Sunday, 30 August 2026
MJI MTAKATIFU WA JERUSALEM, MWINGILIANO, CHANZO IMANI ZA DINI TOFAUTI
Thursday, 27 August 2026
MWANAMKE: KWANINI TALAKA HAIPASWI KUWA SULUHISHO LA MGOGORO JUU YA USALITI!
FIKIRIA: Mwanamke, unamuacha mumeo (Mwanaume wako) kwasababu ya usaliti, alioufanya kuwa na mwanamke mwingine, (Aah!)
Mna familia pamoja, mtoto mmoja" au
wawili. (Ok!)
Hivyo, ukaomba talaka na mkatalikiana kwa sababu
umeumizwa sana na usaliti wake na huwezi kuuvumilia! Na baada ya mchakato wa
talaka kukamilika, ukaondoka na watoto wako! (Ooh!)
Ukaanza kufanya kazi kwa bidii ili ujipatie
mahitaji yako na uwalelee watoto wako mweyewe bila kuonyesha kuhitaji msaada wa
baba yao na kuzimudu gharama za maisha mwenyewe. (Good)
Ili kuendana na kuongezeka gharama za maisha,
unaangukia kwa mwanaume mwengine ‘Labda tajiri) Hujali chochote maana unahitaji
kulipa ada za watoto kama mwanamke unayejiamini na unajitegemea unahitaji
kuuthibitishia ulimwengu unajiweza mwenyewe kwa yote ndio maana ukakubali kuwa
na mwanaume huyo tajiri katika penzi la siri ingawa unafahamu ni mume wa mtu.
(Unajikuta umerudia kosa lilelile lililofanya nyie kutengana kwa talaka)
Hatimaye sasa na wewe umekua mchepuko kwa mume
wa mtu, tena mwenye familia yake na watoto pia (side chick to cheating
situation)
Ndipo unakumbuka na unaanza kufikiria kuhusu
mwanamke wa pembeni aliyekua naye mumeo, na kwa nini alikua naye! “Umechelewa’
Nda yako haipo tena!
Ulichofanya, ndicho alichokifanya mwanamke
uliyemfuma na mume wako, hukufikiria kuhusu maadili, na unaanza kumuelewa
taratibu: Pengine alikuwa na mume wako kwasababu ya ugumu wa maisha, wingi wa
majukumu, watoto aliotelekezewa wa kuwalea! Na zaidi tumbo linalohitaji chakula
kila siku.
NA SASA: Kama yule tu, unatamani hata kumpigia
mwanaume wa sasa uliye naye, lakini huwezi sababu unatambua yupo na mke wake na
familia yake nyumbani, na wewe unalinda nafasi yako kwake maana mkewe akigundua
hawezi kukimbilia kuachana zaidi wewe ndio utaachika. “Mateso yanarudia tena
upya”
Hivyo amekupa masharti yake ambayo utake
usitake lazima uyafuate, na unapaswa kuheshimu faragha yao kuwa sasa yupo
nyumbani na familia yake na wewe utaendelea kuwa option-tu, Linapokuja swala la
Kupunguza mawazo na tamaa zake.
Unafikiria tu kuhusu maumivu yako!
Unafikiria tu kuhusu faraja (Consolation) yako!
Ila walau awali ulikuwa na mume wako pekee
yako’ Ndio alikusaliti lakini bado aliendelea kuwa wako!
Hatimaye unajaribu kutafuta tena kufahamu juu
ya yanayoendelea kwenye maisha yake baada ya kutalikiana na kila mmoja kushika
maisha yake, unang’amua sasa ame ‘move-on’, na tayari anaishi na mwanamke
mwingine pengine mdogo kiumri au mrembo kukuliko wewe.
Unakaza roho, kwakua mawasiliano yake bado
unayo unaamua kupigia na kumuomba miadi ya kukutana sehemu kuongea kwa kigezo
cha watoto wame-mmisi wanataka aje kuwatembelea, kweli anafika na kuwaletea
vizawadi watoto na kukuachia pesa kidogo ya matumizi ya watoto, lakini
haitoshelezi kama ilivyokuwa zamani. (Mke mpya ameshikilia matumizi yake yote)
Mnapanga kutoka matembezi kidogo,
mnakumbushiana wakati mzuri mliokuwa nao zamani na hamadi-bila kutarajia, na
ngono mnashiriki! Kwa muda mchache unasahau taabu na dhiki na upweke uliokuwa
nao wote!
