Thursday, 30 November 2017

USIYOYAJUA KUHUSU NDEGE WAHAMAO KUTOKA MABARA MENGINE KUJA AFRIKA AINA YA KORONGO.

Kila mwaka ifikapo tarehe 10/11 MEI ni siku ya (Destination Flyways; Migratory Birds) “maadhimisho ya ndege wahamao” Tanzania na duniani kiujumla, Yaliyoanza kuadhimishwa tokea mwaka2006. ambapo (TANAPA Tanzania) imekuwa ikiwataka wananchi wa tanzania kuendelea kutunza na kulinda maeneo yote ambayo ni mapitio ya ndege hao wahamao (Ardhi-Oevu-Ramsar), ambapo kama zilivyo nchi nyingine Tanzania ilisaini mkataba wa kuhifadhi maeneo yote ya Ardi-oevu mwaka2000.
 
Wapo aina nyingi sana za ndege wahamao (Aquatic birds) kutoka mabara mengine mbalimbali (Hasa Ulaya na Asia, kuja Afrika) na Miongoni mwa ndege hao ni pamoja na Heroe wadogo na Wakubwa (Flamingo-eng), pamoja na Korongo (Crane & Stock-Pichani) nk.
 
Uhamaji uho wa ndege hawa huweza kukabiliwa na vifo vya takribani robo ya ndege wote kufa, lakini kutokana na kuzaliana kwao kwa wingi hutoshea kuirudisha idadi yao baada ya muda mfupi.
Ambapo kuhamahama kwao huchagizwa na kutafuta malisho yao ambayo hupatikana zaidi maeneo ya mito (Yanapopatikana maji baridi) pamoja na kwenye eneo lenye umajimaji asilia ya Magadi (Ardhi-oevu), ambapo ndipo chakula chao na kirutubisho chao kikuu kwa ndege hawa kinakopatikana.
 
Kwa mfano wa sehemu hizo ni pamoja na Ziwa Natron lililoko Arusha, ambapo asilimia karibu (80%) ya ndege heroe (Lesser Flamingo) ndipo mazalia yao makuu duniani, huku wale wakubwa (Greater Flamingo) wakipatikana kwa wingi zaidi eneo la Ziwa Ndutu, Manyara nk. Huku ndege aina ya Korongo, wakifikilia maeneo hayohayo ikiwemo eneo la hifadhi ya Kilimanjaro.
 
SASA TUMWANGAZIE KORONGO:
 
 
Kuhusu manyoya yake:
 
KORONGO anapiga mabawa yake chini na kuruka juu. Kisha yeye huanza kujipinda-pinda akipaa bila juhudi yoyote kwa kusukumwa na upepo, Akibadili kidogo mwelekeo wa mabawa na mkia, ndege huyo huelea bila kupiga-piga mabawa yake.
 
Ni nini humwezesha kufanya hivyo kwa uwezo wa ajabu na kwa njia yenye kuvutia? Kinachomwezesha kufanya hivyo hasa ni manyoya yake.
 
Hakuna mnyama mwingine leo aliye na manyoya kama ya ndege. Ndege wengi wana manyoya ya aina tofauti-tofauti. Manyoya yanayoonekana kwa urahisi ni yale ya nje ambayo humfanya ndege awe na umbo laini linalomwezesha kupaa. Manyoya hayo yanatia ndani yale ya mabawa na ya mkia, yanayomwezesha ndege kuruka na kukatisha kona hewani.
 
Ndege mvumaji anaweza kuwa na manyoya ya nje 1,000 hivi, naye bata-maji zaidi ya 25,000.
 
Manyoya yamebuniwa kwa njia ya ajabu. Mhimili wa kati wa manyoya ambao unaitwa rachis unaweza kupindwa lakini ni imara sana. Vishina vya manyoya huota pande zote mbili za mhimili navyo kwa ujumla hutengeneza unyoya laini. Vishina hivyo huunganishwa kwa vitu vidogo vinavyoitwa barbule, na kufanyiza kitu kama zipu.
 
