Wanasayansi wa Denmark wamefanya
utafiti ukionesha kuwa, kutia Lithium kwenye maji ya bomba kunaweza kuwasaidia
watu kukinga ugonjwa wa Alzheimer, ambayo itakuwa njia yenye gharama ya chini zaidi
ya kuzuia ugonjwa huo.
Lithium ni aina ya chuma chenye rangi
ya fedha, ambayo iko ndani ya njia ya bomba katika maji ya bomba. Utafiti wa
awali umeonesha kuwa Lithium inaweza kutumiwa kutuliza hali ya moyo, haswa kwa wale wanaosumbuliwa na presha nk.
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha
Copenhagen wametoa ripoti ikisema, wamelinganisha kiwango cha ugonjwa wa
Alzheimer katika baadhi ya sehemu nchini Denmark na kiwango cha lithium ndani
ya maji ya bomba.
Utafiti umeonesha kuwa, kiwango cha juu cha lithium katika njia ya bomba kinaweza kupunguza dhahiri kiwango cha ugonjwa wa Alzheimer.
Utafiti umeonesha kuwa, kiwango cha juu cha lithium katika njia ya bomba kinaweza kupunguza dhahiri kiwango cha ugonjwa wa Alzheimer.
Watafiti wanaona kuwa kutia lithium
kwenye maji kweli kunaweza kuwafanya watu wengi zaidi kuwa mbali na ugonjwa wa
Alzheimer, lakini lithium hiyo inatakiwa kuwa katika kiwango mwafaka, kwa kuwa
kiwango cha juu au cha chini kinaleta madhara.
Wanasayansi wa Uingereza wamesema,
kiwango cha lithium katika maji kina uhusiano wa wazi na ugonjwa wa Alzheimer,
lakini hatuwezi kutia lithium ndani ya maji kabla ya kufahamu kiwango mwafaka.
SOURCE: Radio China Swh.
TEMBELEA PIA HAPA KWA HISTORIA NA ELIMU ZAIDI: https://www.facebook.com/stewart.meena/
Picha na: Getty Image |
TEMBELEA PIA HAPA KWA HISTORIA NA ELIMU ZAIDI: https://www.facebook.com/stewart.meena/
No comments:
Post a Comment