Thursday, 8 November 2018

UKWELI USIOUJUA KUHUSU RADI (THUNDER STORM) NA CHANZO CHAKE (LIGHTNING)



Na Stewart Meena

Radi hutokana na mvutano wa hali ya hewa kinzani katika tabaka la juu la mawingu ambapo ukinzani huo huchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa, mgando wa barafu “kuganda na kuyeyuka” matone ya mvua pamoja na mwendokasi wa mzunguko wadunia “kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake (rotation) na kuzunguka jua (revolution) pamoja na sayari nyingine.
Kimsingi katika dunia yetu ambayo ni sayari ya3, kumegawanyika karibu matabaka 4 ya mawingu, ambapo tabaka la juu kabisa hujulikana kama (stratosphere) na eneo la kwanza la tabaka hilo, hutafsiriwa kama mwisho wa upeo wa macho yetu kwa kuangalia angani, ambapo eneo hilo sio eneo la mawangu halisi.

Eneo unapoona rangi ya bluu na nyeupe hapa ndipo mwanzo wa mzalisho wa mawingu yenye barafu katika tabaka la pili la juu yake ambalo hilo ndilo husababisha mvua kunyesha pindi barafu inapoyeyuka kwa joto kupenya eneo hilo.
Eneo hili la kwanza sio mawingu halisi isipokuwa ni msafirisho wa mvuke na ukungu (fogs) unaozalishwa kwa baridi kuendelea kuzidi kwani kwa kadiri unavyopanda juu kutoka usawa wa bahari ndipo ongezeko la baridi linapotokea kwa wale waliobahatika kupanda mlima kama Kilimanjaro ukiwa karibia kileleni ukiangalia chini huwezi kuona villivyopo chini badala yake utaona ukungu huo mweupe unaotanda eneo hilo, na hii ndio sababu maeneo yote ya uwanda wa juu kaskazini na kusini kwa Tanzania yetu kunakuwa na baridi kali muda wote wa mwaka kutokana na mwinuko wao kutoka usawa wa bahari. Mfano:Iiringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Lushoto-Tanga nk.

Mvutano wa hewa nayozungumzia ni hewa inayopatikana eneo la chini ya tabaka la kwanza la mawingu (sehemu tuliyopo) inayoitwa ‘oxygen’ itolewayo na mimea na ile ya ‘carbon-dioxide’ tuitowayo wanadamu na wanyama wengine, na ile inayopatikana tabaka la juu la mawingu naitrojeni ‘nitrogen’ hizi huweza kuchagiza tabia tofauti ya hali ya hewa katika tabaka hilo la kati na la juu la mawingu na hata eneo tulilopo la ardhi na lile la chini kabisa ya ardhi.
Na hapo ndipo huwa chanzo cha kuzaliwa kwa nishati ya radi, uwepo wa tufani kadhaa duniani kama vile vimbunga na zile za baharini, uwepo wa tetemeko la ardhi ikisababishwa na kusafiri kwa volkaniki (volcano) chini ya ardhi n.k

TUNAPOSEMA RADI NDIO NINI, NA KWANINI HULETA MADHARA DUNIANI?

Radi (thunder) sio muungurumo, kama wengi mnavyodhani ila radi ni mwale wa kama shoti ya umeme unaotokea kabla ya muungurumo na baada ya muungurumo kupita; mwale huo ni nguvu kama nishati ya umeme ambao huu huwa na vipimo-nishati zaidi ya umeme (voltage & watts) ambayo hii huwa na kiasi cha Vol. zaidi ya elfu-10 ukilinganisha na ile ya umeme inayoanzia (vol.110/220-1000)
Kama tulivyoona mwanzo kwanini radi hutukia, lakini bado watu huwa na maswali mengi kwanini mara kadhaa imekuwa ikileta madhara kwa kupiga miti’ nyumba na watu wakati mwingine, hivyo kuhusisha radi hiyo na imani za kishirikina pamoja na kuvaa aina ya mavazi.

KUNA UHUSIANO GANI:
Kitaalamu hakuna uhusiano wa radi na imani za kishirikina isipokuwa kuna mazingira yanayoweza kuifanya radi kupenya kwenye mawingu na kushuka moja kwa moja aridhini na kuleta madhara mahala ilipofikia (gravitation area).
Radi huambatana na mvua na mvutano wa nishati kama ya msumaku, na endapo ikitokea ikawa inasafiri angani na kukawa kunauvutano wowote wa mfumo wa nishati kama ya umeme, umande umande wa barafu na mazingira ya mvua huweza kupiga na kushuka hadi eneo hilo.


Ndio maana nyumba zenye umeme huekewa chuma flani ya rangi ya shaba na kuchimbiwa ardhini ili kuzuia radi hiyo kuwa na uwezekeno mkubwa wa kuipiga nyumba hiyo, na hivyo ni hatari zaidi kutumia umeme wa moja kwa moja pasipo kuweka kizuizi hicho kwasababu nishati ya radi huwa ni mara maelfu zaidi ya umeme wa kawaida

Na inapotokea radi hiyo kupiga basi tambua kuna mvutano uliopo katika eneo hilo, mvutano ambao huivuta nishati ya radi na kuileta hadi aridhini na kisha kuleta madhara kwenye eneo husika palipo na kani mvutano huo (gravitation).


Kuna uhusiano mkubwa sana uliopo kati ya nishati umeme wa radi na umeme wa majumbani, Uvutano wa sumaku, mvukizo wa joto la ardhi haswa maji yanaponyweshwa juu yake; na uwepo maji haswa yale ya mvua pamoja na yale ya bomba na aina ya nyenzo yanayopitia (mipira au chuma) wakati radi ikipiga.
Mabomba yaliyotengenezwa kwa chuma cha zinki, aluminium na shaba, hupitisha umeme na hivyo kwa kuwa maji hupita ndani yake, na ukayatumia wakati radi ikipiga kuna uhatarisho; lakini yale yaliyotengenezwa kwa mipira huwezi kuwepo kwenye uhatarishi ukilinganisha na hizo nlizozitaja.