Punde, mmemaliza kila kitu anakuaga kurudi kwa
mkewe anapiga simu, ghafla unagundua sio wako tena na dhiki, taabu na upweke
unarudi kama ulivyokuwa siku zote!
NDIPO: Unagundua sasa unahusiana ‘dating’ na
wanaume wawili tofauti, ambapo wote wawili wamewasaliti wake zao na wewe ndio
sababu!
Ghafla unaikumbuka ndoa yako, uhuru uliokuwa
nao ukiwa na mume wako wa ndoa, kisha unagundua ni kama dunia nzima imekugeukia
na maisha hayako sawa kwako!
Unaweza kudhani hii ni stori tu, lakini kuna
wanawake wanaoiishi kiuhalisia, na ninge’ au ningalijua huja baada ya kuwa
tukio lishatokea. Siungi usaliti ndoani, Lakini pia siungi vitendo vya ukatili ndoani" Mninukuu vizuri!
Mbali ya tofauti zetu, familia ni baba na mama na sio mzazi mmoja, licha ya changamoto zilizoko ndani ya familia hizo.
Asilimia kubwa ya ndoa zinawaka moto, na sio
salama kwa asilimia mia, (Ni kusameheana na kuvumiliana) Tafakari chukua hatua!
#MwalimuMeena (0778291375) Kwa Maoni, au Unahitaji ushauri wa ndoa nipo hapa kukushauri!
Unaweza
kusambaza elimu hii: (Share) iwafikie wengi zaidi, lakini (usi-copy na ku-paste)
na kufanya kama ni chanzo cha mawazo na Sanaa yako) ukifanya hivyo nipe credit
yangu katika chapisho lako. Asante!
Monday, 24 August 2026
NINI HUTOKEA, MAUMIVU TUMBO LA HEDHI KWA WANAWAKE?

Picha: JohnsHopkin Health Blog
Kuingia hedhi ni jambo la kawaida kwa kila binti/msichana aliyepevuka itoshe kusema "Ni jambo la kujivunia" kwakuwa hedhi ni kipimo sahihi cha kuwa Mwanamke ambaye siku za usoni utatarajia kuitwa mama; na ikiwa binti huioni hedhi yako inapaswa kuwaona madaktari mapema kutibu na kushughulikia tatizo hilo haswa kwa wasichana waliokatika umri wa kuvunja ungo (kupevuka)
Nini hutokea wakati wa hedhi!?: Kibiolojia hedhi hutokea baada ya kupita zile siku za urutubishaji wa yai (Ovulation circle) ambapo hii hutukia wiki ya3 kwa wanawake wengi wenye mzunguko wa siku21, 28 na 31.
Wakati huu, Yai ambalo halijarutubishwa (kwa kukutana na mwanaume) hutolewa kutoka kwenye ovari za mwanamke kwa mfumo maalimu wa mwili (kuflashi) na hapo muhusika huweza kuona uchafuuchafu wa kawaida, na damu kwa muda wa siku2, 3 au 4, huku wengine wakienda mpaka wiki moja (siku7) ambapo hii watabibu wengi huieleza kuwa sio nzuri sana kiafya, ila kikawaida inatakiwa siku4 iwe imekata.
Ni wakati huu wa hedhi: Wanawake wengi hupitia madhila mbalimbali yakiambatana na #maumivu_makali chini ya kitovu, kuumwa na kiuno na mgongo, kichefuchefu, kukosa hamu ya kula na kutapika.
