Image copyright: fakazanews
Na. Stewart Meena
Mahusiano siku
hizi za karibuni yamekuwa na chagamoto nyingi sana kiasi kwamba Watu
wanapoingia katika mahusiano (Uchumba) inakuwa kama kila mmoja ana mashaka na
mwenzi wake kuwa je ana malengo ya kufanya maisha pamoja ama yuko kwa sababu ya
jambo Fulani na anapita tu baada ya muda hudai kuachana.
Kisaikolojia:
Mwanamke hupenda kwanza kasha mengine hufuatia baadae, tofauti na Wanaume wao
hutamani kwanza kasha kupenda huja baadae “Yaani kupenda kwao hutokea ndani ya
huo uhusiano, alikotamani kwanza” na hapa ndipo bahati mbaya kwa Wanawake
huwaona Wanaume zao kama hawaeleweki, lakini pengine Wanawake hawa wameshindwa
kuchunguza mambo ambayo Mwanaumeze wake hupende, kasha aishi humo na baadae
kueleweka na kupenda kwa Mwanaumehuja tu moja kwa moja (Automatic)
Tabia za mwanaume
zinazochagizwa na kuwa na mwanamke kwa kumtamani kwanza ndio hupelekea mwanamke
husika amuone mwanaumw wake ‘Haeleweki’ kasha hujikuta amefanya maamuzi ya
kumuacha Mwanaume wake, na kwenda sehemu nyingine, mpaka pale atakapopata huyo
anayedhani kwake anaeleweka".
Bahati mbaya ni
kuwa kwa kutokufahamu kwake, tatizo halipo hapo kwa (Mwanaume wake haeleweki)
ila lipo hapa kwenye kufahamu Mwanaume wake nini anapenda kutoka kwake kwenye
hayo mahusiano, na ni vipi mwanamke huyo ajiweke vile ambavyo mwanaume wake
anavyopenda ili kutengeneza Uhusiano imara na wenye kuzaa matunda ya ndoa na
Familia.
Kimsingi: Ulishawahi
kusikia Kauli Kama hizi Kwa wanawake, wakisema mwanaume Yule haeleweki, Mpenzi
wake haeleweki, au hata wale walio kwenye ndoa utasikia pia wanasema Mume wake
haeleweki, mchumba wake haeleweki nk.
Nachotaka
kuwakumbusha Wanawake na Wanaume ni kuwa: Mwanaume hutamani kwanza kasha kupenda
huja baadae; na Mwanamke hupenda kwanza kasha kutamani kuwa na huyo mwanaume
huja baadae, ‘Ndio maana wahanga wakubwa wa hii KUTOKUELEWEKA’ ni wanawake
zaidi ya wanaume sababu tayari wameingia sehemu kwa kupenda kwanza, na walicho
kitegemea ni tofauti sana na wanaume zao walichokiwaza.
WANAWAKE WASEMAPO
‘Mwanaume haeleweki’ HUMAANISHA HAYA
YAFUATAYO:
- Mwanaume ameshindwa kumfanya ajione yupo pekeake moyoni mwake, na pia hana uhakika yeye ndio utaolewa.
- Mwanaume kutoa mara kwa mara zisizotimilizika, Wanawake hupenda kuwajaribu wanaume zao kwenye ahadi wawapazo.
- Mwanaume kuficha chanzo cha kipato chake kwa Mwanamke wake, na hivyo kumfanya Mwanamke wake kushindwa kujua siku Mwanaume wake akiwa na pesa ama asipokuwa na pesa, hivyo anakuwa hana uhakika na huduma atakazozipata pindi atakapoolewa.
- Mwanaume kuficha shughuli azifanyazo, kuficha ndugu zake, marafiki zake kwa Mwanamke husika kwa kutokutaka mwanamke huyo atambulike kwao,na kumwambia sio wakati sahihi kutambulishwa, kwa kuwa bado ana hofu ya kutambulisha kasha baadae kuachwa solemba hivyo ni kama na yeye anatega-tega hivi.
- Mwanaume anayepoteza kumbukumbu za matukio muhimu kwa mwanamke wake, hupelekea kutoeleweka na mwanamke husika hushindwa kuelewa wanathaminiwa na kupendwa ama laah. “Wanaume wanaopoteza kumbukumbu hasa zile za muhimu kama birthday zao, Ahadi wazitoazo nk, Mwanamke hufikiri Mwanaume wake hamjali.
Image: ThePrint |
HIVYO: Katika mahusiano (Uhusiano) Mwanamke anahitaji kwanza ‘Life Security’ kama ‘Kuthaminiwa, Kupendwa yeye pekeake, kuhudumiwa mahitaji yake mbalimbali, Kutunzwa au kupewa kipaumbele kwanza na (Kudekezwa – Hii ipo kwa wote wawili).
WANAUME:
Kadhalika, hupendelea kufanyiwa yale wawafanyiao wenza wao, na wasipofanyiwa
huanza kuwa na mashaka na sehemu waliyoko na kukaa nusunusu (Kwa mashaka) na
kuwaza kuachana muda mwingi sababu tunaishi kwenye Dunia ambayo kuachana
imekuwa ‘Faheni’
WANAUME WASEMAPO ‘Mwanamke haeleweki’ HUMAANISHA HAYA
YAFUATAYO:
- Mwanamke kushindwa kumfanya mwanume ajione yupo pekeake kwako, na hata iweje huwezi kumsaliti kwa wengine sababu unafaa kuaminiwa na ni mwanamke unayejiweka mbali na mambo ya anasa kama Pombe, Starehe, kwenda club nk. Lazima Mwanaume wako asikuelewe sababu mazingira kama hayo kumsaliti ki tendo la dakika1 tu.
