mchango mkubwa katika mchakato wa kinga maradhi, halafu kuzihariri, ili kuzifanya seli hizo za T kuweza kutambua na kushambulia seli za saratani.

Jaribio hilo lililowashirikisha wagonjwa 63 limeonesha kuwa baada ya kupatiwa tiba hiyo kwa miezi 3, hali ya ugonjwa ya asilimia 83 ya wagonjwa imepona kwa kiasi.

Baada ya kupatiwa tiba kwa mwaka mmoja, kiwango cha kutokea tena kwa ugonjwa huo ni asilimia 64 huku kiwango cha kuishi kikiwa asilimia 79.

Mkurugenzi wa idara hiyo amesema, kuhariri seli za wagonjwa na kuzitumia kuua saratani, kunamaanisha tumeingia katika kipindi kipya cha ubunifu wa matibabu.
 
HABARI NA REDIO CHINA.

JE! WAJUA MUZIKI ULIOCHANGAMKA WABAINIKA KUINUA UWEZO WA KUBUNI?


Kujitambua ndio njia sahihi ya kuelimika na kufuta maadui watatu: Umaskini, Ujinga na Maradhi, ambapo ujinga huo ufutwa kwa kujiwekea taratibu za kusoma vitabu, kufuatilia wengine wanafanya nini na kuamua wewe ufanye nini.


NA:
      Stewart Meena:

Je! Unasikiliza miondoko yote!, au ipo mirindimo ambayo huipendelea zaidi kuisikiliza..? kama vile Bongo-flavour, HipHop, Mduara, Charanga, Blues, Pop, Zouk, Soukus, Country, Ragga/ Reagae/ Danshal , Ngoma za Asili, Folks nk….

Katika mazingira ya kiAfrika, muziki (haswaa wa kitamaduni) ulitumika kuwafundisha vijana mila na desturi zao, namna ya kuwa hodari katika familia zao, pamoja na kuwa wazoefu wa jambo flani lililokusudiwa kufundishwa kwa vijana hao.
 
 
Muziki huo ulipigwa kwa kutumia vyombo vya asili kama ngoma, makopo yaliyowekwa mchanga, huku kukiwa na mshehereshaji au muimbaji anayeongoza uimbaji kisha wengine huitikia kwa kumfuatisha muimbaji pamoja na mirindimo ya ngoma husika.
 
Wengine wakipanga miduara huku wakicheza, na miilini mwao wakijitanda mavazi ya mapambo ya sili, yote hiyo ni kwanini kufikisha ujumbe Fulani kwa jamii, kuwafurahisha na kuwatuliza nafsi zao zinazotokana na mawazo mengi, uchovu wa siku pamoja na kukuza mshikamano.
 
Kuna baadhi ya tamaduni, ngoma hizi zikipigwa basi tambua lazima mtu ataozeshwa mke, au kupata mume, yote hayo ni matokeo yaletwayo na kamshange hizo..... Je! kwanini ngoma hizo zilikuwepo, ziliibuka wapi! au ni kwanini watu tokea Enzi waliona ndio njia sahihi ya kujiburudisha na kutuliza nafsi zao!?
 
 
 
Ila katika mila hizo hizo yapo baadhi ya makabila na tamaduni zao, huwa na utaratibu wa kuimba nyimbo za kiasili ingawa hawakutumia vyombo vya muziki vyovyote lakini walitoa ala flani za muziki uliochanganyika na mirindimo ya mikolezeo kwa kutumia midomo yao.


Mfano mzuri ni kabila la Wamaasai ambao hawa huwa na taratibu za uimbaji kwa wanaume 9Morani) kuruka juu huku wakiimba na Wanawake (Mama yeyoo) wakiitikia kwa utaratibu uliopangilika kuendanda na taratibu zao, na hiyo imekuwa ikifanyika kipindi cha Jando na Unyago.

Hivyo kwa tamaduni zetu, muziki sio jambo genii la ilitegemea na ni wakati gani muziki huo au ngoma hizo zitachezwa. (Kiafrika tangu zamani ngoma zilikuwa zikipigwa jioni baada ya kazi, na mara nyingi wakati wa wikendi, mfano ngoma ya Baikoko tanga, chakacha-Kilimanjaro, nk)
 

 
Ingawa kwa Wazazi wamekuwa wakitoa malalamiko yao kwa watoto wao kuwa, kupenda kwao kutizama na kusikiliza muziki mbalimbali zaidi kunapelekea kushuka kwao kimasomo na kitaaluma pia.

