Sunday, 29 January 2017

KUMWEPUSHA MTOTO NA UDUMAVU INAWEZEKANA:



  Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zinazokabiliwana changamoto ya kuwa na watoto wenye udumavu, ugonjwa ambao unachangiwa kwa kiwango kikubwa na lishe duni wanazozipata watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Mashirika mbalimbali ya ndani ya nchi na nje ya nchi yamekuwa yakihangaika kuhakikisha kuwa changamoto hii inapungua kama si kutoweka kabisa hapa nchini.
   Kwa nyakati tofauti, jitihada zimekuwa zikichukuliwa katika kuhakikisha kuwa afya inaimarishwa kwa kila mtu, ambapo zimekuwa zikiungwa mkono na taasisi mbalimbali za dini.
 Lakini bado hali ni tete kwa watoto ambao ndio wanaokumbana na tatizo hili la udumavu na ukondefu unaosababishwa na kukosa lishe bora.

   Takwimu za shirika la afya duniani (WHO) zinaonyesha kuwa kila siku zaidi ya watoto 270 waliochini ya umri wa miaka 5 nchini Tanzania hupoteza maisha yao kwa lishe duni, huku zaidi ya watoto milioni 2 na Laki 7 wakikabiliwa na aina ya udumavu unaotokana na utapiamlo.
    Takwimu hizo zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vifo hivyo hutokea katika mwezi wa kwanza wa maisha ya watoto hao.
    Huku takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani UNICEF, zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto wote wa Tanzania waliochini ya umri wa miaka mitano wamedumaa kutokana na kukosa lishe bora.
    Chanzo cha ugonjwa huu wa udumavu kinaelezwa kuwa ni utapiamlo unaosabibishwa na lishe duni kwa mtoto ambapo huchangia mtoto kuwa na kimo au urefu mfupi usioendana na umri wake.
   Japo kumekuwapo na dalili za kupungua kwa kiwango cha udumavu nchini kwa asilimia 30, kati ya mwaka 1994 hadi 2014 japo idadi ya watoto waliodumaa ikiwa imeongezeka kutoka milioni 2.4 hadi 2.7 katika kipindi hicho.
    Sababu nyingine ya udumavu ni kutokana na kuugua mara kwa mara katika miaka mitatu ya mwanzo ya makuzi yake.
   sababu nyingine ni Afya na Lishe duni kwa wanawake kabla ya Ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua, pia kutokupangilia uzazi, yaani kuzaa watoto kwa karibu karibu pamoja na tatizo la wasichana kubeba mimba wakiwa katika umri mdogo.
   Taratibu duni za ulishaji Watoto, ikiwamo kutonyonyeshwa maziwa ya mama pekee katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo baada ya kuzaliwa na kupewa chakula cha nyongeza kisichokidhi mahitaji yao ya lishe pale wanapotimiza umri wa miezi sita.
   Watoto kupewa kiasi kidogo cha chakula au kisichokuwa na ubora au mchanganyiko wa Makundi mbalimbali ya chakula pia ni sababu nyingine zinazodumaza watoto.

ATHARI:

   Mtoto kuwa na Udumavu, huchangia kupata athari zisizoweza kurekebishika katika maisha yake hata kama kwa hapo baadaye atapewa lishe bora, mwili wake tayari utakuwa umedumaa na hivyo kushindwa kupokea Marekebisho.
   Kushuka kwa maendeleo ya akili kwa mtoto pia ni moja ya Athari za udumavu, hatua hii humfanya mtoto kushindwa kufanya vizuri hata kwenye masomo yake.
   kuwa na uzito mkubwa kuliko umbo na umri wake "KIRIBA TUMBO" na kukumbwa na magonjwa yasiyoambukiza kama moyo, Kiharusi, Shinikizo la damu na hata Kisukari katika umri mdogo.

NAMNA YA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU.

   Ni wazi kuwa mpango wa (WHO) kwa Tanzania ifikapo mwaka 2025 walau idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliodumaa iwe imepungua kwa walau asilimia 40.
   Hata hivyo malengo haya yatafanikiwa tu iwapo Watanzania watazingatia lishe bora kwa watoto na Mama wajawazito kulinda afya zao katika kipindi chote cha ujauzito na kuzingatia unyonyeshaji pindi anapojifungua.
   Ni muhimu kwa Akina mama kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama hadi watakapofikisha umri wa "MIAKA 2" Hapa wanawake wajitahidi kutowaachisha watoto wao nyonyo mapema.

"Mama anashauriwa kumnyonyesha mwanaye ziwa lake kwa kipindi cha miaka miwili"



 VISIT ALSO: http://www.facebook.com/stewart.meena
                    FOR AMAZING UPDATES...............
 

No comments:

Post a Comment