MAVAZI:
Kuhusu mavazi hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kupigwa na radi na aina ya mavazi tunayoyavaa (Mfano watu husema ukivaa mavazi mekundu ni rahisi zaidi kupigwa na radi kweli?) Jibu ni kuwa sio kweli.!

Isipokuwa mavazi tunayoyavaa na tabia ya hali ya hewa kwa wakati huo, kwa kushirikiana huweza kuleta uwezekano huo kwa kufuata tabia ya miale ya radi inavyosafiri pekee na eneo ulilopo wakati huo kama ilivyo kwa tabia za vyanzo vya nishati nyingine kama jua na moto.
  • Mfano kivizikia (Physics): Jua hutufikia kwa njia a mnururisho;

  • Umeme au moto husafiri kwa njia ya mpitisho;
Hivyo katika mavazi nayo huwa na tabia yake katika kuakisi na kuvuta miale hiyo ya nguvu za sumaku, nishati ya jua, moto na nguvu nyingine za nishati ya umeme kama ilivyo kwa radi.

Mfano: mavazi meusi husharabu moto, joto au nishati ya jua;
Maazi meupe huakisi hali hiyo apo juu.

Mavazi mengine kama ‘Mekundu, Njano, Zambarau nk’ hayaakisi wala kusharabu nguvu hizo za nishati isipokuwa haya huwa na uwezo wa kutunza joto hilo kwa muda flani, na ndio maana katika uvutano wa sumaku mavazi haya na yale yenye asili ya unailoni au mipira huweza kuzalisha miale mfano wa cheche za moto ambazo hizi hutoa muangaza.
(Fanya zoezi moja: Chukua moja ya mavazi hayo, kasha yavae mwilini au yasugulie kwenye nywele zao kisha yafikiche yenyewe kwa yenyewe gizani usiku utaona yakitoa miale hiyo mfano wa cheche)

NINI KINATOKEA HAPO MTU KUPIGWA NA RADI NA UNAWEZA KUJIKINGAJE!:

Kwa utangulizi nilioueleza katika tafiti na makala yangu hapo juu: Imeelezwa kitaalamu kuwa radi huambatana na nishati nyingine duniani, na kuna uhusiano mkubwa sana kati yake na mvua/maji; uvutano wa sumaku na hali-joto ya mahali haswa ardhi wakati radi inapiga pamoja na mwingiliano wa hewa tofauti inayochagizwa na kujizungusha kwa dunia katika mhimili wake (Rotation) na kulizunguka jua (Revolution).
KUJIEPUSHA: usipende kukaa chini ya miti wakati mvua inanyesha na huku ukiwa umevaa mavazi yoyote yenye uwezo wa kutengeneza Usumaku yanapogusana (rejea kwenye mavazi juu); kuweka kizua radi majumbani unapofunga umeme lakini usipende kusikiliza redio au kutumia internet ukiwa kwenye eneo la mwinuko na penye umande umande au chini ya miti wakati mvua ninanyesha.

Unashauriwa kuepuka kutumia maji kwenye mabomba yasiyo ya mpira wakati radi inasafiri, kuoga wakati huo nk; lakini pia ni vyema ukapunguza matumizi makubwa ya vifaa vinavyotumia umeme wakati huo kama vile kuwasha Tvs, Radio, kutumia pasi na Heater kupikia au kuchemshia maji kuchaji simu kwa wakati mmoja.
MWISHO: radi ni mwale ule unaoonekana kabla ya muungurumo kusikika, na muungurumo huo huzalishwa kutokana na nguvu za radi hiyo (mwale) na mgandamizo wa barafu (Mawingu mazito yaliyoganda na matone ya mvua kugusa eneo hilo kutoka tabaka la juu zaidi la mawingu) msuguano wa hali za hewa kinzani.

Tahadhari: Radi ni kama ilivyo kwa nishati ya umeme, na huweza kuleta maafa kwa kuwakisha moto au kumuunguza muhusika, usikae karibu na nyaya za umeme (haswa unaosafirisha voltage kubwa) wakati mvua zinanyesha au radi kupiga.
JIFUNZE ZAIDI NAMNA GANI EATH-QUAKE NA THUNDER STORM’ HUTOKEA KWA KUBOFYA VISAIDIZI HAPA CHINI NA VILIVYO NA RANGI BLUU JUU:

Radi

Tetemeko la Ardhi

Thursday, 31 May 2018

MAAJABU! ZIFAHAMU NCHI-12 AMBAZO ZINAONGOZA KWA UPUNGUFU WA JINSIA YA KIKE KATIKA NDOA.!




Idadi ya wingi na uwiano wa jinsia ya kiume na jinsia ya kike duniani inazidi kutofautiana sana nah ii ikichagizwa na jeografia na historia ya eneo husika, katika rika zote kwa jinsia hizi mbili.
Leo hii, utofauti wa uwiano huo umeingia hadi katika maswala ya mahusiano, ingawa idadi ya mabinti na vijana walio-wapweke (Yaani-single) ikibakia kufanana isipokuwa kuna baadhi ya nchi nyingine hali ni mbaya sana kutokana na vijana au mabinti wengi waliofikisha rika la kuoa au kuolewa wakikosa watu wa kuwaoa kabisa.
Hiyo inasababishwa na nini?