Hiyo imekwenda mbali sana hadi wanafunzi hawaruhusiwi kwenda na simu yoyote mashuleni na wakibainika hupokwa simu zao na kupewa notes ya kuwaita wazazi wao, lakini kwa nchi za wenzetu wanafunzi huruhusiwa kwenda na simu zao, computer zao mashuleni, (ivyo kikubwa hapa sio simu wala muziki bali ni matumizi yapi sahihi ya simu hizo na Laptop zao)
 

 
KWELI MUZIKI UNAWEZA KUINUA UWEZO WA VIJANA KUBUNI MAMBO MBALIMBALI
 
Mashuleni: Vijana wengi wa kileo (walioko mashuleni vyuoni nk) muziki sio jambo geni kwani kwa sasa maendeleo ya sayansi na teknolojia umerahisisha Vijana hao ku-download na kuhifadhi miziki mingi tofauti kwenye simu zao (Smartphone) ambazo kwasasa zimeboreshwa na kuwekewa chip yenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi nyimbo hizo.
 
Ambapo ukikutana na wanafuzi hao utawaona wakiwa na Wingi wa masomo, muda hafifu wa mapumziko nao pia unaelezwa kuleta matokeo tofauti ya ubunifu kwa vijana wengi wa kiTanzania, ikiwemo kufanya vyema katika masomo yao au shughuli zao za kila siku.
 
Kwa mfano: Utafiti uliofanyika nchini Australia umeonesha kuwa, kusikiliza muziki uliochangamka sio tu kunaweza kuboresha hisia ya moyo wa muhusika, bali pia kunaweza kuinua uwezo wake wa kubuni mambo mbalimbali.
 
 
Watafiti hao kutoka chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha (Sydney) wametoa ripoti hii ikisema, “katika utafiti wetu mpya tumechagua miziki minne, ambayo inaweza kuleta hisia ya utulivu, furaha, huzuni na wasiwasi”.

Ambapo katika majaribio ya kung’amua hilo, Watafiti hao waliwagawanya washiriki 155 kwenye vikundi vitano, na kuwataka kumalizia kazi zinazohitaji ubunifu, kama vile kufikiria matumizi tofauti ya ubunifu, ikiwemo ya kupanga vitofali vilivyovurugwa.

Vikundi vinne vilipewa kazi hiyo ya ubunifu kwa kusikilizishwa muziki wa aina nne tofauti (miondoko) ambao unaoleta hisia tofauti pia, huku kundi la tano waliifanya kazi hiyo pasipo kusikiliza muziki wa aina yoyote (yaani mazingira tulivu).

Baada ya zoezi hilo, Matokeo yameonesha kuwa, kusikiliza muziki uliochangamka kunaweza kuinua wazo la ubunifu kwani wote waliofanya ubuni huo waliibuka na aina tofauti pamoja na ufanisi tofauti wa kuifanya kazi hiyo.
 

Watafiti wamesema, kuinua uwezo wa uvumbuzi ni jambo muhimu la kuhimiza maendeleo ya sayansi na teknolojia, na ni muhimu sana kuelewa athari zinazotokana na muziki kwenye maswala ya ubunifu, na hivyo jukumu lako kama mlezi, mzazi au mwangalizi wa muhusika unatakiwa utumie njia sahihi ya kuinua na kukuza ubunifu kwa walengwa.

Kwani Mazingira tofauti pia yanaweza kuathiri ubunifu huo wa wahusika, (mfano nyumbani wanakotokea, majukumu yanayowangojea, pamoja na wana himizwa vipi) kadhalika miondoko ya muziki pia ni moja ya njia zinazoweza kubadilisha mazingira hayo.

Kwamfano wapo baadhi ya watu wanapotizama filamu zenye mchanganyiko wa huzuni hujikuta nao machozi yakiwatoka pasipo kujizuia, au kulia, au matukio ya ajali huwafanya watazamaji kuhisi ni mojawapo ya eneo husika la ajali nk.