Ndege huunganisha sehemu hizo ndogo za manyoya yao wanapojisafisha. Wewe unaweza kufanya hivyo pia kwa kuvuta unyoya kati ya vidole vyako.
 
Pande mbili za manyoya ambayo hasa hutumiwa kwa kuruka hazilingani, yaani, upande wa mbele wa unyoya ni mwembamba kuliko upande wa nyuma. Muundo huo wa ajabu unafanya kila unyoya uwe kama bawa dogo. Pia ukiangalia chini ya mhimili utaona mfereji, ambapo Mfereji huo unasaidia mhimili uweze kujipinda bila kuvunjika.
 
ENDELEA HAPA: https://wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102007250
 
UWEZO WA KUONA WA NDEGE
 


Rangi za manyoya ya ndege huwapendeza sana wanadamu, Lakini inawezekana kwamba manyoya yanawapendeza ndege wenyewe hata zaidi ya wanadamu.
 
Ndege wengine wana aina nne za chembe za kuwawezesha kutambuana rangi, huku wanadamu wana aina tatu tu, Uwezo huo wa ziada huwasaidia ndege hao kuona miale ambayo wanadamu hawawezi kuiona.
 
Wanadamu huona kwamba ndege wa kiume na wa kike wa jamii fulani wanafanana, lakini manyoya ya ndege wa kiume hutokeza miale hiyo kwa njia tofauti na ya ndege wa kike, hivyo kuchagiza Ndege wenyewe kutambuana jamii yao na familia yao kiujumla kwa kupitia utofauti huo, na hilo limeelezwa kitaalamu kuwasaidia ndege hao kutambua wenzi wao au hata watoto.
 
NDEGE WAHAMAO:


 
Korongo akiwa ni miongoni mwa ndege wengine wahamao (Migratory birds), hupendelea kuishi zaidi sehemu zenye umajimaji au unyevunyevu msimu wote wa mwaka, na pia maeneo hayo pekee ndipo wapatapo vitoweo vyao, na hiyo ndio sababu kubwa inayowafanya kuhamahama mara kwa mara sehemu waliyopo kunapotokea mabadiliko ya hali ya hewa tofauti na waliyoizoea.

Ndege wengine wahamao ni pamoja na Penguins, Auks, Puffins, Ducks, Geese, Swans, Loons, Grebes, Herons, Egrets.
(Kwa kubofya kwenye Majina ya ndege hao, Mfano: “Penguins” utapelekwa kwenye picha ya ndege husika)
Mguu wa Korongo
 
Korongo haitaji viatu na wala hagandi hata akiwa amesimama miguu mitupu juu ya barafu au maji, swali ni kuwa je! Ndege huyu hudumishaje kiwango cha joto mwilini mwake?
Njia moja kuu ni kupitia mfumo wa kudumisha joto ulio miilini mwao, ambapo Mfumo huo wa kudumisha joto una mrija ulio na umajimaji wenye joto na mwingine ulio karibu na huo wenye umajimaji ya baridi.
Umajimaji kwenye mirija hiyo ukielekea upande mmoja ni nusu ya kiwango cha joto kitakachopitishwa, Lakini umajimaji ukielekea pande tofauti kiwango chote cha joto kitapitishwa.
Mfumo huo tata wa kudumisha joto mwilini mwa Ndege Korongo, unapunguza kiwango cha joto cha damu inayoelekea miguuni hadi karibu igande na kisha huipasha joto damu hiyo inaporudi katika mzunguko wake.
Mtaalamu wa ndege, Gary Ritchison, anaandika hivi kuhusu ndege wanaoishi katika maeneo yenye baridi: “Mfumo huo wa kudumisha joto hufanya kazi vizuri sana hivi kwamba wanadamu wameuiga katika ujenzi ili kuzuia kupoteza nishati.”
Je, mfumo huo wa kudumisha joto katika miguu ya korongo ulijitokeza wenyewe? Kama wanasayansi wanavyoamini kila kitu kilijifanyiza chenyewe (Theory) Au ni kwamba, ulibuniwa na aliyewaumba!?
 

No comments:

Post a Comment