Kwa tafiti zilizofanyika kwenye baadhi ya nchi hizo imebainisha kuwa, ukatili wa kijinsia kwa Wanawake, matukio ya vita vya wenyewe mara kwa mara, kutafuta nafasi nzuri za kazi na umaskini uliokithiri ndio hupelekea watu hasa Mabinti kuhama-hama au kutafuta makao sehemu nyingine salama zaidi kwao, na hivyo katika maeneo waliyotoka kubakia na Upungufu huo mkubwa wa kupata wachumba wa kufunga nao pingu za maisha (ndoa).

Kwa mfano: Nchini Tanzania, tazizo hili lipo zaidi kwa wanawake (Mabinti) kukosa Wanaume waliotayari kuwachumbia na kufunga nao ndoa, ambapo –
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2016, Tanzania inakadiriwa kuwa na wakaazi zaidi ya milioni 47, ikipanda kutoka milioni 45 kwa mwaka 2005, na kati ya idadi hiyo wanaume ni robo ya wanawake wote Tanzania.
Hii inamaanisha kuwa idadi ya (wanawake) au jinsia ya kike kwa tanzania ya leo imeiizidi idadi ya (wanaume) jinsia ya kiume kwa zaidi ya asilimia 35%, ambapo kwa hesabu za haraka haraka inabidi kila mwanaume awe na wake wa3 ili kufidia (gape) uwazi huo uliopo.

Sasa wakati hapa kwetu Tanzania idadi ya wanaume ndio ndogo kulinganisha na wanawake, kwa nchi za wenzetu mambo ni tofauti kabisa, na idadi ya wanawake ni robo ya wanaume wote kwenye nchi hizo ambapo asilimia 72% ndio wanaume na asilimia 28% ndio wanawake.

Kwa mfano huo, Na kwa sababu hizo basi, tofauti na ilivyo kwa Tanzania mabinti wakikosa wanaume waku-waoa, hii hapa orodha nyingine kabisa ya baadhi ya (Nchi-12) zinazoongoza duniani kwa kuwa na upungufu wa wanawake na sio Wanaume kiasi kwamba pindi mtoto anapozaliwa huwekewa (oder) na wazazi wenye mtoto wa kiume kwa minajili ya kuchukua jiko katika nyumba hiyo kwa siku za baadaye pindi watoto wao watakapokua kwa kuwa Vijana wao wanakabiliwa na tatizo la kukosa au kuwa na wakati mgumu kupata wenzi wao wa maisha.
Qatar




Nchi ya Qatar iliyopo katika nchi za kiarabu ni miongoni wa nchi ambazo kuna upungufu wa mabinti, na kushikilia rekodi hiyo kwa muda mrefu kwa sasa. Sababu kubwa ya upungufu huo ni pamoja na taratibu na sheria ya nchi hiyo inayozingatia maadili ya kiislamu zaidi na hivyo kutopendelewa zaidi na mabinti na raia wengine kuingia nchini humo, ikichagizwa na serikali ya nchi hiyo kutotoa visa kwa (Jinsia ya kike) wa mataifa wengine ispokuwa Uingereza na Canada pekee.

Sababu nyingine kubwa ni uzalianaji duni, tokea pale wanaume (karibu-94%) huihama nchi yao na kwenda kufanya kazi mataifa mengine ya kigeni kiasi ya kwamba serikali ya Qatar kwa sasa ikawalazimu kutoa nafasi za wahamiaji na kuwapatia kibali maalumu (Visa) ili kuziba upungufu huo wa nguvukazi taifa waliohama makwao kwa ajili ya kutaka kuinua uchumi wan chi hiyo.

Uwiano (ratio) kati ya wanaume na wanawake kwa nchi hii iliyo mashariki ya kati na iliyo tajiri kwa uzalishaji wa mafuta ni 3.41 to – 1.54.
United Arab Emirates (UAE)


 

Hadi kufikia karne ya (20th-century), UAE ilikuwa na upungufu wa karibu watu 40,000 kwa raia wazawa, huku wanawake pekee wakiwa 22,000, hiyo ikitokana na raia wake kuhama nchi hiyo na kwenda nchi jirani kutafuta maisha kabla ya kugundulika kwa mafuta, ambapo kidogo kwasasa idadi ya wakazi wake imeongezeka kidogo, huku wengi (85%) wakiwa sio raia wa nchi hiyo bali wapo hapo kula maisha. Wengi mtakubaliana na mimi kwa kufanya utafiti mdogo tu wa wakaazi wa dubai, kwa kuangalia wazawa na wale wasio wazawa.

Lakini katika kuongezeka huko bado uwiano baina ya wanaume na wanawake sio sawa, ambapo kwasasa inawalazimu wanaume wan chi hiyo kwenda nchi nyingine za kiarabu kutafuta wachumba huko.

UAE pato lake kubwa hutokana na Mafuta na Utalii, kwa wageni kutoka mataifa mbalimbali kwenda nchini humo kula bata.
India


India inashika nafasi ya 3 kuwa na upungufu wa mabinti duniani, ingawa tunaweza kusema inashika nafasi ya3 duniani kwasasa kwakuwa na watu wengi ukiacha China na Marekani, huku idadi ya raia wake ikikisiwa kuzipita China na USA na kushika nafasi ya kwanza ifikapo mwaka2024. lakini wengi wa watu hao bado wanaume ndio wengi.

Kwa muda sasa na kwa mila na desturi za nchi hiyo, Mabinti ndio wamekuwa wakitoa mahari ili kumposa Kijana, hii imekaa vipi? Ndio tuseme unafikiria kuwa wanaume ndio adimu! Hapana.

Uwiano uliopo kwasasa kati ya wanaume na wanawake nchini humo ni asilimia karibu 1.08 ya kila mwanaume kwa mwanamke mmoja, yaani sawa na tuseme kila mwanamke wa india awe na wanaume 5 kuleta uwiano sawa.