Swali kubwa ni kuwa je! Wewe huwa unapenda kusikiliza miondoko ya aina gani..? mzazi unamzuia vipi mwanao kuacha kusikiliza miziki isiyo na tija kwa taaluma yake? Muda gani unamuhimiza kujisomea vitabu mbalimbali ya kukuza ufahamu, kupumzika, na kufanya shughuli nyingine za nyumbani za kila siku.

 

NINI KIFANYIKE?

Kubwa zaidi wewe kama mzazi, unapaswa kuchagua aina za muziki ambazo utawapa watoto wako waisikilize wakati umewapa majaribio yanayohitaji ubunifu.

Kupanga ratiba za kujisomea vitabu na notes mbalimbali, na ukiwasimamia kuhakikisha hilo linatekelezeka, pamoja na kuzuia watoto wako kutumia muda wao mwingi kutizama filamu au televisheni.

(Katika nchi zilizoendelea huwezi kukuta watu wakitumia muda wao wa mapumziko zaidi ya masaa mawili kutizama filamu kwa siku)

Kija kujitambua nini unataka, ufanye nini kufikia malengo yako ya kitaaluma, kupumzika kwa wakati na kuwa na ratiba nzuri za kubadilishana mawazo na watu waliokuzidi taaluma nk.

Je! Aina gani za filamu zinazowafaa?, tafuta filamu nzuri zenye mafundisho kwa watoto wako ukilinganisha na jinsia, umri au rika lao (sio filamu za wavulana unawapa wasichana!)

Hata hivyo, kulingana na utafiti huo wa Chuo cha Sydney, bado Watafiti hao wanasema, wataendelea kutafiti athari za mitindo tofauti kwenye ubongo na kutoa matokeo zaidi kwa siku za usoni.

NINI MAONI YAKO, WAFIKISHIE WENGINE ELIMU HII KUIJENGA NCHI YAKO KWA VIJANA CHIPUKIZI (New generations)

Waweza show love HAPA PIA HISTORIA, Link: https://www.facebook.com/stewart.meena

Monday, 23 October 2017

TUPA UCHAWI: NENO LA KIFIPA LENYE MAANA YA SUMBAWANGA, HISTORIA

Sumbawanga ni moja ya Wilaya zinazounda mkoa wa Rukwa, ikiingia moja kwa moja kwenye ziwa Rukwa mashariki na Ziwa Tanganyika upande wa magharibi.

Sumbawanga ni neno lenye asili ya Kifipa likitamkwa ‘Sumbu wanga’ kwa lugha ya Kiswahili likiwa na maana ya (Tupa uchawi wako – throw away your witchcraft in english) na lilianzishwa na Mwana wa mtawala mmoja wa zamani wa eneo hilo aliyeitwa (Mwene Ngalu).

Sumbawanga ni Wilaya mojawapo inayounda mkoa wa Rukwa, ikiwa na wakazi takribani laki2 na 50 (250.000) na ipo ukanda wa eneo la magharibi mwa nchi ya Tanzania, na ikipakana na mikoa ya Mbeya na Shinyanga, na inaingia hadi ziwa Tanganyika.

Wilaya hii ina makabila mengi, lakini kabila la asili kabisa hapa (wenye wilaya yao) ni Wafipa, ambapo Sumbawanga ni mji ulioanzishwa rasmi mwaka 1803 chini ya chifu wa kwanza wa ufipa aliyeitwa (Chifu KAPUFI) ambaye alitawala miaka ya 1885 wakati wa ujio wa Wajerumani Tanganyika.




Chini ya milki ya wajerumani alianza makazi yake eneo hili la Ufipa na makao yake makuu yalikuwa kijiji cha KISUMBA nje kidogo ya mji wa sumbawanga (Lakini huyu sio mwanzilishi halisi, alikuwa mtawala tu kwa jina lingine). Wakazi wa huko bila shaka mtakifahamu kijiji hiki.

Mke wa mwazilishi wa eneo hili aliitwa (Mwene Wakulosi) ambaye walijaaliwa kupata watoto wa3, wakwanza wa kiume (Mwene Kiatu) na wawili waliofuatia walikuwa mabinti (Mwene Ngalu Chisichaafipa na Mwene Mwati). CHISICHAAFIPA ni jina la asili lenye maana ya ‘Utawala’.
 