Nikiwanukuu baadhi ya kina dada wanasema:
"Mimi staki kuongea maana nahesabu siku tu nianze kuhangaika daa mungu sijui sababu zake lakini kwakweli ata ukielezea akuna atakaye kuamini";
- "Tunywe Maji Ya Karafuu, Ikifika Siku Wala Tumbo Haliumi"
- "Chai ya moto yenye mchanganyiko wa tangawizi, karafuu, mdalasini, hiliki inanisaidia sana"
- "Ikianza tuu day one chemsha mizizi ya mkunde pori kunywa ila hii #kupata_mimba ni nje nje inasaidia na tatizo halijirudii me nshasahau hzo mambo za kuumwa tumbo baada ya kupata ujauzito na kujifungua"
- "Kpindi Cha ubinti wangu nilikuwa naumwa mnoo yaani hadi home walikuwa wanajua, lakini tangu nijifungue mwanangu siumwi tena na chochote yaan"
- "Tumbo la P, mdogo wangu alikuwa anaumwa mpaka anazimia... Ila tulijitajidi kumchemshia #mzugwa mara nyingi tuwezavyo sa hivi anaumwa ila cyo km zamani"
Asante kwa kutufuatilia, na tafadhali Like page hii: https://www.facebook.com/stewart.meena na utu - Follow, ili kusoma na kupata habari, na makala nyinginezo za kuvutia kama hizi.Saturday, 22 August 2026
MFAHAMU NDEGE KORONGO AINA YA MARABOU, 'THE UNDERTAKER'
Na.
Stewart Meena
Kutana na ndege wasio na sauti au
"mlio", wenye miguu mirefu na wenye kuweza kuhimili ongezeko kali la
joto" ikilinganishwa na ndege wengine warukao, na hiyo ikampatia sifa ya
upekee na majina mbalimbali kama:
"Undertaker, na Marabou storks" Kiswahili
wakijulikana kama ‘KORONGO MARABOU’
Ndege hawa, ni waviziaji na vyakula vyao vikuu
ni pamoja na mabaki ya mizoga ya wanyama tofauti, mabaki ya vyakula vitumiwavyo
na wanadamu, samaki pamoja na vyakula vingine kama, mijusi, nyoka, vyura,
wadudu, panya na ndege wengine wadogowadogo.
Makazi makuu ya ndege hawa ni maeneo yote
karibu na mito, maziwa, milimani ndani ya miamba, na kwenye hifadhi za
wanyamapori, tambarare zilizo na miti mirefu, ambapo licha ya urefu na ukubwa
wao, wanaweza kuruka katika eneo kubwa la anga na kupaa umbali mrefu.
Kuruka kwao, huweza kuruka hewani umbali wa
futi-13,000 (feet) toka usawa wa bahari, na inapokuja swala la mwendokasi
katika jamii yao ya ndege, Korongo huwenda hawa wakawa wana kiwango kidogo cha
mwendokasi huo.
UKWELI USIOUJUA KUHUSU NDEGE HAWA.
Marabou stork, ni miongoni mwa ndege wasiovutia (ugliest bird on the world) kwa kuwatazama, kwa mwonekano wao (wakiwa na Miguu mirefu, shingo ndefu na eneo kama tumbo la kuhifadhia chakula linaloning’inia karibu na shingo yao likiwa na rangi ya pinki (Eng: a pink gular sac).
Ndege korongo huyu, hutambulikana pia kama
ndege muuwaji kwa muonekano wake kwa nyuma ukiwa unamtazama, wazungu wakimuita “Nature’s
eyesore / the undertaker bird” na ndiye ndege jamii ya tai mwenye miguu mirefu
katika jamii hiyo centimita karibu 50, huku mbawazao zikiwa na urefu wa futi11
na kuwafanya ndege hawa kuwa na upekee tofauti na ndege wengine.
Sambamba na ndege wote kuwa au kutambulikana
pia kwa milio yao, ndege hawa hawana milio hiyo, ingawa huweza kuwasikia
wakitoa milio Fulani inayotokana na kugongesha midomo yao au mbawa zao.
Hadi kufikia umri wa ukomavu ndege hawa,
huchukua karibu miaka mine ‘4’ na kuwafanya miongoni mwa ndegw wanaokua
taratibu-taratibu Zaidi ikilinganishwa na ndege wengine wanapoanguliwa kwenye
mayai yao.
Korongo hawa wa marabou, hupatikana pekee yake
barani Afrika (Ukiacha waliohifadhiwa katika zoo za wanyama) kwenye maeneo ya
kitropiki kwenye nchi kama, Senegal, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Tanzania,
Kenya, Uganda, Namibia, Congo, Afrika ya Kusini nk.