Ukilinganisha na nchi za (G-20) na ikiwa miongoni,  India kwasasa inapiga hatua kimaendeleo zaidi duniani ingawa bado kuna changamoto za wanandugu kuendelea kushikamana pamoja, wazee wakiwa wengi kuliko nguvu kazi ambapo ni vijana na hivo wanaume wenye uwezo kidogo kuwasaidia wazazi na ndugu zake wote.

Sababu kubwa ya upungufu huo haijawekwa bayana lakini watafiti wanaamini kuwa Wanaume wa nchi hiyo huwa na bahati sana ya kupata watoto wa kiume kuliko wa kike, hivyo familia moja yenye watoto 7, wakike ni wawili tu pekee.
China


China inashika nafasi ya 4 kwa upungufu wa wanawake kwa hivi sasa licha ya kuwa inaongoza duniani kwa kuwa na watu wengi zaidi, Idadi Wanaume kwa nchi hiyo kwasasa ni karibu (40-million) zaidi ukilinganisha na wanawake robotatu ya hiyo, yaani sawa na tuseme kila Mwanamke atatakiwa awe na wanaume3 ili kuweka uwiano sawia.

Upungufu huo umechagizwa na sheria ya muda mrefu ya nchi hiyo, kuwa shurti wazazi wawe na watoto2 pekee ili kupunguza ongezeko la watu nchini humo, hatua iliyowanya wazazi kuzingatia uzazi wa mpango.
Lakini sasa hasara yake ni kuwa, Wazazi wengi walipendelea  kupata watoto wa kiume zaidi, kw imani kuwa wao ndio watakao kuwa Warithi na hivyo pindi mimba ilipopatikana ya mtoto wa kike ilitolewa.

Hivyo, ubaguzi wa jinsia ya watoto, utoaji wa mimba ya mtoto wa kike na sheria ya serikali ya kuzaa watoto wawili pekee ikizidi wa3 ndio imepunguza idadi ya mabinti nchini humo.
Greece

Nchi ya 5 ni ugiriki, ambapo katika nchi hii nako kuna upungufu wa Wanawake ukilinganisha na nchi nyingine, chanzo kikuu cha kushuka idadi ya wanawake wa eneo hilo hutokana na kuhama kwa mabinti wengi kwenda nchi nyingine za ulaya na huko hukaa muda mrefu na kuanzisha familia zao hukohuko.
Tatizo kubwa linalofanya uhamaji huo ni kutokana na kutokuwepo kwa usawa kati ya ujira na nafasi za kazi baina ya wanaume na wanawake na hivyo wanaume pekee ndio huonekana kupewa kipaumbele zaidi kuanzia ngazi ya familia hadi ya taifa.

Idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo sio wazawa huku karibia robo yao ni wahamiaji ambao nao ni wanaume kutoka mataifa mengine, zaidi ya hapo nchi hii ndio njia kuu na kimbilio zaidi kwa wahamiaji wanaotaka kwenda barani ulaya hasa kwa nchi za uingereza na ufaransa.

Nigeria



Nchi ya Nigeria inashikilia nafasi ya6, kwa kuwa na upungufu wa wanawake ukilinganisha na idadi ya wanaume wa nchi hiyo, Wanaume hukadiriwa kufikia (ratio) 1.04 na Wanawake 1.0 Sababu kubwa ya upungufu huo huchagizwa na mabinti wenyewe kutoroka makwao kutokana na kukithiri na kuendelezwa kwa mila za ukeketaji kwa mabinti (FGM), Mabinti kulazimishwa kuolewa wakiwa katika umri mdogo (Forced marriage) Kurithishana wanawake baada ya mume kufariki, na hivyo mabinti wanaofikia rika la kuvunja ungo, hulazimika kutorokea sehemu nyingine ambapo watapata maisha yaliyosalama zaidi kwao, pamoja na machafuko ya waasi (Boko Haramu) na serikali ya nchi hiyo kuwania eneo lenye utajiri wa mafuta.

Mwaka jana serikali ya Nigeria ilitangaza kuwepo kwa upungufu huo endelefu wa mabinti kupatikana kuolewa, na hivyo kuacha idadi kubwa ya vijana wanaotafuta wake wa kuwaoa kubakia mabachela (Ukapera).
Afghanistan


Nchi hii inashikilia nafasi ya 7 kwa upungufu huo wa mabinti kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa sasa, lakini pia (Sharia) au sheria kali zinazoelemea maadili ya ki-Islam, kwa kutokuwaruhusu mabinti kuwa na sauti mbele ya wanaume.

Matukio ya ubakaji unaofanywa na wanamgambo waliojitenga na serikali (Al- Quaeda) nao umechagiza eneo hili kutokuwa salama zaidi kwa jinsia ya kike na watoto, na hivyo wengi wa mabinti wa nchi hiyo hutorokea nchi jirani kuanzisha familia zao huko huku wanaume wakisalia kupambana vita vyao wenyewe kwa wenyewe.

Sweden



Inashikilia nafasi ya 8, kwa upungufu huo na hiyo hutokana na uhaba wa makazi kuwatosheleza familia nzima na wananchi wote wa Sweden, tatizo hilo pia limechagizwa na ukaribu uliokuwepo kwa nchi marafiki wa nchi hiyo hasa jumuia ya ulaya kuwa ndio kimbilio la mabinti wa nchi hiyo wanaosifika kuwa na urembo mkubwa.

