Tuesday, 21 March 2017

FAIDA ZA MISITU HUKUTEGEMEA WEWE KUZILINDA

Moja ya miti iliyopandwa na Binadamu kwa ajili ya kurejesha halimisitu iliyopotea katika eneo hili. Picha Na Stewart Meena

Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti ya aina mbalimbali, mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu. lakini pia ipo misitu mingine ya Kupandikizwa na binadamu katika mazingira yaliyomzunguka na kwa muundo anaoutaka yeye mwenyewe (Artificial)

 https://sw.wikipedia.org/wiki/Msitu

Kila mwaka ifikapo Tarehe 21/03 ni siku ya Misitu duniani ambapo sambamba na maadhimisho hayo pia elimu hutolewa kuhusiana na utunzaji wa misitu asilia pamoja na ile ya kupandwa na Binadamu ili kurejesha Muingiliano mzuri kati ya binadamu na Mimea (Frora & Fauna)
Mtiririko wa Maji katika chemchem zitokazo ardhini kwenye misitu ya asilia. Na Stewart Meena
Hivyo basi palipo na utunzaji mzuri wa  Uoto wa Asili, hua ndio chanzo kizuri zaidi cha maji safi na salama pamoja na hewa safi kwa ajili ya kuendeleza maisha ya mwanadamu ambaye hutegemea mimea hiyo kujipatia hewa ya (oxigen) ambayo huibadilisha na ile waitoayo ya (Cabondioxide) ambayo hufyonzwa na Mimea.

Pasipo mimea hakuna mvua, kutokana na mzunguko mzima wa kuvukiza Maji kwenda angani, na kisha tena kurejea Ardhini, hutegemea sana misitu hii kuvuta mvua hiyo.
Kuanza kufunga kwa mawingu ikiwa kama ishara ya kutaka kunyesha kwa Mvua. Na Stewart Meena
Misitu hii huzua pia uharibifu wa Upepo mkali, mvua nyingi kwa kutunza mmomonyoko wa udongo unaoweza kupelekea majanga makubwa zaidi kama ukame, pamoja na vifo viwezavyo kutokana na mabaa ya njaa kwa ukosefu wa chakula.

TUNZA MISITU IKUTUNZE

No comments:

Post a Comment