(Unaweza kusoma pia hapa)
Kwa nchi ya Tanzania: Ndege hawa ni maarufu Zaidi
kwenye ukaanda wa ziwa Victoria na Tanganyika, na huweza kuwaona Zaidi kwenye
hifadhi ya taifa ya Serengeti, Manyara, Nyerere, Tarangire nk. Ambapo wenyeji
wa mikoa ya Manyara, Mara, Mwanza, Geita ndege hawa huingia hadi maeneo ya
masoko na mijini.
Marabou (Korongo) ni ndege anayependa
kuchangamana Zaidi na binadamu ndani ya makazi yao na hii ni kwa ajili ya
urahisi wa kupata vitoweo vyao, huku wale kwenye hifadhi ya wanayama hupendelea
Zaidi kuwa karibu na wanyama wawindaji kama Fisi, Chui, Duma, Simba na Mbweha
ikiwa ni sehemu rahisi kwao kuvizia mawindo yao na kuyaiba. (Marabou stork are
known to be scavenger bird) Kimsingi ndege hawa korongo sio wawindaji hodari,
ila ni waviziaji hodari.
Picha: Natalie Carberi
Wanawezaje Kuhimili Joto Kali La Uwanda Wa
Savana?
Ili kupunguza ongezeko la joto na jua kali
linalowatesa ndege wengi, kwa ndege Korongo ni tofauti kidogo, ambapo miili yao
inauwezo wa asili wa kubadili kanijoto mwili wao kuendana na ukali wa jua au
joto la maeneo waliyopo, kuficha uso wao ndani ya mabawa na kutanua mfuko wao
wa pinki uliopo chini ya shingo huwawezesha kuendana na mabadiliko hayo ya
joto.
Na endapo kutakua na baridi kali na wanahitaji
joto, basi hutanua mabawa yao (mbawa) na hiyo huwawezesha kurudisha kwa haraka
ongezeko lao hilo la joto ndani ya miili yao.
Kimazingira kwenye jamii yao, huwenda hawa
ndio ndege wavivu zaidi na wasiopenda kuhangaika kutafuta vitoweo, isipokua
kusimama karibu na wanaotafuta (kuwinda) na wakishapata kitoweo chao wao ndio
huenda eneo hilo na kuwafurusha kwa ajili ya kuiba kitoweo hicho. Mfano: Kanda
ya ziwa huiba samaki zilizovuliwa na wavuvi.
Mazaliano yao hupendelea zaidi majira ja
kiangazi wakati kina cha maji maeneo mengi yakiwa yameshuka au kukauka, kwani
ndio urahisi zaidi wa wao kupata vitoweo vyao kwa urahisi zaidi.
Ni msimu huu huweza kuwaona ndege hawa wakiwa
karibu-karibu zaidi, na madume wakipambana kwa midomo yao ili kuwania haki ya
kumiliki korogo jike kwa ajili ya mwanzo wa mazalia yao, ambapo atakayeshinda
ndio kuanzia hapo ataambatana na jike husika kwa muda wote wa kujenga kiota,
kurutubisha mayai, kutaga na kuyaatamia, kisha watoto watakao anguliwa
kushirikiana kuwatafutia chakula kwa pamoja hadi watakapoweza kujitegemea
wenyewe.
Ndege hawa wakishaungana, huishi hivyo wawili
pekee kifamilia hadi mwisho wa maisha yao, na ajabu nyingine ni kuwa
hawachanganyi mwenza na ikitokea mmoja kati yao amekufa mwingine huakia hivyo
hivyo na huelezwa, sababu ya upweke na yeye hachukui muda mrefu kabla ya kufa, ambapo
baadhi ya tafiti husema ndege mwenza aliyesalia huweza kujinyima chakula kama
njia ya yeye kufa.
Waweza pia kusoma HAPA
MWISHO: Kwa sababu ya urefu wa miguu yao, mbawa zao na midomo yao hii huwafanya kuwa na uwiano sawa wenye kupungua uzito hivyo kumuwezesha kuruka kwa urahisi zaidi wanapopaa angani, ikilinganishwa na jamii nyingine za ndege walio na urefu na uzito kama wa kwake.
Pia eneo la pinki karibu na shingo yake,
hutumia hapo kama akiba ya kuhifadhi chakula chake akiwa ameshiba, kisha kula kwa
wakati mwingine hususani anapokuwa ana njaa.