Karibu kiasi cha watu takribani 35,000 ambao ni wakimbizi kutoka mataifa yanayokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe (war-torn countries) huishi nchini humo na hivyo kupelekea mchangamano wa wazawa na wageni kuzalisha upungufu mpya wa mabinti kuolewa na wenyeji.
Egypt


Misri ikiwa ndio nchi inayoongoza barani Afrika kwa kuwa na wingi wa watu na ikishika nafasi ya nne kwa Duniani, lakini nayo inashikilia nafasi ya9, kwa uhaba wa mabinti ukilinganisha na idadi ya Vijana (kiume) wote katika nchi.


Wastani uliopungufu kwa sasa unakadiriwa kuwa kati ya (1-ratio) wa Wanawake, huku idadi ya wanaume ikiwazidi kwa (1.7-ratio) kiasi ambacho kinapelekea kutokuwa na usawa kwa idadi ya jinsia zote mbili.
Chanzo kikuu cha upungufu huo wa mabinti ni pamoja na, jinsia hiyo kuwa bize zaidi na kazi mbalimbali maofisini kiasi kwamba hujikuta wamepitiliza muda wao wa kuwa na familia stahiki, lakini pia kama hutambui mabinti wengi wa misri ndio wasomi wenye shahada za juu kabisa kuhusu maswala ya sheria, madawa na sheria hivyo hujikuta wakihama au kuhamishwa kwa wingi zaidi kwenda kuhudumu katika vitengo hivyo kwa nchi nyingine zilizoendelea kama Ulaya na Uarabuni.
“A large portion of female Egyptians have advanced degrees and aspire to work in the fields of science, medicine, and law, As a result, a lot of them have been immigrating to more progressive countries, This has left a lot of Egyptian guys with lonely heat”

Libya

Libya inashikilia nafasi ya10 duniani kwa upungufu huo wa mabinti wenye rika la kuolewa ukilinganisha na idadi na mahitajio ya wanaume wa nchi hiyo waliowazidi kwa wastani (ratio) wa0.7; yaani sawa na kusema kila mwanamke mmoja anatakiwa awe na wanaume5 ili kuleta uwiano huo sawa.


Nchi ya Libya imeingia katika nafasi hii kutokana na mapambano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoendelea kwa muda mrefu tokea enzi za Rais Ghaddaf hadi kifo chake, na hivyo wanaume wengi wa nchi hiyo huchukuliwa kama wapambanaji na wengi miongoni mwao walifia vitani, hivyo kupelekea uchache wao na kuwa na idadi kubwa ya wanawake walio wapweke ukilinganisha na idadi ya wanaume.
Iceland


Kisiwa hiki kinashikilia nafasi ya11 Duniani kwa kuwa na upungufu wa kupatikana kwa mabinti wa kuweza kuolewa.


Unapofikiria kuhusu nchi ya Iceland, jambo moja kubwa huja kwenye mawazo yako kwamba ni nchi iliyozungukwa au kutawaliwa na barafu (baridi) katika muda wote wa mwaka (ingawa sivyo), lakini pia ukweli uliopo kwa sasa ni nchi mojawapo yenye idadi kubwa ya wanume ukilinganisha na wanawake waliopo, utofauti wa kiasi cha (1.7%) na hivyo kuwafanya vijana kuwa wapweke wakikosa mabinti wa kuoa, na kulazimika kutoka nje ya nchi yao kutafuta wachumba.
Kuliwahi kuwa na uvumi na tetesi kuwa, serikali ya nchi hiyo ilitoa ofa kwa mabinti wa nchi nyingine waliotayari kuolewa na wanaume wa nchi hiyo kiasi cha dola za kiMarekani ($5,000) kwa usiri mkubwa, ingawa Habari hizo ziliposambaa serekali ya nchi hiyo ikajitokeza na kukanusha vikali tetesi hizo na kusema sio za kweli. (Sawaa, kazi kwenu mabinti wa kitanzania, unaweza kuchangamkia fursa hizi – Hahaha, natania..)

Philippines


Ufilipino ikiwa ni nchi iliyo maskini zaidi kwa nchi za ukanda wa nchi za bahari ya Pasific, inashikilia nafasi ya12 kwa kuwa na Uhaba huo wa wanawake wakuweza kuolewa, kutokana na kuwa
Mabinti wa kiFilipino huihama nchi yao kwa minajili ya kutafuta kazi nje ya nchi yao haswaa maeneo ya Australia, Asia na hadi kwenye nchi za Mashariki ya kati.
Matokeo yake sasa, kuondoka kwao huko hupelekea upungufu wa karibu wastani unaofikia  (1.02% to 1) na kw takwimu za hivi karibuni zinaonyesha idadi ya wenzi kufunga ndoa imekuwa kipungua siku baada ya siku, na kuweka ukweli juu ya upungufu huu kuwa idadi ya wanawake imepungua.

SOURCE: Difficulties2GetWife

Sunday, 27 May 2018

FAINALI UEFA, MADRID AMERUDISHA HESHIMA ALIYOTAKA KUIPOTEZA


HAYAWI HAYAWI HATIMAYE YAMEKUA: Uefa FAINALI usiku wa kuamkia Leo, Ni Madrid tena amenyakua ndoo hiyo ya UEFA na kumfanya kuwa (UN-STOPABLE) Kwenye Michuano hiyo mikubwa Barani Ulaya.

Lengo la kurudi kuandika hapa sio kufurahia Liverpool kutolewa kwa kufungwa mabao 3-1, wala sio kwa kitendo cha Mo-Salaa kulazimishwa kutoka nje ya uwanja kwa maumivu ya kuumia Mkono, kitendo kilichomfanya abubujikwe na machozi.

