PICHA NA: NASA |
Darubini ya taasisi ya unajimu ya
Chuo Kikuu cha Hawaii cha Marekani imegundua sayari ndogo ya kipekee mwezi
uliopita, Sayari hii imepewa jina la Oumuamua, ambalo linamaanisha "mjumbe kutoka mbali"
katika lugha ya Kihawaii.
Hii ni mara ya kwanza kwa binadamu
kugundua sayari inayotoka nje ya mfumo wa jua, ukiacha zile sayari 9
zilizogundulika na zinazofahamika hadi wa hivi sasa, na kufanya idadi ya sayari
sasa kuzidi kuongezeka.
Lakini kuhusu picha za awali za
sayari hiyo mpya “Oumuamua” iliyogunduliwa,
haikuwezekana kukusanywa data za kutosha kwani ilikuwa tayari imeondoka katika
eneo lake la awali na hivyo bado juhudi zinaendelea kufanyika ili kutambua kama
sayari hiyo nayo inatumia mfumo (orbit)
unaotumiwa na sayari nyingine kulizunguka jua.
Lakini ajabu kubwa
hapa, Baada ya kugundua sayari hii watafiti wameichunguza kupitia darubini mbalimbali
zilizoko duniani kote, na Uchunguzi huo unaonesha kuwa sayari hiyo inazunguka
mara mmoja kila baada ya saa 7.3, na kiasi cha mwanga unaotolewa na sayari hiyo
pia kinabadilika kwa mara 10, Hali hii haijawahi kutokea kwenye sayari ndogo au
vimondo vya mfumo wa jua.
Mnajimu wa taasisi hiyo Karen J. Meech
amesema mabadiliko makubwa ya mwanga yanamaanisha kuwa sayari hii ni nyembamba
sana, ambayo ina kipenyo cha mita 400, na urefu wake huenda ni mara 10 ya
kipenyo chake.
Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA
inasema tarehe20 Novemba sayari hii ilikuwa umbali wa kilomita milioni200
kutoka dunia, na inatarajiwa kupita katika mzingo wa Jupiter mwezi Mei mwakani,
na itaondoka kwenye mzingo huo mwezi Januari mwaka 2019 na kuelekea kundi la nyota la Pegasus.
Ili kufahamu kuhusu Oumuamua pamoja na (Link) ambazo zitakupa uelewa Zaidi kwa muhusika anayezungumziwa ingia kwa kubofya kwenye neno husika lililopigiwa mstari.
SOURCE: http://swahili.cri.cn/
No comments:
Post a Comment