Baada ya kifo cha mwanzilishi (Chifu kapufi) utawala wake uliendelezwa na mwanae wa kiume (Chifu kiatu) ambaye naye alihamia kijiji cha LWICHE, ambayo hiyo ilitokana na taratibu za jamii ya wafipa ‘kiutawala’ ukitawazwa kuwa kiongozi lazima uhame na kwenda kuanzisha kijiji chako, na huyu aliitawala ufipa yote.

Hakujaaliwa kupata watoto, na alipofariki utawala wake ulirithiwa na dada yake aliyemfuatia (Mwene Ngalu) ambaye ndiye mwanzilishi halisi wa mji wa Sumbawanga.

Cifu Mwene Ngalu alikuwa mtu mwenye upendo, na hakupenda mauza-uza ya aina yoyote ikiwemo uchawi, hivyo kabla ya kuingia kijiji cha sumbawanga alichokianzisha (kabla ya kuwa wilaya) aliwataka watu wote wanaomfuata na kumkubali yeye kama kiongozi wao WATUPE UCHAWI WAO WOTE WALIOKUWA NAO KWENYE MTO LWICHE kisha waingie katika kijiji cha Sumbawanga wakiwa watu safi kabisa.

Na aliyekiuka Amri hiyo, na kutaka kuvuka mto Lwiche kuingia katika kijiji cha Sumbawanga akiwa na Uchawi basi hakumaliza safari yake salama Alifariki katika eneo hilohilo. UCHAWI ULIOJE HUU.!?

Mkoa wa Rukwa na eneo lake la utawala katika Ramani ya Tanzania. Sumbawanga Ndilo eneo mashuhuri Zaidi kwa mkoa huu kutokana na uwepo wa Wamisionari wa Kijerumani waliojulikana kama (White Fathers) ambao waliishi eneo hilo kwa karne nyingi wakifundisha Ukristo (dini ya Roma Katoliki)
 

Huo ndio ukawa mwanzo wa sumbawanga mpya ya watu safi, na hakukuwa na matatizo kama ya awali yaliyokuwepo wakati wa utawala wa baba yake (Mwene Ngalu) na utawala wa kaka yake (Mwene Kiatu)
 
Mwanamama huyu, kwa sababu hiyo alipendwa na watu wake na kulipojitokeza matatizo ya aina yeyote chifu huyo alikwenda milimani kuomba na majibu yalipatikana haraka (ikiwemo mvua kunyesha nk) hasa kwa imani ya usafi waliyokuwa nayo. SWALI NI KUWA JE! Uchawi ulitumika; mizimu au Nguvu ya Mwenyezi Mungu.!?
 
Chifu Mwene Ngalu alijaaliwa watoto-7, chini ya himaya yake mpya iliyojengwa Sumbawanga kati ya mwaka 1918-1920, na ikisimamiwa na walowezi au Mabruda wa dhehebu la ROMA  (yaani Wakatoliki) ambao walikuwa wajerumani.
 
 
 
MAAJABU: Milki yake hiyo ilibomoka, lakini yamebakia magofu (pakihifadhiwa kama Makumbusho ya eneo hilo na umuhimu wake) ambapo kwa nje kuna sehemu ya makaburi ambapo mpaka wa hivi LEO panatumiwa na Watu wa ukoo wake kwaajili ya kufanya Maziko.
 
Na jambo la kushangaza ukitembelea eneo hilo, ni wingi wa nyuki waliojenga kwenye pango na wasiohama na wamekuwepo hapo kwa muda mrefu (miaka na miaka) ambapo inaaminika ni tangu enzi za utawala wa kizazi cha Chifu Mwene Ngalu.
 
TEMBEA ILI KUJIFUNZA: mimi nimejifunza hayo, Pia ukienda maktaba ya Sumbawanga au Ya mkoa wa Rukwa omba kusoma kitabu cha zamani kilichoandikwa na PADRE SIMCHILE kiitwacho White Father’s na Ufipa.
 
 
SOURCE: Wikipedia.org; Wakongwe wa Sumbawanga' Sumbawanga Museums and White Fathers na Ufipa (book).

For Others Opinion and Amazing history Up-Dates visit also Here: https://www.facebook.com/stewart.meena/