Tafadhali unaposasisha (Kushare taarifa hii),
hakikisha unatambulisha chanzo cha taarifa hii kwa kutupa ‘credit’ Asante! StewartMeena
Wednesday, 19 August 2026
ATHARI / MADHARA YA KUKAA NA HAJA NDOGO KWA MUDA MREFU
![]() |
| Image by: Harbin Clinic |
Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call.
Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika
mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na
kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji-taka mwili, haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli
anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili 'kuwa kibofu chake kimejaa.
Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli,
ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi
wafanyavyo kimazoea kitu ambacho hakishauriwi kitabibu na kwa afya ya mwili wako.
Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia katika milo yetu kila wakati, kibofu cha mkojo
huanza kujaa mkojo, unaojitengeneza wakati vyakula vinachaguliwa (Kuchakatwa) na mwili, hivyo mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huyo husika huanza
kuhisi hitaji la kwenda haja ndogo (kukojoa).
Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili (Receptors)
vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia
au kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa
katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli
maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.
Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe
yaani, automatic, kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha Ubongo
upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa Ubongo nao
hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa
mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo kutoa taarifa
hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha
mkojo kupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo.
Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika kuvumilia kidogo ili
afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena na kujikuta muda mdogo
tu….mtu tayari kaloanisha nguo yake.
Mpenzi msomaji, mtu kujibana na kupuuzia kwenda haja ndogo mara
kwa mara husababisha uwezo wa kibofu chake cha mkojo kushindwa kujitawala upotee.
Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu
mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi misuli maalumu ya
kubana mkojo (sphincter) itashindwa kuachia na matokeo yake mtu ataendelea
kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu ambacho ni hatari
kwa afya yake.
Endapo mkojo huu utashindwa kutoka, utatengeneza mazalia ya
bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection), kama vile U.T.I
(Urinary Tract Infections), na pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na
mchafuko wa damu, (bacteremia).
Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu, yawezekana
alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila akinywa maji
au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka bombani, basi
atahisi kwenda kukojoa.
Mpenzi msomaji, ni vyema tukawa wasikivu pale mtu unapobanwa na haja (mkojo), hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa
ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo, usisite kuonana na wataalamu
wa afya..
Monday, 17 August 2026
ELEWA CHANZO CHA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI (KIDNEY FAILURE)
![]() |
| Picha na: Ahli Hospital |
FIGO ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji
kazi wa mwili wa binadamu. Wiki iliyopita nilieleza jinsi kiungo hiki
kinavyopata mawe na jinsi ya kujikinga na tatizo hili.
Chanzo: Global
Nashukuru wengi wamepiga siku kushukuru kwa elimu ile. Kwa
kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale
ya maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo
ya mbavu za chini.
Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu
katika damu na hivyo kusaidia katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na
madini (electrolytes) mwilini.
Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji
yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini
huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu
na kutoa nje uchafu usiohitajika.
Kazi nyingine za figo ni kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu
mbalimbali katika damu pamoja na kiasi cha maji katika mwili, husaidia
kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana katika
utengenezaji wa chembe nyekundu za damu, husaidia uzalishaji wa vitamini D na
husaidia pia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).
Kwa kawaida damu inayozunguka mwilini hatimaye huingia kwenye
figo kwa ajili ya kuchujwa, kutoa uchafu pamoja na sumu nyingine zisizohitajika
mwilini.
Kitendo hiki cha utengenezaji mkojo hufanyika katika hatua kuu
zifuatazo;
Hatua ya kwanza ni UCHUJAJI.
Damu kutoka nje huingia ndani ya mafigo na kupita kwenye
glomeruli, lenye umbo kama chekeche/chujio ambalo limeundwa na mishipa mingi
midogo ya damu iliyojizungusha pamoja.
Vitu mbali mbali, maji pamoja na sumu zilizo katika damu
inayopita kwenye vimishipa hivi na kisha kuingia katika mirija mingine mikubwa
kwa ajili ya uchujaji zaidi.
Mirija inayofuata huendelea kuchuja damu na kunyonya baadhi ya
vitu vilivyo chujwa kimakosa kuvirudisha mwilini, mpaka kiasi sahihi cha uchafu
kinachotakiwa kuchujwa kinapokuwa kimefikiwa.
