Ikiwa ni mwaka 2020, na baada ya kimya kirefu kidogo hatimaye tumerudi tena kukuletea zile Makala zako pendwa katika blogi hii, nikukaribishe tena tuwe pamoja.
Makala
hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa
wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika
kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe
inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa, Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane
ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya
kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu
za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la
ndoa’. Na inapokuwa
tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.
Kupungukiwa
kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni
hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha maumbile hayo, au hali ya kutokuwa na
uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Pamoja
na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za
kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali
zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.
VYAKULA VINAVYOONGEZA NGUVU ZA KIUME
Chukuwa
punje 8 mpaka 10 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo
kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja.
Pia
hakikisha kila chakula unachopika basi kitunguu swaumu lazima kiwemo kama moja
ya viungo na ukiweke mwishoni mwishoni kwamba kisiive sana katika moto wakati
unapika hicho chakula.
Kula
tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote.
Kula
ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe.
Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume.
Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo10 ongeza
ngano kilo3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na
unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake.
FANYA
HIVI KATIKA FAMILIA YAKO KWA MAISHA YAKO YOTE
Chumvi
ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango
mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako
kila siku.
Kunywa
maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka
10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.
Ziloweke
katika maji yenye chumvi, zikaushe, Zikaange kidogo bila kuziunguza, Tafuna
mbegu 100 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja, Ukitafuna meza vyote, hakuna
cha kutemwa hapo.
Mbegu
hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo
la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako.
Chukuwa
lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko
vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja; Lamba kijiko kimoja
kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.
Tangawizi
ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na
tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi
yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama
unga.
Ulaji
wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu
na nguvu ya tendo la ndoa.
Unaweza
ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza
ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima
nusu saa kabla ya tendo.
Kunywa
chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka
tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai
humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja
na ganda lake la nje.
Sasa
badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na
ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni
dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!
Source: FadhiliPaulBlog