Ila naandika Makala haya tena kukumbushia Makala yangu iliyopita wakati timu takribani nne (4) zilipofuzu kuingia hatua ya Nusu fainali na Nikasemaa:

MADRID ANASTAHILI HESHIMA JAPO KIDOGO, NA HII NI MARA BAADA YA KUTINGA HATUA YA NUSU FAINALI KWA UTATA KIDOGO KUTOKANA NA PENATI YA BAO LA USHINDI KUWAVUSHA:
Rudia Hapa Mwenyewe: Mbabe Uefa-2018

NITOE TU KONGOLE KWA MADRID NA MASHABIKI WAKE WOTE DUNIANI KWA KUENDELEA KUITAWALA MICHUANO HIYO YA UEFA:

Thursday, 24 May 2018

KWANINI USUMBULIWE NA MBU WAKATI NJIA YA ASILI YA KWAFUKUZA UNAYO.?


FAIDA MPYA YA MMEA WA MCHAICHAI....
Imeelezwa kitaalamu kuwa: Ukitaka kuwafukuza Mbu wanaoleta ugonjwa wa Malaria nyumbani kwako, basi panda Mmea wa Mchaichai au weka huo Mmea
ndani ya nyumba yako kama pambo basi Mbu hawata sogea kabisa nyumbani kwako na utakuwa umewathibiti Mbu hao wanaoeneza ugonjwa wa malaria.
Kiufupi ni kuwa, Mbu wanauchukia sana Mmea huu wa Mchaichai kiasi kwamba huyakimbia mazingira uliopo, kama vile tu wajifichapo pindi taa ikiwa imewashwa.
Lakini mbali na faida kubwa hii ya mchaichai, lakini una faida nyingine lukuki katika kuulinda mwili thidi ya maradhi mbalimbali pindi utumiwapo kama kinywaji (Yaani kupikia katika chai) kama ifuataavyo.


FAIDA YA KUTUMIA MCHAICHAI KAMA TIBA NA CHAKULA

Faida za mchachai zipo nyingi sana wengi wetu hudhani mchaichai ni kuongo cha kuweka kwenye chai pekee, au ni dawa kwa ajili ya kuua mbu pekee, ila mchaichai huwa na faida lukuki zaidi ya hizo tu. Naomba uweze kusoma makala haya ili uone faida nyinginezo za mchaichai.

Zifuatazo ni faida za kutumia mchaichai kiafya.

1. Mchaichai ni kinga dhidi ya saratani.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha
sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani.

2. Hutibu magonjwa ya kuhara.
Husaidia umeng’enyaji wa chakula Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi.

Hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini Katika matibabu, unatibu magonjwa mengi ikiwemo kushusha joto, hasa kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na malaria kali.

3. Husaidia kusafisha figo na mkojo.
Mchaichai pia una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu mwilini, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali kiwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.

Figo inapokuwa safi na imara, hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika kirahisi kwani mkojo unapozidi kuwa mchafu mtu hujikuta akivimba mwili na wakati mwingine kufikia hata hatua ya kupoteza maisha.

4. Hupunguza maumivu wakati wa hedhi.
Mchaichai pia huwasaidia kina mama ambao wanaumwa na tumbo kipindi cha hedhi, ambao wengi wao huchukulia kama chango.

“Unapokunywa mchaichai, unawezesha kusafisha mirija ya uzazi na hivyo kuwezesha damu kupita kwa urahisi,”

5. Mchaichai hutibu vidonda vya tumbo na kupunguza kiwango cha gesi tumboni.
Hata hivyo kwa wagonjwa wanaosumbuliwa hasa na vidonda vya tumbo, mchaichai husaidia kuondoa gesi ambazo huwapata mara kwa mara.

Unachotakiwa kufanya ni ;
Kuendelea kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara.

Sunday, 20 May 2018

ZIFAHAMU FAIDA NYINGI TOFAUTI ZA ULAJI WA MATANGO KATIKA MWILI WAKO



 

HEBU LEO TUANGAZIE KUHUSIANA NA MATANGO:
Watu wengi tunapenda kula baadhi ya matunda flani tu, labda kutokana na ladha yake na kuyabagua mengine kutokana na kutokuwa na ladha unayoihitaji, haswa wengi mkipenda ladha yenye utamu-utamu.
Lakini hasara zake kuna baadhi ya vitamin na faida lukuki unazikosa kwa kutokula baadhi ya matunda mengine ambayo haya hauyapendelei kuyala kutokana na uchachu wake, au kutoyazoea katika milo yako ya kila siku.

Katika makala ya leo, Hebu tuangazie faida za kula matango (Tango),

TANGO: Asili ya kilimo cha matango inaaminika kuwa ilianzia kaskazini magharibi mwa India ambako yamekuwa yakilimwa kwa zaidi ya miaka thelathini sasa, Hata hivyo kwa sasa, matango, hustawishwa katika sehemu nyingi za kitropiki.
Matunda yake hukatwa katwa na kuliwa kama achali, au kachumbari, au huwekwa kwenye siki na pia hupikwa na kuliwa.
Katika nchi yetu ya Tanzania matango hulimwa kwa wingi katika mikoa mbalimbali kama vile: Tanga, Morogoro, Mbeya, Lindi, Mtwara na Pwani ambako kuna jua la kutosha, na Pia mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kilimo cha matango hukubali vilevile.
Tango (cucumber in English) ni zao muhimu katika mazao ya mboga na matunda nchini Tanzania na hata nje ya Tanzania, kwani licha ya kuwa ni zao la biashara pia ni zao la chakula.
Hili ni tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa mlo, na kama ilivyo kwa mboga kuwa muhimu kwa afya ya binadamu, Ndivyo Matango nayo yana faida nyingi mbalimbali kw mlaji.
Kwa mkulima hulifahamu vyema Tango. Ikiwa Tunda hili huwa na umbo refu hadi kufikia sm 15, na Matunda yake hukatwakatwa na kuliwa kama achali au kachumbari, pia huweza kuwekwa kwenye siki au kupikwa na kuliwa.
Ukuzaji wa matango huwa njia ya kuongeza mapato kwa mkulima na kwa muda mfupi sana, pia husadia kurutubisha ardhi kwa majani yake na mizizi yake kama ilivyo kwa mkunde.
FAIDA YA KULA MATANGO KWA BINADAMU:
1-KUONDOA HARUFU MDOMONI

Matango huondoa bakteria zinazofanya mdomo kunuka. Ili jambo hili litendeke unafaa kukata pande ya matango na kuweka mdomoni kwa dakika zisizopungua tano ukiwa umekaa kimya (Pasipo kuongea) ili iweze kutenda kazi au kuksaidia. Unafaa kuruda jambo hili mara tatu kila siku.

