Stewart Meena'
Mji wa Yerusalemu (Jerusalem) umegawanywa katika pande mbili, Jerusalem Mashariki na ile ya Jerusalem Magharibi, ambapo Jerusalem ya Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu (tokea ilipotangaza hilo 1980 kama mji wake mkuu wa milele), huku Jerusalem Mashariki hutazamwa na Palestina kama mji wao mkuu wa taifa lao.
Eneo lote la Jerusalem, kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na Israel tangu vita vya mwaka 1967 taifa hilo lilipojitangaza kuwa dola huru chini ya umoja wa mataifa, ambapo Tangu wakati wa vita hivyo, Israel imejengwa nyumba za walowezi wa Kiyahudi takriban 200,000 ambao huishi Jerusalem Mashariki, hatua iliyoshutumiwa na jamii ya kimataifa kama ukiukwaji wa haki ya umiliki wa mji huo.
Ingawa inakadiriwa eneo hilo huishi Wapalestina takriban 370,000, na kutambuliwa kama eneo halali la waPalestina na Mataifa mengi ya nchi za Kiarabu na zile zenye waislamu wengi duniani.
Je! ni kwa nini mji huu huzozaniwa kwa kiasi hicho na mataifa haya mawili?
Sababu kubwa ni kuwa maeneo haya, hupewa umuhimu wa pekee na imani au "Dini kubwa tatu duniani" (Ukristo, Uislamu na Uyahudi) Ambapo imani zote hizi tatu humuangazia 'Abraham/Ibrahim' kihistoria ambaye anatajwa kwenye Biblia na Koran kama mmoja wa waanzilishi au mababu wa imani ulimwenguni kote. Mfano: 'Biblia humuita kama baba wa imani'
Kwa Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim na kwa Kiarabu al-Quds. Kwa Kiswahili, jina lake halisi ni Yerusalemu, ikiwa ni miongoni mwa mji wa kale zaidi ambao upo hadi sasa duniani.
Kihistoria mji huu uliwahi kutekwa, ukabomolewa na kuharibiwa vibaya sana, kabla ya kuja kujengwa upya tena, kwa kuyarudisha na kuhifadhi yale maeneo muhimu yaliyokuwepo tokea enzi maeneo hayo.
Eneo hili, ukichimbua sehemu ya ardhi yake kwenda chini, hufichua enzi fulani katika historia yake kuonyesha eneo ilo palikuwa na mji uliopotea (Lost city), hivyo ingawa kumekuwa na ubishani au mzozano kati ya dini mbalimbali kuhusu umiliki wa eneo hilo, lakini dini zote huungana kwa pamoja kuungama na kusali katika eneo hilo kwa vipindi na misimu, kwa kuutaja ni mji takatifu.
Ndani yake kuna Mji Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale, ikigawanyika katika pande au maeneo manne makuu, likitofautishwa na upekee wa aina ya majengo yake kuwa na muundo wa tofauti kulingana na tamaduni za wenyeji wa mitaa husika.
Moja ya maeneo hayo manne: Kuna eneo la Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Waarmenia, na kila eneo likiwa limezungukwa au kutenganishwa na ukuta mkubwa wa mawe. kama ilivyo kwenye ukuta wa maombolezo (Wailing wall & west bank)
Wakristo wana maeneo mawili, yale madogo ya wakristo wa Kiarmenia, na ya wakristo wengineo, kukiwa kumehifadhiwa kwa vituo vya vya kale zaidi vya wakristo hao hususani utamaduni wa Waarmenia duniani, uliohifadhiwa ndani ya Kanisa la St. James na nyumba kubwa ya utawala.
Nje ya Lango la Damascus, kuna Kanisa kuu Ndani ya mtaa huo wa Wakristo, likiwa na ukumbusho wa mahifadhio ya pango au 'Kaburi lenye historia kuhusu kifo na Ufufuo wa Yesu Kristo kama masihi na muokozi wa wakristo kote duniani. Ni eneo hilo inaelezwa 'Yesu alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary na hapo ndipo alipofufuka.
Kanisa takatifu hilo husimamiwa kwa pamoja na kwa ushirika wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo wakihudumu hapo, wale wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia. Pia kuna Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.
Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la Yesu na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.
Al Qudus: Mtaa wa Waislamu huu ndio mkubwa zaidi kati ya maeneo hayo manne na ndani yake kunapatikana madhabahu ya Dome of Rock (Kuba ya Mwamba) na Msikiti wa al-Aqsa kwenye eneo linalofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif, au Mahali/Hekalu Patakatifu.
Msikiti huo ndio eneo la tatu kwa utakatifu katika dini ya Kiislamu na husimamiwa na wakfu wa Kiislamu ambao hufahamika kwa Kiarabu kama Waqf, ambapo Waislamu hao huamini kwamba Mtume wao 'Muhammad' alisafiri kutoka hapo hadi Mecca usiku na aliomba pamoja na roho za manabii wengine wote katika viunga vya eneo hilo.
Hatua chache kutoka hapo kunapatikana Dome of the Rock (Kuba ya Mwamba) ambapo kuna jiwe jeusi la msingi, huko Waislamu huamini kwamba ni kutoka hapo ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni. Hadi hivi wa leo Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila wakati katika mwaka ku hiji, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mamia ya malelfu ya Waislamu hufika kuomba kwenye msikiti huo.
Katika mtaa wa Wayahudi, kunapatikana Kotel, au Ukuta wa Magharibi ambao ni masalio ya ukuta wa nje uliozunguka eneo lote lililokuwa Hekalu Takatifu, ambapo hapo ndipo eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi.
Wayahudi huamini kwamba hapo ndipo kulikuwa na jiwe la msingi ambapo kutoka kwake dunia iliumbwa; Kadhalika, wanaamini ni hapo ambapo Abraham alikuwa amejiandaa kumtoa kafara mwanawe Isaac.
Wayahudi wengi huamini kwamba Dome of the Rock ndipo lilipokuwa eneo takatifu zaidi ndani ya hekalu lililofahamika kama Patakatifu pa Patakatifu.
Ukuta wa Magharibi ndilo eneo la karibu zaidi ambalo Wayahudi wanaweza kufanya maombi yao, wakisimamiwa na Rabbi wa Ukuta wa Magharibi na kila mwaka hutembelewa na mamilioni ya mahujaji wa kiyahudi kutoka kila pembe ya dunia.
Hivyo: Kwa mujibu wa imani zote hizo tulizojadili na kuuchukulia kwao kwa upekee sehemu na baadhi ya mitaa ya eneo hilo, ndio maana kumekua na kuongezeka kwa mzozano wa kiimani na kiitikadi kila mmoja kutaka kudai na kutambuliwa kuwa eneo hilo ni lake, huku wengine wakifika mbali kutaka kufuta kabisa kumbukumbu na historia za imani nyingine ili kusiwepo na muingiliano huo.
Ni maeneo haya hususani nyakati za siku kuu za kidini, umati wa wageni hufurika maeneo haya kwa lengo la kutimiza moja ya nguzo zao kiimani, kama njia ya kuenzi na kuwa karibu zaidi na Mungu muweza aliyeziumba mbingu na dunia.
CHANZO:
BBC Swahili, & Blogsite washirika


No comments:
Post a Comment