Mara baada ya mkojo kutengenezwa na kutolewa kwenye figo,
husafiri kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa kupita kwenye mirija ijulikanayo
kama ureta.
Kutoka kwenye kibofu, mkojo hutolewa nje ya mwili kupitia kwenye
mrija wa urethra.
Kushindwa kufanya kazi kwa figo hutokea iwapo sehemu ya figo au
figo lote litapoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kutoka katika damu na
kutengeneza mkojo.
Kitendo hiki husababisha kusanyiko la uchafu pamoja na sumu
kadhaa katika damu ambazo ni hatari kwa afya ya mhusika.
Figo kushindwa kufanya kazi kumeganyika katika makundi
yafuatayo, Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF),
Figo kushindwa kufanya kazi kwa kiasi (Mild renal/kidney insufficiency) na
tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi (Chronic renal failure).
Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure
(ARF) Hii ni hali inayotokea kwa ghafla, na kudumu kwa saa chache mpaka siku
chini ya 14, na kusababisha ongezeko la kiwango cha creatinine na urea katika
damu.
Hali hii huwapata karibu asilimia 5 ya wagonjwa waliolazwa
hospitali kwa sababu ya matatizo mbalimbali. Aidha hali hii hutokea zaidi kwa
wagonjwa mahututi na wale wanaohitaji uangalizi wa kipekee, yaani waliolazwa
ICU.
SABABU ZAKE
Visababishi (au aina) vya ARF vinaweza kugawanywa katika makundi
makuu matatu: Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika
figo (Prerenal causes/failure), matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na
kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure),
matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/
failure)
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika
figo (Prerenal causes/failure) Aina hii hutokea kwa takribani asilimia 60 mpaka
70 ya ARF zote. Katika kundi hili, figo hukosa damu ya kutosha kwa ajili ya
kuchuja na hatimaye hushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Mambo
yanayoweza kusababisha pre-renal failure ni pamoja na:
Upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kutapika kupita kiasi,
kuharisha, au kupoteza damu kupita kiasi (kwa sababu ya ajali au kuumia),
kuvurugika kwa mtiririko wa damu inayoingia kwenye figo kwa sababu ya: Kushuka
kwa ghafla kwa shinikizo la damu kwa sababu ya kupoteza damu nyingi wakati wa
upasuaji mkubwa, kuumia au kuungua sehemu kubwa ya mwili, au maambukizi katika
mfumo wa damu (sepsis) yanayoweza kufanya mishipa ya damu kutanuka na kushusha
shinikizo la damu, kuziba au kusinyaa kwa mishipa inayopeleka damu kwenye figo.
Figo inaweza kufeli pia kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi
(heart failure) au shambulio la moyo (heart attack) linalosababisha kushuka kwa
shinikizo la damu na ini kushindwa kufanya kazi (liver failure) kunakoweza
kusababisha mabadiliko katika mfumo wa homoni zinazoathiri shinikizo la damu
pamoja na mtiririko wa damu kwenda kwenye figo.
Mwanzoni kabisa mwa pre-renal failure huwa hakuna athari yoyote
inayotokea kwenye figo, na mara nyingi, figo laweza kurudi katika hali yake ya
kawaida iwapo chanzo cha tatizo kitagunduliwa na kushughulikiwa ipasavyo.
Mambo yanayosababisha madhara katika figo husababaisha karibu
asilimia 25 mpaka 40 ya vyanzo vyote vya ARF. Visababishi vilivyo katika kundi
hili hujumuisha vile vinavyoathiri uchujaji, mtiririko wa damu ndani ya figo na
seli za figo zinazoshughulika na uchujaji na ufyonzaji wa chumvi na maji.
Visababishi hivyo ni pamoja na: Magonjwa katika mishipa ya damu,
kuwepo kwa damu iliyoganda ndani ya mishipa ya damu inayopita katika figo,
ajali/ Kuharibika kwa tishu na seli za figo, magonjwa ya mzio katika glomeruli
na figo kwa ujumla (glomerulonephritis).
Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na maambukizi
(infection) ya bakteria jamii ya streptococci.
(More: Here Endelea kusoma hapa)