Mbali na kuswaki, Madaktari husema kuwa, Ulaji wa matango husaidia kuodoa joto jingi tumboni ambayo hua ndio sababu kuu ya mdomo kuwa na harufu hiyo mbaya.

2- KUPUNGUZA MAWAZO
Watu ambao hutumia mafikira sana katika kazi zao, hushauriwa kula matango kila siku kwani yana vitamini B, pamoja na B7, B5, B1 ambazo kwa pamoja hizo husaidia kupunguza mawazo mengi au (stress)

Na kwa Watumiaji wa pombe, au wanaofanya kazi nzito (za kutumia nguvu zaidi) huweza kuondoa hangover kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.

3- HUSAIDIA KATIKA UREMBO
Matango husaidia kulainisha ngozi ya mwili, kwa kina dada Unapokula matango nywele zako hupunguza kukatika, kuwa na afya bora na huweza kumea kwa haraka, Lakini pia matango hutumika kuondoa umbo la duara ambalo hupatikana machoni, kuondoa macho mekundu na kuwa meupe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.
 
(unafaa kufunga macho na kuekelea kipande cha tango juu yake kisha kusubiri kwa masaa kadhaa kila siku au waweza kuyafunga machoni usiku na kulala nayo hadi asubuhi kwa siku kadhaa – matokeo utayapata)
 
Unaweza kuyaponda matango na kupaka usoni, kisha kuacha kwa dakika ishirini ili kulainisha uso na baadaye kuosha uso, jaribu utajivunia sasa.
 
4- HUTUMIKA KUONDOA SUMU MWILINI (Tango ni chanzo kizuri cha maji navitamin B
 
Tango huupa mwili maji ya kutosha na vitamin B zote. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.
 
Unaweza kutengeneza kinywaji cha matango na matunda mengine kwa kuchanganya na mboga au matunda mengine kama limau na machungwa ili kuondoa sumu ambayo hupatikana mwilini, iliyojirundika baada ya muda mrefu.
 
5- HUSAIDIA KATIKA UBONGO NA KUTIBU KANSA
 
Matango hua na vitamini ambazo husaidia kukumbuka mambo kwa haraka, na kuchochea uwezo wa kutunza kumbukumbu. Unashauriwa upendelee kuwapa watoto wako matango kuchanganya na ndizi mbivu hiyo itawasaidia kuwa na akili na kufanya vizuri darasani na katika shughuli mbalimbali za kibunifu.
 
Tango lina virutubisho kama Lariciresinol, Pinoresinol na Secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.
 
FAIDA NYINGINE ZA JUMLA:
 
Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

(Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo
Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure).
Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari.
Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho Sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu.
Tango lina kiwango kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure.
Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue).
Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).
Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango  kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji.
Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu.

