Serikali ya Marekani imepitisha tiba ya kubadilisha seli za
kinga ya maradhi ya mwili wa wagonjwa ili kutibu ugonjwa wa damu ambayo hii ni
tiba ya jeni ya kwanza inayoidhinishwa na Marekani.
Wataalamu wanaona kuwa tiba hiyo imefungua ukurasa mpya wa tiba
ya saratani.
Idara ya usimamizi wa chakula na dawa ya Marekani imetoa taarifa
ikisema, tiba mpya ya kampuni ya Novartis ya Uswisi imeidhinishwa, ambayo
itatumiwa kutibu wagonjwa wa damu chini ya miaka 25.
"Imeongeza kuwa hii ni hatua ya kihistoria itakayofungua ukurasa
wa kutibu saratani na maradhi mengine makali ya kuharibu maisha"
Tiba hiyo mpya ni tiba ya CAR-T inayoendelezwa katika miaka ya
hivi karibuni. Tiba hiyo inakusanya seli za T zinazotoa mchango mkubwa katika
mchakato wa kinga maradhi, halafu kuzihariri, ili kuzifanya seli hizo za T
kuweza kutambua na kushambulia seli za saratani.
Jaribio hilo lililowashirikisha wagonjwa 63 limeonesha kuwa
baada ya kupatiwa tiba hiyo kwa miezi 3, hali ya ugonjwa ya asilimia 83 ya
wagonjwa imepona kwa kiasi.
Baada ya kupatiwa tiba kwa mwaka mmoja, kiwango cha kutokea tena
kwa ugonjwa huo ni asilimia 64 huku kiwango cha kuishi kikiwa asilimia 79.
Mkurugenzi wa idara hiyo amesema, kuhariri seli za wagonjwa na
kuzitumia kuua saratani, kunamaanisha tumeingia katika kipindi kipya cha
ubunifu wa matibabu.
HABARI NA REDIO CHINA.
No comments:
Post a Comment