Haki miliki ya picha Reuters Image
caption Visitors to the festival in al-Dahna, north of Riyadh, can also watch
camel racing
|
Imezoeleka kuwa na aina ya mambo au vitu vinavyofanyika katika eneo au nchi flani kwa Jeografia yake kulitangaza eneo hilo au nchi husika kimataifa kama vile ilivyo kwa matukio tofauti yanayowahusisha wanadamu kukusanyika eneo flani moja kushuhudia jambo flani.
Pengine ni ubunifu, au uwepo wa tafsiri tofauti na baadhi ya mambo ambayo binaadamu tunavutiwa nayo, yatumiwe vyema kutangaza, kuliwaza na kutuliza akili zetu na mawazo yetu kama vile ilivyo muziki mzuri wenye ala zilizopangiliwa vyema kimirindimo.
Kubwa nalotaka kuzungumzia leo ni kuwa, tanzania na nchi nyingine za afrika mashariki nao wabuni baadhi ya tukio (Event) muhimu ambayo itawakushanya watu pamoja kama njia ya kupata burudani lakini wakati huohuo wakiitangaza nchi yao na utamaduni wao duniani.
HEBU TUANGAZIE HILI LA SAUDI-ARABIA.
Ngamia 12 wamepoteza sifa
za mashindano ya urembo nchini Saudi Arabia baada ya wamiliki wao kuwachoma
sindano ya kubadili maumbile.
Maelfu ya ngamia wameshirikiswa katika tamasha la Mfalme Abdulaziz na kushindanishwa kwa muonekano wa nyuso zao, nundu na maumbile yao.
Lakini majaji waliingia kati wakati walipogundua kwamba baadhi ya udanganyifu ulifanyika na baadhi ya wamiliki waliotaka kushinda tuzo za fedha.
Vile vile tamasha hilo
lina mashindano ya riadha ya ngamia na kuonja maziwa, lina tuzo ya fedha taslim
dola milioni 57.
Mtandao wa habari wa The
National imeripoti kuwa Ali Al Mazrouei, mwana wa mfugaji bingwa , alisema dawa
ya botox ilitumika kwenye midomo, pua na hata taya.
"Dawa hiyo
inavimbisha kichwa kwa hio ukimuona ngamia unadhani ana kichwa,mdomo na pua
kubwa" aliezea Mazrouei.
Majaji pia walikuwa
wakishindanisha nundu na misuli ya ngamia.
Kabla ya tamasha hilo,
vyombo vya habari vya Saudia viliripoti daktari wa wanyama alikamatwa akiwa
pasua ngamia hao ili kuwabadilisha ukubwa wa masikio pamoja na kuwachoma
sindano ya dawa ya kubadilisha maumbile.
Haki miliki ya picha Reuters Image
caption Shindano lina vigezo vikali vya urembo
|
Pia unaweza soma
yafuatayo §
Binti shujaa mbunifu wa Emoji iliyo
na Hijab
Jaji mkuu Fawzan al-Madi
amesema kuwa ngamia ni mojawapo wa "nembo ya Saudi Arabia" kimataifa
na mashindano hayo ya urembo wa ngamia nchini humo yalianza kufanyika kwa mara
ya kwanza tokea mwaka 2000.
SOURCE: bbc Swahili
No comments:
Post a Comment