KIUNDANI KUHUSU MMEA WA MTANGO HAPA: CUCUMBER
 
AINA ZA MATANGO: Zipo aina nyingi sana za matango ambayo hulimwa duniani lakini kuna aina kadhaa za begu za matango ambazo zimefanya vizuri hapa Tanzania nazo:
- Palmetto.
- Chicago
- Straight 8
- Colorado
HALI YA HEWA NA UDONGO: Matango hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto kidogo pia hustawi.
Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C – 25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi husababisha magonjwa kwenye majani na maua.
Kwa ustawi mzuri wa matango, udongo unatakiwa kuwa na rutuba ya kutosha, na chachu ya kuanzia 5.5 hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa ni kuanzia mita 1000-1200 kutoka usawa wa bahari. Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji.
Tofauti na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu maua na matunda, au mmea kwa ujumla.
UPANDAJI WA MATANGO Upandaji Zipo aina mbili za upandaji, 1.ya kwanza ni ile ya kupanda mbegu moja kwa moja na 2. ya pili ni ile ya kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10.
Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi. Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei itatumika Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda.
Matango huhitaji kupandwa wakati wa jua. Huu mmea unahitaji joto na maji mengi. Mbegu hupandwa kivyake kwanza karatasi lililo na mchanga na kutunzwa kabla ya kupandwa shambani. Mara nyingi matango hupandwa moja kwa moja shambani. Wakulima wengine hupanda kwenye vitalu au makopo na baadae kuhamishia miche inapofikia sentimita 8-12. Endapo mbegu zimepandwa shambani moja kwa moja, inatakiwa ipunguzwe na kubakia mche mmoja tu kwenye kila shimo.
Baada ya wiki moja mbegu zako zitaanza kuota, endelea kunyunyizia maji kila siku na baada ya wiki mbili hadi tatu mimea itakua na kuanza kutaka kutambaa. Mbegu hiyo humwagiliwa maji mara kwa mara kwa wiki tatu. Baada ya wiki tatu mmea huwa umetokea kwa mbegu hiyo hivi basi ni sawa kuupeleka shambani.
Kabla ya kupeleka mmea huo shambani, hakikisha kuwa umechagua pahali ambapo pana jua. Hakikisha mchanga huo una rutuba nyingi, ni vyema kumwita mtu aliye na ujuzi wa mchanga ili kukueleza kama mchanga huo unaweza kuzwa matango.
NAMNA YA UPANDAJI WA KISASA:
Changanya rutuba na mchanga hadi inchi nane chini. Weka mimea yako midogo ukihakikisha umezitofautisha kwa inchi kumi na mbili. Unapopanda mimea hakikisa umefunika mchanga na neti ii kuzuia wanyama au wadudu ambao hula mmea mdogo.
Hakikisha umeangalia mmea wako kila siku. Ili kupma kiwango cha maji ingiza kidole chako kisicho na maji mchangani kila siku, unapoona kuwa hakina maji katika mgawanyo wa kwanza wa kidole chako basi mimea yako inahitaji maji.
Wakati mzuri wa kunyunyuzia maji ni wakati wa asubuhi au masaa ya mwanzo wa mchana. Unaponyunyizia mmea huo hakikisha kuwa hununyizii matawi yae bali mchanga. Ni vyema kuchunguza kiwango cha maji kwani matango yasiyoshughulikiwa na maji huwa na ukali kiasi unapoliwa.
NAFASI: Nafasi kati ya mche na mche ni sentimita 60-70, na nafasi kati mstari na mstari ni sentimita 70-90. Mimea inatakiwa iwekewe miti ili iweze kuzaa matunda mengi na kuepuka kukaa chini ambapo matunda yanaweza kuoza au kuharibiwa na wadudu.
MBOLEA: Mbolea ni muhimu sana, kabla ya kupanda au kuhamisha miche. Mbolea inayoweza kutumika ni samadi au ya viwandani isiyokuwa na madhara kwa mazingira na afya ya binadamu. Baada ya kupanda, tumia mbolea ya maji maji kila baada ya siku 14-21, mpaka mmea uweke matunda.
Jambo la kuzingatia ni kuongeza rutuba katika mchanga. Baada ya kuongeza rutuba na kabla ya kuweka mmea katika mchanga, unafaa kungoja hadi wiki moja iishe kisha uongeze rutuba kila baada ya wiki tatu. Unaweza kuongeza rutuba ya mimea ambayo imeoza na kuchanganya na vyakula ambavyo umeviweka hivi basi vinaoza.
Rutuba nyingine ambayo unaweza kutumia ni kemikali unazonunua dukani, aina hii ya rutuba inafaa kuangaliwa kuwa kiwango chake cha nitrogen kiko chini nacho kiwango cha potassiumu kiko juu. Rutuba huwekwa kwa changa kando ya mmea, Unaweza kuweka ikiwa katika njia ya maji maji au mchanga mchanga.
Hakikisha kuwa hujaweka rutuba nyingi zaidi ya ile inayofaa  kwani jambo hili husababisha mmea kutoongezeka katika urefu. Pia waweza Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda na kisha tumia NPK yenye uwiano mmoja kama, 18:18:18, 17:17:17 ama 16:16:16 baada ya wiki tatu toka Usegekaji. Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza.
PALIZI: Palizi ni muhimu , ili kuepuka magonjwa na kunyang’anyana chakula kati ya zao na magugu. alilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Njia nyingine ni matumizi ya plastiki maalum kuzuia magugu yaani ‘plastic mulch’
Baada ya mmea kufikisha inchi nne, kata pande zake ambazo hazina maua. Unafaa kuweka majani kwa mchanga ili kuzuia mchanga usipoteze maji ambayo yanahitajika na mimea yao. Ni vyema kunyunyizia matango na maji ya sukari ili kuhakikisha nyuki zinafika kwa mimea hiyo na kuongeza maua.
Kuna uwezekano kuwa matango yako yasitoe matunda kwani maua yote ni ya aina ya kiume, ili matunda yatokee inafaa maua ya aina yote ya kiume na kike yawe yakimea pamoja. Unafaa uwe na uvumilivu kwani jambo hili laweza kuchukua muda kabla ya kutendeka. Kuchelewa kwa matunda kunaweza kusababishwa na kutowasili kwa nyuki katika mimea yako pengine kwa ajili ya hali ya hewa au baridi. Ndiposa unashauriwa kupanda matango wakati wa jua. Sababu nyingine ni kuwa umenyunyizia dawa ya kuwauwa wadudu.
MATANDAZO (MULCHING) Baada ya kupalilia na kuweka mbolea weka matandazo (mulch). Mkulima anaweza tumia nyasi au mabaki ya mimea mingine kufunika ardhi, baada ya miche kutambaa kwa kiasi unaweza weka matandazo kwaajili ya kuzuia upotevu wa unyevu, kupunguza uotaji wa magugu na pia matandazo yakioza huongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko.
Kita miti (staking) ya kupandia: Chomeka miti ya kupandia matango yanayotambaa. Hii husaidia matango yanayotambaa kupanda kufuata miti uliyoikita/chomeka. Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza.
UCHAVUSHAJI. Hii ni muhimu sana kuzingatiwa kwani tango huchavushwa kwa wadudu na si upepo, Bila wadudu kama nyuki uzalishaji huathrika sana, Ni muhimu kupanda mazao kama alizeti na maua mbali mbali yanayopendwa na wadudu wachavushaji ili kuhakikisha uwepo wa wadudu hao shambani.
Aidha inapolazimu ni vema kuweka mizinga kadhaa ya nyuki katika shamba la tango Matumizi ya viuatilifu Katika udhibiti wa wadudu na magonjwa matumizi ya viuatilifu yafanyike kwa maelekezo ya wataalam.
MAKALA KWA MSAADA WA:
Wikipedia
Anzisha project: (Here)
Tiba asilia (Natural Herbs