Monday, 14 December 2015

HALI YA MAMBO BADO SI SHWARI NCHINI SOMALIA

Watu 10 wauawa kwenye mapigano Somalia
Baadhi ya Waliojeruhiwa katika tukio hilo huko somalia, na hali halisi ilivyokuwa.http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/53624
Habari kutoka Somalia zinasema kuwa, takriban watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye mapigano yaliyotokea katika mji wa Beledweyne nchini Somalia

Habari zaidi zinasema kuwa, mapigano makali yameibuka kati ya makundi mawili ya kikabila ambayo yametumia silaha nzito na kusababisha uharibifu mkubwa. Mashuhuda wamesema watu wasiopungua 25 wamejeruhiwa ambapo wengi wao ni raia wa kawaida

Duru za hospitali zinasema huenda idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na baadhi ya majeruhi kuwa katika hali mahututi.

Ugas Adirahman Ugas Khalif, kiongozi wa kikabila katika eneo hilo amelaani mauaji hayo ya raia wasio na hatia na kuzitaka koo zinazozozana kutatua hitilafu zao kwa njia za amani.

Baadhi ya duru zinasema juhudi za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika za kuzitenganisha pande hasimu hazikufua dafu na kwamba mwanajeshi mmoja wa Djibouti kutoka kikosi hicho ameuawa wakati wa makabiliano hayo

SOURCE: radio Iran Swahili

No comments:

Post a Comment