Monday, 1 January 2018

UTAFITI MPYA WAONYESHA MAZOEZI BAADA YA MAFUNZO KWA MABINTI HUSAIDIA KUTUNZA KUMBUKUMBU

Wanafunzi wa Lk. Vicent Arusha wakiwa katika mazoezi yao ya kila wiki baada ya masomo. Picha: na Zuhu-Hamza
Utafiti mpya uliofanywa kwa pamoja baina ya Australia na Marekani umeonesha kuwa, kufanya mazoezi baada ya kujifunza kunaweza kuimarisha kumbukumbu za mambo mbalimbali uliyojifunza, kwa watu wote lakini Zaidi haswa kwa mabinti.

Watafiti hao waliwagawanya washiriki 265 wenye umri wa wastani wa miaka 14-20 kwa vikundi kadhaa na kufanya jaribio husika, ambapo kwenye jaribio hilo Washiriki wote wa kila kikundi walitakiwa kukumbuka sura pamoja na majina ya watu 15 kwa kuonyeshwa tu mara moja na kutajiwa jina lake.

Baada ya utambulisho na kuziweka akilini, kikundi kimoja kikatakiwa kufanya mazoezi ya kupanda ngazi kwa dakika tano bila kupumzika, huku kundi jingine likipewa jaribio la kwenye mchezo wa meza (dati/drafti) na baada ya hapo, washiriki wote kwa pamoja walitakiwa kuandika majina wakilinganisha na sura walizozihifadhi akilini mwao.

Na Matokeo yalipotoka yameonesha kuwa wasichana ndio waliofanikiwa kukumbuka kwa wingi wa asilimia zaidi ya 80, ukilinganisha na wavulana 65%, hivyo kwa matokeo hayo ndipo ikabainishwa kuwa "kufanya mazoezi baada ya mafunzo kunaweza kuimarisha kumbukumbu za mambo tofauti tuliyojifunza".

Lakini kwa tamaduni zetu tofauti na mazingira tofauti tunayolelewa na kukulia huelezwa pia kuchagiza uelewa mkubwa au duni wa watoto, kutokana na kuwa kupata au kupewa fursa ya kufanya udadisi kwa watoto wenyewe kama vile kucheza michezo ya kibunifu, kupewa vitabu mbalimbali vya kukuza uelewa nk. ikiwa haipo haswa kwa nchi zetu za kiafrika.

Uelewa wa mtoto haupatikani kwa kufundishwa nadharia mashuleni pekee, bali lazima iambatane na michezo na mafunzo ya vitendo kwa watoto wenyewe kujifunza na kuweza kutatua mafumbo magumu mbalimbali peke yao, Mfano: Kwa shule zile za kibunifu, St.Constantine Arusha na nyinginezo hizi huelezwa wanafunzi wake kufanya vizuri Zaidi kiakili na kiugunduzi kutokana na kuwa  watoto huandaliwa kwanza kutatua mafumbo magumu ili kukuza "Ufikiriaji wao" kabla ya kuanza kufundishwa kwa nadharia mafunzo mengine)

Hivyo basi, Wasichana wengi hasa katika nchi zetu za kiafrika hutingwa na majukumu mengi ‘haswa "kazi za nyumbani" ukilinganisha na mtoto wa kiume, na hivyo nafasi ya wasichana hao kujihusisha na mazoezi au kupata muda wa kuufikirisha ubongo wao zaidi kuwa hafifu, lakini pia hawaandaliwai kufanya mazoezi ya aina yoyote.

Na kwasababu hizo na nyinginezo mabinti hawa wanaotingwa na shughuli nyingi, wengi wao wanapofika mashuleni huanza kusinzia wanapofundishwa kidogo, au pengine mawazo yao kuwa mbali na darasani na hivyo kutokuelewa maramoja kwa kile walichojifunza darasani kwa wakati  huo huo.

Wataalamu hao kutoka Australia na Marekani, wanasema kwamba wasichana wanaofanya mazoezi baada ya mafunzo, wana asilimia zaidi ya 70 kufanya vizuri katika mambo yanayohitaji kumbukumbu, ukiilinganisha na wasichana wangine wasiofanya mazoezi baada ya mafunzo.

Sasa wewe mzazi binti yako humpi hata nafasi ya kucheza michezo na kufanya mazoezi mbalimbali, sasa unategemea nini! wakati unatambua fika chochote wanachojifunza mashuleni au vyuoni huitaji kuufikirisha ubongo Zaidi.


Sehemu ya utafiti huo imedokeza pia, ili kuongeza kumbukumbu kwa wanafunzi kwa kile wanachojifunza, shule zinatakiwa kutenga muda wa walau nusu ya muda darasani na nusu ya kufanya mazoezi, ili kuupa ubongo nafasi ya kutunza kile kilichosomwa. (Mfano muda wa masomo ni 8 kwa siku, basi 4 yawe darasani na masaa mengine ma4 yawe kufanya mazoezi kwa kucheza michezo mbalimbali.)

Shule nyingi zimepunguza muda wa kufanya mazoezi, lakini ukweli ni kuwa mazoezi yanaweza kuwasaidia wanafunzi hao kuimarisha kumbukumbu zao.

Sasa hapa niulize swali kwa mabinti, uonavyo wewe kati ya kulala na kufanya mazoezi kama njia moja wapo ya kutunza kumbukumbu zako mwenyewe, wewe ungechagua au ungependekeza kuifuta njia gani zaidi.?!

Binafsi, naamii baada ya Utafiti huu, na endapo walimu na wazazi wakiutumia vyema, basi itasaidia kukuza uelewa kwa wanafunzi kufanya vyema kwenye masomo yao, lakini pia utazisaidia shule husika kuweka ratiba mpya za mafunzo na kuinua ufanisi wa kujifunza wa wanafunzi hao. Kwanini zero ziendelee..! Tutokomeze ziro kwa pamoja.

Tuma kwa Rafiki zako nao wapate Elimu hii.......
TUANZE MWAKA HUU MPYA KWA TAFITI HII (HERI YA MWAKA MPYA-2018)

MUENDELEZO CHANZO:
Radio-Crn & Sydney research: ASANTE NA ENDELEA KUPERUZI!

No comments:

Post a Comment