- Mwanamke, kutamani kila jambo zuri ufanyiwe wewe tu, na wewe huna hata siku moja unayotamani kumfanyia mwanaume wako mambo hayo mazuri wewe unayotaka ufanyiwe. Mfano: Kutafutwa kwa simu, wewe ndio utafutwe tu, vijizawadi wewe ndio upewe tu, kusifia wewe ndio usifiwe tu, birthday wewe ndio ikumbukwe tu na ufanyiwe, khaa! Kwani yeye sio mja (Binadamu!?) Lazima mwanaume wako ahisi hufurahii yale ambayo anakufanyia.
- Mwanamke kufuja fedha, yaani wewe hujui kama kuna kupunguza matumizi yasio ya lazima sana, hujui ‘kuSave’ kwa ajili ya kesho au maisha yenu ya siku zijazo, wewe kila siku ni kuitisha vitu tu vya gharama, badala ya kupika mle nyumbanikila siku unataka mitoko ya hoteli kubwakubwa-, sawa utapewa yote hayo lakini mwisho wa siku mwanaume huyo utamuona haeleweki kwako, punde akishakutumia. ‘Wanaume hupenda na hutulia kwa Wanawake wanaoifikiria kesho yao’
- Kama ilivyo kwa Wanaume, Mwanamke kuficha kipato chake, kushindwa kumsaidia mwanaume wake hata kwa mambo madogo-madogo, lazima taa nyekundu iwake kichwani kwa Mwanaume husika “Yaani Mwanaume anaweza kukwambia hata kwa kukutega-naumwa, sina hata pesa ya kwenda kupima, na wewe kwa kujitutumua unamwambia ‘Pole utapata, badala ya kumwambia ngoja tufanye maarifa, au nna elfu5 hapa tafuta ya kuongezea, au ngoja nikuletee paracetamol utilize maumivu nk. Mwanaume lazima akuone hueleweki na mwishowe hutafuta huyo atakayeeleweka.
HIVYO: Katika
mahusiano (Uhusiano) Mwanaume kamailivyo kwa Mwanamke, naye anahitaji kwanza ‘Love
Security’ tofauti na Mwanamke anahitaji kwanza (Life Security), kama
‘Kuthaminiwa, Kuonyeshwa anapendwa pia, kutekelezewa huduma na mahitaji yake
mbalimbali ya msingi, Kupewa kipaumbele kwanza kabla ya ndugu zako na marafiki
zako, na zaidi kumsikiliza kwa yale anayotaka ufanye na yale asiyoyataka
usifanye. (Wanaume hupenda sana kusikilizwa na kupewa nafasi ya kuwa kiongozi
wa uhusiano wenu, na sio kupandwa kichwani n.k).
WANAWAKE: Huwaelewa
wanaume wanaotimiza ahadi hasahasa ahadi ndogondogo kwani kupitia kutimiza
ahadi kunamfanya akuamini na azidi kukupenda, yaani ni Bora usimuahidi jambo
lolote kuliko utoe ahadi ambazo utashindwa kuzitimiza, jambo ambalo yeye analichukulia
Kama Deni.
Fikiria: Unapenda mwenza wako akufanyie nini,
hivyo upendavyo vivyo hivyo Mwanza wako naye hutamani wewe umfanyie hay ohayo “Na
ukimfanyia atafurahia vile ambavyo wewe ufurahiavyo”
MWISHO: Wanaume wenye kufikiria kutumia
mabavu, Maneno machafu, makali au Kauli za vitisho na Kuhisi mabaya kwa
mwanamke wake, “Mfano, kumwambia – Unachepuka eeh, ondoka kwenu, nitakupa talaka,
nitaongeza mke mwingine n.k” huwanyong’onyeza wanawake husika na kujiona hawako
sehemu sahihi, sababu Wanaume wanachopaswa kufahamu ni kuwa “Wanawake huamini maneno
zaidi kuliko hata matendo” yaani Kadiri unavyomtisha mwanamke wako unamtengezea
mazingira ya kujihami na kujiandaa Kwa lolote ‘Kuachana, Kuchepuka nk’.
Kama ilivyo kwa Wanawake, Wanaume pia hawapendi kuishi na mtu wasiyemuelewa, kwani kila mmoja hufikiria usalama wake kwenye huo Uhusiano, hufikiria kumpata mtu sahihi wakufanya naye maisha na atakaye mthamini katika wakati wa shida na raha hadi umauti umfike mmojawapo.
Tafadhali, uchukuapo na kunakili makala tambulisha na blog hii: Saysteefeatures.blogspot.com" asante; Share Makala haya na Wengine wapate kuelimika zaidi kuboresha mahusiano yao.
Source: (Msaada wa Mitandao Washirika)
Tufuatilie Mitandao ya Kijamii:
Facebook: www.facebook.com/stewart.meena
Instagram: @ Master The Last
No comments:
Post a Comment